Mei 2005, Fortaleza – Brazil.
Hapo ndipo kazi ya kweli ilianza –
kuchimba handaki. Wale jamaa wa Alemão walikuwa na countdown yao kali: lazima wamalize kabla ya tarehe yao ya dhahabu –
Agosti 6, 2005.
Sasa unajua kwa nini waliichagua hiyo tarehe? Si bahati mbaya bwana. Hiyo siku ilikuwa ya kusafirisha
ma-bundle ya noti mbovu kutoka mabenki zingine kupeleka Benki Kuu wakazipige
check. Zile ambazo hazina maana zingechomwa moto. Lakini bado – zilikuwa na thamani mbichi, na mbaya zaidi (au bora kwao),
hakuna rekodi ya serial numbers. Yaani ukishapata, hakuna system inaweza kufuatilia. Pesa safi kabisa, ghost money.
Sasa imagine scene. Hapo
Rua 25 de Março namba 1071, nyumba ya kawaida tu, lakini ndani yake kulikuwa
gateway ya pesa za ndoto. Umbali? Ni kama kuvuka barabara kuu –
Avenida Dom Manuel – basi unakutana uso kwa uso na Benki Kuu.
Handaki walilochimba? Ebu sikia specs:
- Urefu: mita 80 straight,
- Kina: mita 4 chini ya ardhi,
- Kipenyo: sentimita 70 tu – enough kwa mtu kujisukuma kama snake.
Sasa kazi ya kuondoa udongo? Wamepiga
creative cover-up. Udongo wote waliweka magunia, waka-pack kwenye lori. Guess what? Lori limepambwa vizuri na stika za ile kampuni yao fake ya
landscaping. Majirani wanawaona wakitoa tani 30 za mchanga, lakini wanadhani ni “biashara ya bustani inasonga mbele.” Yaani hakuna mtu hata mmoja alihisi kuna kitu kinaenda chini ya ardhi.
Walikuwa wameset kila kitu kama pro project:
- Mlango wa chumba walipoanzia shimo? Waliufunga na kufunika kwa mbao na carpet – hata yule katibu wa kampuni (shemeji ya Alemão) hakushuku chochote.
- Handaki yenyewe? Walipiga finishing safi kama site ya ghorofa: nguzo za mbao zili-support ukuta, umeme ulipigwa connection, kulikuwa na maji, simu, AC na ventilation system kali. Hapo ndani ilikuwa kama mini-office chini ya ardhi, sio shimo la kawaida.
- Wachimbaji waligawanyika zamu tatu – yaani 24/7 shovels zikichapa, mchanga ukipigwa clearing.
Na sasa boss wa finance –
Fernandinho mdogo. Jamaa ndiye alifungua wallet, akadrop
zaidi ya 200,000 reais ili mradi usimame. Bila yeye, hakuna hata spade moja ingeangukia pale chini.
Kwa kifupi, Mei 2005 ilikuwa moto. Waliishi kama watu wa kawaida juu ya ardhi, lakini chini ya miguu yao –
ndoto kubwa ya wizi wa karne ilikuwa inakua taratibu, mita baada ya mita.