DOKEZO Wizi wa mita za maji, mita hizi zinapelekwa wapi?

DOKEZO Wizi wa mita za maji, mita hizi zinapelekwa wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

chaz beezz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
217
Reaction score
865
Zimepita siku mbili sasa sina huduma ya maji, hii ni baada ya kuibiwa mita ya maji na wezi usiku. Walifika wakafungua mita ya maji kisha wakaondoka nayo, tumekuja shituka asubuhi tunakuta maji yanamwagika kwa wingi sana kucheki mita imeng'olewa.

Sijui hizi mita zinapelekwa wapi na istoshe zimesajiliwa kwa majina ya muhusika, ili limekuwa tatizo sana hapa mtaani. Mimi ni kama muhanga wa tano sasa kukumbwa tatizo hili na hasa mita zilizo nje ya uzio wa nyumba zinaibiwa sana.

Nilitoa taarifa kwa mwenyeketi wa mtaa ninapoishi ili niweze pewa barua ya kwenda nayo idara ya maji ili nipewe mita nyingine, kufika idara ya maji wanadai nitoe laki mbili ili kuwekewa mita mpya.

Hii imekaaje wakuu, mbona Kama napigwa? Ndio taratibu zilivyo kweli?

Pia soma: Albert Chalamila: Sijaridhishwa na hiki mlichofanya DAWASA, pia wanaoiba Mita za Maji washughulikiwe

√ - Dar: Emmanuel Kalungwana kortini kwa wizi wa Mita za DAWASA
 
Zimepita siku mbili Sasa Sina huduma ya maji hii ni baada ya kuibiwa mita ya maji na wezi usiku walifika wakafungua mita ya maji Kisha wakaondoka nayo.Tumekuja shituka asubuhi tunakuta maji ya amwagika kwa wingi Sana kucheki mita imeng'olewa...
Hi sio poa asee, huenda inarudishwa ilipotoka
 
Kweli maisha yamekuwa magumu na kuongezeka kwa watu ni mtihani mwingine

Enzi hizo mita hakuna anaegusa siku hizi hata taa ya Treni wanaiba sasa jiulize ataiuzia kampuni gani

Zamani ukikutwa navyo utajuta kuzaliwa
 
Zimepita siku mbili sasa sina huduma ya maji, hii ni baada ya kuibiwa mita ya maji na wezi usiku. Walifika wakafungua mita ya maji kisha wakaondoka nayo...
Ni wapi huko mkuu?
 
Hizo ni dili sana huwa zinaadimika alafu itokee mtu anahitaji kuunganishiwa maji na dawasa hawana kinachofanyika ndicho kilichofanyika kwako
 
Back
Top Bottom