PreGE2025 Wizi wa kura; tathmini yangu ya ibara ya 8 ya katiba yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kuelekea uchaguzi mkuu 2025, kumekuwa na mijadala mingi, mkubwa katika hiyo ni vuguvugu la "No reform, no election" lililoasisiwa na CHADEMA.

Yapo madai mengi yaliyotolewa na CHADEMA katika vuguvugu lao hili, miongoni mwao likiwa ni hili la wizi wa kura. Mjadala wa uwepo au kutokuwepo kwa vitendo vya wizi wa kura utakuwa ni mjadala wa siku nyingine, tafakuri yangu ya leo naielekeza kwenye ibara ya 8(1) ya katiba yetu dhidi ya vitendo tajwa.
Kwaajili ya uelewa wa pamoja nanukuu masharti katika ibara hiyo kama ifuatavyo:
8 (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo–
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Kwa muktadha wa masharti haya ya katiba, kura za wananchi ndio ruksa pekee halali anayopewa kiongozi wa serikali kuweza kushika hatamu: Kitendo au jaribio lolote likifanywa na mtu yeyote aidha kutangaza matokeo tofauti na jinsi kura zilivyopigwa, kupunguza kura halali ama kuongeza kura za kughushi katika masanduku ya kura ili kutoa matokeo tofauti na uhalisia wa kura zilivyopigwa; kwa maoni yangu mtu huyo atakuwa:

Mosi: Anavunja katiba kwa kubadili msingi wa madaraka ya serikali, ambapo badala ya msingi wa madaraka kuwa ni wananchi sasa msingi mpya utakuwa ni ujanja ujanja uliofanyika. Hii inaondoa kabisa maana ya uchaguzi na sababu ya wananchi kwenda kupiga kura.

Pili: Anadhulumu wananchi kumweka kiongozi wanayemtaka, badala yake anamuweka kiongozi anayemtaka yeye. Huyu kimsingi sio kiongozi wa wananchi, bali ni kiongozi wa aliyemuweka. Vivyo hivyo hawezi kuwajibika kwa wananchi kama katiba inavyoelekeza, badala yake atawajibika kwa aliyemuweka.

Tatu: Anamdhulumu aliyechaguliwa haki yake ya kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili linachochea hisia za kuona kuna kuonewa na kubaguliwa kwa huyo aliyedhulumiwa na wafuasi wake jambo linaloweza kupelekea uwepo wa uvunjifu wa amani na machafuko.

Mwisho: Kama uchaguzi huo ulikuwa ni wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzinia, kitendo hicho kitakuwa na ukakasi zaidi, maana katika uhalisia wake ni kitendo cha kumpindua rais aliyechaguliwa, ambacho sina uhakika kuwa hakitaweza kuhesabika kuwa ni uhaini hususani ikizingatiwa maana ya sasa ya uhaini iliyopo mtaani.

Rai yangu; wizi wa kura sio jambo dogo la kufanyiwa mizaha kama tulivyowasikia habari za maporini na vibonzo vya halali, nusu halali na haramu; ni jambo la kupigwa vita kwa nguvu zote kama tunayo nia ya dhati ya kujenga umoja wa kitaifa katika nchi yetu. Na katika hili Rais alituonyesha njia walau kwa kuwachukulia hatua waliotoa kauli za kutatanisha.
 
Yapo madai mengi yaliyotolewa na CHADEMA katika vuguvugu lao hili, miongoni mwao likiwa ni hili la wizi wa kura. Mjadala wa uwepo au kutokuwepo kwa vitendo vya wizi wa kula utakuwa ni mjadala wa siku nyingine, tafakuri yangu ya leo naielekeza kwenye ibara ya 8(1) ya katiba yetu dhidi ya vitendo tajwa.

Kwaajili ya uelewa wa pamoja nanukuu masharti katika ibara hiyo ni kama ifuatavyo:
8 (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo–
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Kwa muktadha wa masharti haya ya katiba, kura za wananchi ndio ruksa pekee halali anayopewa kiongozi wa serikali kuweza kushika hatamu: Kitendo au jaribio lolote likifanywa na mtu yeyote aidha kutangaza matokeo tofauti na jinsi kura zilivyopigwa, kupunguza kura halali ama kuongeza kura za kughushi katika masanduku ya kura ili kutoa matokeo tofauti na uhalisia wa kura zilivyopigwa; kwa maoni yangu mtu huyo atakuwa:

Mosi: Anavunja katiba kwa kubadili msingi wa madaraka ya serikali, ambapo badala ya msingi wa madaraka kuwa ni wananchi sasa msingi mpya utakuwa ni ujanja ujanja uliofanyika. Hii inaondoa kabisa maana ya uchaguzi na sababu ya wananchi kwenda kupiga kura.

Pili: Anadhulumu wananchi kumweka kiongozi wanayemtaka, badala yake anamuweka kiongozi anayemtaka yeye. Huyu kimsingi sio kiongozi wa wananchi, bali ni kiongozi wa aliyemuweka. Vivyo hivyo hawezi kuwajibika kwa wananchi kama katiba inavyoelekeza, badala yake atawajibika kwa aliyemuweka.

Tatu: Anamdhulumu aliyechaguliwa haki yake ya kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili linachochea hisia za kuona kuna kuonewa na kubaguliwa kwa huyo aliyedhulumiwa na wafuasi wake jambo linaloweza kupelekea uwepo wa uvunjifu wa amani na machafuko.

Mwisho: Kama uchaguzi huo ulikuwa ni wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzinia, kitendo hicho kitakuwa na ukakasi zaidi, maana katika uhalisia wake ni kitendo cha kumpindua rais aliyechaguliwa, ambacho sina uhakika kuwa hakitaweza kuhesabika kuwa ni uhaini hususani ikizingatiwa maana ya sasa ya uhaini iliyopo mtaani.

Rai yangu; wizi wa kura sio jambo dogo la kufanyiwa mizaha kama tulivyowasikia habari za maporini na vibonzo vya halali, nusu halali na haramu; ni jambo la kupigwa vita kwa nguvu zote kama tunayo nia ya dhati ya kujenga umoja wa kitaifa katika nchi yetu. Na katika hili Rais alituonyesha njia walau kwa kuwachukulia hatua waliotoa kauli za kutatanisha.

Nchi yangu Tanzania, 😢.

Kama kura za wananchi haziheshimiwi kwa nini pesa zitumike kuendesha uchaguzi ambao mwisho wake watu wachache ndiyo huamua kupanga viongozi wanaowataka wao na si waliochaguliwa na wananchi?!
 
Kama wasimamizi wa uchaguzi baada ya kuwaengua waangalizi wa vyama vya upinzani wakabaki wao na mapolisi nani wa kuwazuia kuiba kura na nani atawashtaki?
Be realistic this is Tanzania ambapo mgombea huchagua marefa hata wakiwa ni ndugu zake.
 
Wanapora Uchaguzi halafu wanakuja kujiapisha kuwa watailinda na kuiheshimu Katiba.
Wanamdanganya nani?
 
Kuelekea uchaguzi mkuu 2025, kumekuwa na mijadala mingi, mkubwa katika hiyo ni vuguvugu la "No reform, no election" lililoasisiwa na CHADEMA.

Yapo madai mengi yaliyotolewa na CHADEMA katika vuguvugu lao hili, miongoni mwao likiwa ni hili la wizi wa kura. Mjadala wa uwepo au kutokuwepo kwa vitendo vya wizi wa kura utakuwa ni mjadala wa siku nyingine, tafakuri yangu ya leo naielekeza kwenye ibara ya 8(1) ya katiba yetu dhidi ya vitendo tajwa.

Kwaajili ya uelewa wa pamoja nanukuu masharti katika ibara hiyo kama ifuatavyo:
8 (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo–
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Kwa muktadha wa masharti haya ya katiba, kura za wananchi ndio ruksa pekee halali anayopewa kiongozi wa serikali kuweza kushika hatamu: Kitendo au jaribio lolote likifanywa na mtu yeyote aidha kutangaza matokeo tofauti na jinsi kura zilivyopigwa, kupunguza kura halali ama kuongeza kura za kughushi katika masanduku ya kura ili kutoa matokeo tofauti na uhalisia wa kura zilivyopigwa; kwa maoni yangu mtu huyo atakuwa:

Mosi: Anavunja katiba kwa kubadili msingi wa madaraka ya serikali, ambapo badala ya msingi wa madaraka kuwa ni wananchi sasa msingi mpya utakuwa ni ujanja ujanja uliofanyika. Hii inaondoa kabisa maana ya uchaguzi na sababu ya wananchi kwenda kupiga kura.

Pili: Anadhulumu wananchi kumweka kiongozi wanayemtaka, badala yake anamuweka kiongozi anayemtaka yeye. Huyu kimsingi sio kiongozi wa wananchi, bali ni kiongozi wa aliyemuweka. Vivyo hivyo hawezi kuwajibika kwa wananchi kama katiba inavyoelekeza, badala yake atawajibika kwa aliyemuweka.

Tatu: Anamdhulumu aliyechaguliwa haki yake ya kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hili linachochea hisia za kuona kuna kuonewa na kubaguliwa kwa huyo aliyedhulumiwa na wafuasi wake jambo linaloweza kupelekea uwepo wa uvunjifu wa amani na machafuko.

Mwisho: Kama uchaguzi huo ulikuwa ni wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzinia, kitendo hicho kitakuwa na ukakasi zaidi, maana katika uhalisia wake ni kitendo cha kumpindua rais aliyechaguliwa, ambacho sina uhakika kuwa hakitaweza kuhesabika kuwa ni uhaini hususani ikizingatiwa maana ya sasa ya uhaini iliyopo mtaani.

Rai yangu; wizi wa kura sio jambo dogo la kufanyiwa mizaha kama tulivyowasikia habari za maporini na vibonzo vya halali, nusu halali na haramu; ni jambo la kupigwa vita kwa nguvu zote kama tunayo nia ya dhati ya kujenga umoja wa kitaifa katika nchi yetu. Na katika hili Rais alituonyesha njia walau kwa kuwachukulia hatua waliotoa kauli za kutatanisha.
Samia yeye hatambui haya, anaamini katika wizi wa kura, sasa imagine mtu kama huyu anapata wapi courage ya kuongoza wananchi?
 
Back
Top Bottom