Wizi wa mtandao: Akaunti za Twitter za Bill Gates na Elon Musk zadukuliwa, mamilioni ya dola yaibiwa

Wizi wa mtandao: Akaunti za Twitter za Bill Gates na Elon Musk zadukuliwa, mamilioni ya dola yaibiwa

Ni ndani tu ya saa moja lililopita, wadukuzi wamefanikiwa kuingilia faragha za akaunti za Twitter za Bill gates na Elon Musk na kutuma ujumbe ukiwataka watu watume kiasi cha pesa kwa njia ya bitcoin kisha, Watatumiwa mara mbili ya hiko kiasi.
Mashambulizi yamekua makubwa maana kila Twitter wakijaribu kufuta ujumbe, wadukuzi hufanikiwa kuja na ujumbe mwengine, wenye taarifa kama hiyo.
Hadi sasa USD 8 millioni zaidi ya billioni 20 zimeshaibiwa(yaani ndani ya saa moja tu). View attachment 1508007View attachment 1508008View attachment 1508009

Dah. Yaani nimesoma huu uzi ghafla kale kasoundtrack ka “la casa de papel” kakaanza kupiga kichwani [emoji23]

O bella ciao, Bella ciao,bella ciao, ciao,ciao,ciao,
O’ partigiano, portamina
 
Ila hawa wadukuzi wana akili sana, kwanza akaunt za Twitter za hao matajiri wawili zinaamikika na zaidi ziko verified.

Pili, ni vinara wa teknolojia na kwa kuwa njia yenyewe ya kutuma ni kimtandao na inahusisha bitcoin, kufuatilia mwenendo wa hiyo miamala sio kazi ndogo.

Mara zote nasema wahalifu wakati mwingine wanatumia akili ya kiwango cha juu sana kufanikisha mambo yao.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Wajinga hawaishi mjini
Yaani umpe mtu hela ili akupe mara mbili yake kwa nini asikupe tu?
... ajabu sana Chief! Mtu just online; humjui hakujui hata kama anatumia ID ya mtu maarufu, anakuambia nitumie pesa na wewe unatuma lazima uwe na ugonjwa wa akili sio bure.
 
Ila hawa wadukuzi wana akili sana, kwanza akaunt za Twitter za hao matajiri wawili zinaamikika na zaidi ziko verified.

Pili, ni vinara wa teknolojia na kwa kuwa njia yenyewe ya kutuma ni kimtandao na inahusisha bitcoin, kufuatilia mwenendo wa hiyo miamala sio kazi ndogo.

Mara zote nasema wahalifu wakati mwingine wanatumia akili ya kiwango cha juu sana kufanikisha mambo yao.
... lakini na sie raia sometimes tuna tatizo. Hata kama ni message from a person like Bill Gates ya kutuma pesa kwenye akaunti au kwa means atakayokuwa amei-specify will it be OK kwa mtu mwenye akili timamu kutuma pesa simply 'Bill Gates' kasema tuma? Tena ndani ya muda mfupi wameshapiga mamilioni!
 
Hapo ndio akili kubwa nnayoiongelea ilivyofanya kazi sasa. Kukuzubaisha tu ilimradi upagawe na kupigwa
 
Wamemkamata mpopo Hushpup na wahauni wenzie nikajua wameisha.Kumbe kuna wababe bado wapo duuh hatari.

Serikali iwakodi hao akili mingi wamkamate mbaya wao Kigogo wanafeli wapi.
 
Any security system is as strong as its weakest link. For twitter, its employees and internal access system is its weakest link.

Poleni sana wakuu. Uzuri watatoa report nili dunia nzima ijifunze fro their mistake.
 
Ila hao scammer inabidi wapongezwe kwakweli
Hackers need to get it right only once, wakati security professionals need to get it right everytime.

Pamoja na kwamba social engineering imetumika (udhaifu wa kibinadamu wa wafanyakazi wa twitter kutokukagua kila kitu mara mbili mbili kuhakikisha ni sahihi) bado hao scammers wamefanya kazi kubwa mno.

N ujinga wa bitcoin ndio huu, hiyo hela hakuna anayeweza kuitrace wala kuizuia. Ingekiwa mfumo wa kawaida wa kibenki hiyo scam isingekuwepo.
 
Ule msemo wa waswahili kila mbabe na mbabe wake umedhihirika hapo jana baada ya matajiri wa Dunia ku hakiwa account zao na vijana wa Bitcoin. Mpaka sasa matajiri hao wamekuwa katika hofu huku vijana hao Wakiwa na taarifa za matajiri hao zenye thamani ya mabilioni ya dola. Hizi ni baadhi ya ujumbe zilizotumwa na hao ma hackers , Na kushtusha mamilioni ya watumiaji wa Twitter hapo jana...
51ACF033-C44B-4EC2-936E-A2500AD31A85.jpeg
 
Back
Top Bottom