Kisusi Mohammed
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 563
- 470
Habari za majukumu wanajamii,
Habari hii ni kupata uzoefu zaidi, kutahadharishana na kuwekana sawa wakati huu mgumu wa uchumi wa kati.
Nimekutana na matukio mawili kwa nyakati tofauti ya kuibiwa na wahudumu wanaotoa huduma ya kuweka mafuta katika kituo kimoja cha mafuta cha TOTAL kilichopo Oysterbay (pale ambapo kuna vituo pacha katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na mataa ya kwenye makutano ya kuelekea St. Peter, kile kilichopo upande wa FAO, upande ambao kuna JANGID BUILDING).
Mara ya kwanza nilimgundua muhudumu kuwa ameanza kunijazia mafuta hali ya kuwa kwenye pampu kulikuwa kunasomeka Tshs 5,000 ambayo inaonekana alimuwekea mteja aliepita na hakutoa risiti, nikamueleza alichofanya na akakiri kosa lake na kuniwekea mafuta yangu ya Tshs. 5,000 nikaridhika na kimoyomoyo nikasema kuwa haya ni matokeo ya malipo duni kutoka kwa waajiri na ugumu wa maisha, mara ya pili leo (ambayo imenilazimu kuandika uzi huu mrefu), muhudumu kama kawaida kanifanyia ujanja wa kuniita pampu ya mbele halafu baadae akabadili mawazo na kuniambia nisogee nyuma ili aniwekee kutokea pampu ya nyuma (kumbe hii ilikuwa janja yake ya kunifanya nisiweze kusoma vema pale kwenye pampu).
Nami kwa haraka haraka nikakumbuka nilichofanywa mara ya kwanza, nikashuka kwenye gari na kuwahi kusoma kwenye pampu, nikakuta keshaanza kuweka mafuta na kwa sekunde kama 5 tayari pampu imeshafika Tshs 12,000, nikamwambia dada najua umeanzia kwenye elfu 10, akataka kubisha na kuwa mkali, nikamwambia ntakuharibia kazi yako kwa sababu ya Tshs. 10,000 naomba uniwekee mafuta yangu kama pesa niliyokupa. Akataharuki na kuniwekea mafuta yangu yote kulingana na pesa niliyompatia, kwahiyo kwenye pampu ikasoma Tshs 10,000 zaidi ya ile pesa niliyompa aweke mafuta na risiti nikapata ikiwa na Tshs. 10,000 zaidi.
SOMO KWA WAMILIKI WA KITUO
Tafadhali sana wamiliki wa vituo hivi, siwaingilii kwenye biashara yenu ila ni vema kuwashauri kwa ustawi wa biashara yenu: Wale wahudumu sio waaminifu, fanyeni uchunguzi wenu na mkibaini hilo chukueni hatua stahiki, kwa sababu haya wanayoyafanya yatawaharibia biashara zenu na kuleta mdororo. Walipeni vizuri, wapeni mazingira mazuri ya kazi, hakikisheni mnaweka mashine nzuri zinazosomeka kwa ufasaha bila shida.
USHAURI KWA WATUMIAJI WA HUDUMA HII
Tuwe makini wakati wa kuwekewa mafuta, tuhakiki kuwa namba zote kwenye display ya pampu zinaanzia sifuri (zero) kwenye Lita na Kiasi cha pesa. Ikiwezekana tusikubali kuwekewa mafuta mpaka tushuke na kuhakiki kuwa pampu inasomeka vema na inaonesha inaanzia sifuri. Tusiwaamini wahudumu, nao ni binadamu, wanaingiwa na majaribu na vishawishi. Kuna mbinu nyingi za udanganyi kwenye hizi pampu tushirikishane ili tupambane na kuumizana huku ambako hakuna sababu. Tumuogope Mungu na kusema ukweli wakati wote, ikiwezekana unapokutana na uovu kama huu ukomeshe kwa njia yoyote inayowezekana ili kuwaokoa wengine na udhalimu huo.
Ahsanteni sana