Wizi wa nyota

Wizi wa nyota

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Karibu binti na mwana wa Afrika.

Nyota ni nini?.

Lugha za dini, huita bahati, Neema, upako, n.k Kinyume chake ni mikosi, laana, gundu, nguvu za mapepo wabaya, bahati mbaya.

Lugha za kidunia, Ni Zali, nyota, bahati. Kinyume chake ni gundu, laana, nyota chafu, n.k.

Kila jamii ina amini kama, kila mtu ana nguvu isiyoonekana ambayo inamuwezesha kujikinga na matokeo mabaya ( mikosi ), au kumsaidia kupata matokeo mazuri ( bahati ).

Kiasili ina maana ya mtu mmoja kununua hatima ya mafanikio ya mtu mwingine. ( kuuza mikosi kwa kununua Bahati ). Yaani kumpa mtu mikosi na yeye kukupa bahati.

Usilazimishe akili kufafanua utanielewa mbele.

Visa vya kuibiana nyota au kununua nyota. Havijaanza leo vilikuwepo hasa katika kizazi/zama za Yakobo, yule wa Biblia.

Ipo hivi.

Isaka alizaa mapacha wawili, Esau na Yakobo.

Neno mapacha ni kumaanisha watu wawili waliokuwa wameshibana, lao moja, watu walioaminiana mno.
Esau alikuwa ni mtu wa pilika ( muwindaji ), wakati Yakobo alikuwa ni mvivu ( home boy ) kwa lugha ya biblia ina mwita mtoto wa mama, sawa na lugha ya kihuni ya leo.

Neno mfugaji linamaanisha alikuwa ni muweka hadhina ( bank leo) wa Esau
( sawa na Yuda alivokuwa muweka hadhina wa Yesu, naye kwa tamaa akamuuza Yesu). Kwa yuda hawajatumia neno mfugaji sababu enzi za Yesu walitumia pesa kama leo, lakini enzi za Esau walibadili mali kwa mali.

Sababu ya tamaa ya kumiliki mali, alizomtunzia Esau, Yakobo alienda kwa mganga (Mama).
Mganga akasuka mpango wa Kununua Nyota ya Esau.

Sawa na matukio yanayofanyika leo, matukio ya kununua na kuuza nyota.
Katika biblia wametumia neno kununua ukubwa, yaani kununa hatima.

Ukichukua kitu muhimu, cha mtu bila ridhaa yake ni wizi.

Ila ukimshauri akupe kwa ridhaa, sababu ya faida fulani atakayopata toka kwako. hiyo ni biashara
Biashara ni kununua na kuuza, Unanunua kwa gharama ndogo unauza kwa gharama kubwa.

Esau aliuza ukubwa ( hatima/ nyota/ bahati) kwa kupewa chakula.

Anayenunua nyota si mganga/mnajimu, Ni watu wetu wa karibu. mtu ambaye ukiambiwa huwezi kuamini. Sababu ni mtu muhimu kwako, ndiyo maana biblia ikatumia neno mapacha.

Na anayeuza ni wewe mwenyewe, nyota ya mtu huuzwa na mlengwa.

Mwenye kuitaka nyota yako, ni lazima akutafute ili umuuzie, Sababu kiroho bahati ya mtu ina mamlaka na mtu mwenyewe. Yaani bahati ya mtu haiwezi kwenda kwa mwingine bila muhusika kuridhia.

Mfano. mimi na wewe tunauza mchele kwenye meza moja. Mimi kwa siku nauza gunia mbili, tatu, wewe ukijitahidi sana ni gunia moja.

Hata siku nisipokuja kuuza, wewe utauza vilevile gunia lako moja. Ila nikikwachia gunia zangu mbili uniuzie, na kweli uanze kuniuzia, basi siku hiyo utauza gunia zako zaidi ya unavyouza siku nyingine.

Inatokea hivyo sababu, umetembelea nyota yangu, baada ya mimi kutoa ridhaa.

Sababu nyota inachukuliwa kwa lidhaa, hivyo wachukua nyota utumia njia za kukulaghai wewe.

Atatafuta fedha kwa jasho lake. haruhusiwi kutumia ela ya mkopo, ya kupewa, wala isiyotokana na jasho lake.
Kisha hiyo fedha ataipeleka kwa mganga. ( Yakobo alimpa mama mfugo ili amwandalie baba)

Yaani Yakobo alimpa mganga fedha ili aiandae kwa ajili ya kuchukua baraka alizo barikiwa Esau.
Hiyo fedha ikitoka kwa mganga, ndipo unapewa.

Mtu anayetaka kukuchukulia nyota, atakupa fedha moja kwa moja. Heidha kwa kukopesha kama anasaidia au kukupa kama mtaji. Sababu ni lazima nyota aichukulie kwenye biashara. kupitia faida.

Uhalisia. Bank zote zipo chini ya IMF Bank. inayoendeshwa na ILLUMINAT, ndani ya Freemason.
Luminat / luminus ni neno la kilatini, lenye maana ya Nuru, Wakati Lucifer ni enye kusababisha Nuru, Mwana wa Nuru, ndani ya biblia ( shetani ) ndio maana kwa kilatini cha biblia Lucifer wanaifafanua kama shetani.

Ina maana Illuminat ni watangaza shetani. Hivyo kutengeneza mfumo wa Kifedha ili wakukopeshe, lengo ni moja.

Pesa yao ina nguvu ya shetani. Ndiyo maana mikopo yao ni mateso kwa watu.

Iwe umekopa kwa mtu binafsi, taasis, saccos, Kausha damu, au popote, ambapo pesa ina riba.

Ni sawa na umemkopa Luminat, yaani umeuza ukubwa wa bahati yako, ukubwa wa hatima yako kibiashara. zile alama za freemason kwenye hela si alama tu zina maana na nguvu.

Rejea kauli ya yesu kuhusu pande mbili za fedha. Angalia maisha ya wakopaji wengi wakubwa na wadogo.
Huanza kuyumba baada ya kukopa.

Jiulize kwa nini maandiko yanapinga riba, yalijuaje ya kausha damu leo?.

Si ktk hizo taasisi tu hata mitaani, watu wanakopa hawaoni matokeo, mpaka wanajihisi ni gundu.
Sio gundu chunguza, nani kakupa hela ya bure, nani kakukopesha hujamlipa, nani kakupa mtaji, na aliutoa wapi. nani kakupa ya riba. wengine si misaada , umeuza nyota yako.

Namna Wanunuzi wanavyojua nyota yenye nguvu, ( kubwa).

Wanaangalia mahusiano yako na watu.

unapendwa, una wateja kwa unachofanya, vingi kati ya unavyopanga na kufanya vinafanikiwa.
Na vingine vya kuonyesha kuwa ni mwenye bahati nzuri.
(Oanisha na mashart ya watoa mikopo).

Tuwe pamoja.

Sisi ni Afrika sisi tu umoja.
 
WIZI WA NYOTA

Karibu binti na mwana wa Afrika.

Sehemu ya pili.

Post iliyopita nilikujuza jinsi wezi wanavyopima nguvu ya nyota yako.
Na nilikuanzia katika kisa cha Biblia.
Leo nahamia katika uhalisia.

Nyota ndiyo imebeba hatima ya kila mtu.
Hivyo kila mtu na kila kitu kina nyota yake. ( mfano ngekewa, nyoka, kinyonga, Bundi, kuku,nk.)
Freemason, wanajua nguvu na umuhimu wa nyota ya kila kitu, ndiyo maana huwezi kujiunga/ kukuunga kama nyota yako haieleweki.
Asiye amini Freemason ipo na ndiyo inayocontro Dunia na wenye vipawa, ( vipaji/nyota ). Akasikie wimbo wa paschal Kasiani.

Freemason ndiyo walioshikilia mifumo yote ya kuitawala Dunia, iwe kidini, kisiasa, achilia mbali uchumi na sanaa.
Siri ya Nyuma kwa wanaotamani kujiunga, Hiki chama hakitoi hela kama wengi wanavyodhania, bali wanakufundisha jinsi ya kumudu maisha kwa kipawa ulichonacho, yaani nyota yako.

Maeneo ambayo ndiyo hasa hutumika na wezi wa Nyota.
Ni katika misaada.
Wezi wa nyota hutoa misaada ya bila masharti katika raha.
Ukiona mtu fulani anapenda kukusaidia, eneo la mtaji, eneo la sherehe, lakini eneo la msiba magonjwa haonekani. Chunga anaweza akawa.
Ndiyo maana huji kusikia Tajiri, maarufu, Kaenda kutoa msaada msibani, Hospitali, Maeneo hayo ni magumu kununua nyota.
Ndiyo maana uji kusikia sumu imeuwa watu, msibani na katika sherehe za kijamii.
Ukiona mtu anataka kujua sana, habari za biashara yako hasa upande wa mauzo. chunga anaweza akawa.
Ukiokota pesa njiani, usijione ni mwenye bahati. Nyingine zimetegwa na nakusihi, Usiwahi jaribu kuichanganya na mtaji kwa namna yoyote.
Wenye bahati huwa hawazioni, wala kuokota. Ukiwa naye atakwambia okota wewe.
Ukiona mtu kama msanii, kakupa msaada wa mtaji. Kamwe usiifanye kuwa mtaji, utauza nyota.
Wasanii wengi hugawa pesa, ambazo si zao.
Kuna Majitu yana pesa nyingi freemason, hivyo yanaweza kumtumia msanii kusambaza hizo fedha. Kwa lengo la muhusika kuwa ameuza nyota.
Jiulize hao wasanii wanaogawa pesa, hawana watu muhimu.
Unafanya biashara inaenda vizuri kisha anakuja mtu anakwambia, eidha nikuongezee mtaji, au tuchange mtaji na mwisho wa siku tutagawana mtaji. chunga si wote wana lengo hilo.
Ukiona mtu anakuja katika Biashara yako na kutaka kukuongezea mtaji, labda kwa sababu kaona una mtaji mdogo. Utauza nyota.
Kubwa zaidi na Gumu.
Kamwe usichukue mkopo wa aina yoyote ili ukaanze Biashara hata kama mkopo hauna riba.
Kila pesa ya mtu inaendana na jasho la mwenye pesa. Haiwezi ikakupa matokeo.
Wengi ambao hizo pesa zinaleta matokeo, wanazipandisha thamani kwa damu za watu.

Wewe unapotafuta pesa, huwa una mipango, hiyo mipango ndiyo, manuizo yako, na wengine hunuiza kabisa.
Na wengine si kunuiza kwa uzuri, ni kwa kila pesa yake inapopita itavuta pesa nyingine. Mtu huyo akikupa pesa yake uwezi fanikiwa wewe, yeye ndiye anafanikiwa.
Tukirudi katika Maandiko, Kutoa sadaka ni kuhitaji upendeleo toka kwa Mungu, Ndiyo maana wanaojua hilo kila sadaka atakayo toa atahitaji baraka za pesa ambayo hakutoa.
Hilo kila mtu analo iwe kwa kujua au kwa kutojua.
Kwani we ukitoa sadaka msikitini/kanisani unataraji nini?.

Wengine wapo mbali zaidi, wamatoa sadaka ya mtu, ili kupata pesa.

Hitimisho:
Aliyeuza nyota, ni ngumu kupata fedha ya ziada, sababu Mungu anajua unahitaji kula ili uishi.
Aliyeuza nyota, hupata pesa sawa na tatizo lililopo mbele yake.
Na utokea hivyo eneo la Tukio.
Yaani utaangaika kutafuta pesa ya marejesho, magonjwa, ila unaweza kuipata siku mgonjwa anakaribia kufa, au siku ya marejesho.

Utafanyaje kama upo katika haya.
Mungu ndiye wa kwanza, katika hili.
Muombe wewe kama wewe, akusamehe na kukutakasa.
Kama una madeni weka lengo la kulipa na hata ukiweza lipa.
Usiogope kuanza upya kwa fedha yako mwenyewe.

Kisha utachukua ndimu moja.
Kama we ni wa meditation kaa kama una meditate, kama siyo, kaa mkao unaotumia kusali, kama siyo kaa katika kiti cha asili.
Kata hiyo ndimu kati kati, kisha shika kila mkono mmoja kipande kimoja.
Kisha Muombe Mungu wako aliyeumba Ndimu abariki nguvu zilizo katika ndimu zikusafishe.
Maji ya ndimu nayo yana nguvu za kuchukia uchafu, wako kama ulisemewa vibaya, kama ulifungwa, kama ulifubaishwa nyota. Vyote vinakutoka.
( Somo langu lilikuwa kuuza nyota kufubaishwa ni jambo lingine, Hili hufanywa na wake zetu, ingawa nalo linamahusiano na bahati/ mvuto wako ilo somo lingine ).
Ukisha kumuomba Mungu wako akusafishie nyota na manuizio mabaya ya watu.
Kwa kila mkono utakamulia hivo vipande vya ndimu kwenye chombo, kwa pamoja ukiwa umekaa hivohivo. Ukiendelea na manuizo yako.
Kisha kunywa hayo maji ukisema Imekwisha.
Ndimu, huondoa mikosi, kurejesha nyota, kisafisha nguvu hasi za kulishwa au za kunenewa, mbali na kusafisha nyumba, kugundua mtu muongo, au kujua kitu kibaya, kama paka na viumbe wanaoweza kutumiwa vibaya.

Tuwe pamoja.

Sisi ni Afrika tu Umoja.
 
Kuamini mambo ya nyota ni ushirikina
 
Nimekupata mkuu..
 
Mambo matano ambayo yanaweza yakapelekea nyota yako ikachukuliwa au kufifishwa kirahisi ni yafuatayo;

a) kufanya ngono hovyo hovyo na watu mbali mbali ni rahisi kupoteza nguvu kubwa ya kiroho katika mwili wako, lakini pia ni rahisi kuibiwa au kufifishwa nyota ya yako. Kupitia ngono ni rahisi kuwekewa vikwazo na kuletewa changamoto nyingi,, kwa sababu manii zako zikichukuliwa na kufanyiwa mambo mabaya ni rahisi ubaya kukupata.

b) kusahau nguo yako nje nyakati za usiku na kuivaa ni rahisi kuibiwa au kufifishwa nyota yako, kwa sababu kiza kinapoingia nguvu ya kiroho inatawala, hivyo ni rahisi watu wabaya kuifanyia mambo mabaya nguo yako,,

c) kuazimana nguo na kuvaliana nguo sio jambo zuri kinyota, kwa sababu mtu akinuia kukufanyia ubaya kupitia nguo yako ni rahisi ubaya kukupata.

d) kupitia salamu ya mikono ni rahisi mtu kuififisha na kuiba nyota yako. Hapa nazungumzia salamu ya mgusano wa viganja vya mikono

e) nyota yako inaweza ikafifishwa au kuibiwa kupitia pesa,, kwa sababu unapompa mtu pesa kwa njia ya mkono, kama ni mtu mbaya ni rahisi kuifanyia mambo mabaya pesa yako ili uchumi wako ushuke.,, hivyo mtu akiwa anahitaji msaada wa chakula ni bora umnunulie chakula kuliko kumpa pesa mkononi, au kama kuna uwezekano wa kumtumia kwa njia ya benki au simu ni bora ufanye hivyo.

Nyota yako ndio funguo ya maisha yako

Nawatakia siku njema wapendwa.
 
Back
Top Bottom