Wizkid ajaza ukumbi wa 02 Arena

kwa takwimu ya faster faster wanigeria wanaoishi huko ughaibuni ni wengi kuliko wanaafrika mashariki wanaoishi huko na ukichangia na majamaa wanavyopenda vya kwao ndo maana kinatokea kitu kama hcho
 
Wabongo uchawi mwingi. Watakuja mbio kukubishia. Ila mwanzisha uzi kuhusu wizkid watakubali kwa vigeregere kabisa
Wabongo sijui ni laana inatusumbua...kwanza uliza uingereza kuna wanaijeria wangapi plus mataifa mengine ya west africa....so kwa msanii toka west africa siwezi shangaa...wa kumshangaa ni Diamond kuisimamisha east africa kila anakoenda
 
Wasanii wengi wa bongo wakienda mbele wanapiga show zao sebuleni tu..au bar
 
Columbiahalle Berlin..With a capacity of up to 3,500 standing places, it is spacious and at the same time very intimate. It offers a good view of the stage from all perspectives. A seating of the main hall is possible, as well as on the balcony level...O2 20,000 capacity..Tunajua mnampenda Mondi ila msimfananishe na Wiz
 
Ata kiba alijaza sema hapendi kujionyesha
 
Sijasema diamond ni sawa na Wizkid sema mtoa mada anavyosema tunakwama wapi? Wakati Kuna mtu kama diamond anajitahidi kufanya makubwa
 
Sijasema diamond ni sawa na Wizkid sema mtoa mada anavyosema tunakwama wapi? Wakati Kuna mtu kama diamond anajitahidi kufanya makubwa
Mzee Baba tunataka siku moja Mond afanye hivi pale 02 Dunia itajua kuna raia anaitwa Mond kutoka Tz. Ni Davido tu na Starboy ndio waliwahi kujaza pale. Hao tu Wiz karudia tena na kafanya vile vile Sold out all ticket. Imagine afrika nzima vichwa viwili tu ndio vinauwezo wa kujaza.
 
Wana roho mbaya kupitiliza. Wabongo hawataki mwingine atusue. Hawajui wizkid mpaka hapo alipofikia,anapata sapot kubwa sana kuanzia kwao Nigeria.
Kizuri kinajiuza mzee Wizkid yupo juu anaiwakilisha vizuri Africa nzima na sapot anaipata kila sehemu si Nigeria tu sasa jiulize anatumia ndumba au ni nn kinamfanya apendwe sana
 
Wabongo tunafeli kwenye lugha, tunakidanganya kuwa tunakuza kiswahili lakini tunadanganyana.

Tuanze kuuimba kingereza kwanza
Lugha siyo sababu mzee mpangilio mzuri wa mashairi beat nzuri na ubunifu kwenye wimbo wako unatoboa kila sehemu.. mfano Latin America, marehemu Dj arafat, Stromae hata Nigeria asilimia kubwa wanaimba lugha yao Igbo kuna namna tu ila lugha si sababu
 
Kwahiyo Tz hatuna ubunifu mkuu?
 
Kwahiyo Tz hatuna ubunifu mkuu?
Ubunifu wa level za kawaida kama ungekuwa ni wa high level wala isingehitaji nguvu ya maneno na promo kujulikana duniani.. no disrespect mi mwenyewe nafurahishwa na wasanii wengi wa Bongo wanafanya vizuri mfano Marioo, Nandy, Maua sama wengi siwezi kuwamention wote mziki umepiga hatua sana bt kufikia hatua za kina Wizkid we have to something extra kuna kitu inabidi kiongezeke kama tumeridhika na hizi tour za ndani its okay its good music ila kufikia level za wizkid inabidi tufunge mkanda
 
Lugha siyo sababu mzee mpangilio mzuri wa mashairi beat nzuri na ubunifu kwenye wimbo wako unatoboa kila sehemu.. mfano Latin America, marehemu Dj arafat, Stromae hata Nigeria asilimia kubwa wanaimba lugha yao Igbo kuna namna tu ila lugha si sababu
Mzee, watu kama hao huwa wana hit na ngoma moja au mbili basi, dj Arafat alikuwa anaimba kingereza lakini pia hakuwa level za kina wizkid na davido,

Hebu nitajie mnaija aliyeimba ki igbo mwanzo mwisho akatoboa..

Wasanii wetu hawajui kuimba kingereza. over
 
Nachofahamu huwa wana changanya kidogo. Mfano Ojuelegba ya Wizkid ina kingereza na mchanganyiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…