Wizkid vs Man Fongo

Mi pia namkubali sana mwamba geu, chuma nondo steel wire, kuliko man fongo (promo zinambeba sana). Sholo anajua, magoma kama sembe tembele, sayona, sina msaada, panya, geto, kazi kazi (kolabo na prof jize) zote ni noma. Ana amsha amsha sana kiukweli
Wahuni nna gheto langu
Mashosti wanalala
Masela wanalala...

Hivi watu wanaielewa Singeli kweli au wanafurahia kelele? Hakunaga kama Mwamba Geu...
 
Wahuni nna gheto langu
Mashosti wanalala
Masela wanalala...

Hivi watu wanaielewa Singeli kweli au wanafurahia kelele? Hakunaga kama Mwamba Geu...
Mwaga maji tucheze kama kambale
Mwaga tena mwanangu kama kambale

Huyu sholo wamuache tuu kama alivyo, yeyote anaejua singeli na kuifuatilia atakua anajua wazi kua sholo anajua kuliko huyo man fongo. Sholo hakopeshi, ni amsha amsha mwanzo mwisho tangu enzi zile wakati anatoa ngoma kwa dj tito, kabla hata ya kuingia kwa mesen
 
Kuna huyu wa kuitwa Dullah Makabila na ngoma yake ya kuitwa Tabia Yake.
Ngoma nyingine kali kutoka kwa S Kide mtoto wa mama shamte. Fongk anakalishwa sana maana anajisahau.
 
mi simjui huyo sholo mwamba..ila kama yupo bas Single moja ya Man fongo imehit kuliko album ya sholo
 
sholo mwaba anajua sana
aloimba proffesor J
na kile kiamsha amsha chake cha " mwaga maji tucheze kama kambale"
salute zake...
manfongo namkubali kwenye "msingi kiuno"
 
et umalaya wa waTz
ni kweli lakini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mi simjui huyo sholo mwamba..ila kama yupo bas Single moja ya Man fongo imehit kuliko album ya sholo
Ignorance yako kuhusu Muziki haitengezi odds, 'hit' ni tofauti na muziki mzuri...
Inawezakana Man Sifongo kaja kuhit, ni vema na haki. Mwamba Geu ni nabii wa huu muziki, nadhani ndio msanii wa kwanza kufanya mradi wa maana kwenye Singeli, kurekodi kisasa, kutoa video ya kisasa na kuwavuta wasanii Wakongwe na Wakubwa kwenye Singeli.
Shollo ni Mwanamageuzi, akina nyie hamfuatilii huu muziki, mnasikia makelele ya kwenye magrupu ya WhatsApp na mitandaoni...
Tutasema yote lakini mwisho wa siku mwaga maji tucheze kama kambale!
 
Tutasema yote lakini mwisho wa siku mwaga maji tucheze kama kambale!

Mwaga tena mwanangu kama kambale...

Mi siwashangai wasiomuelewa sholo maana mwenyewe kwenye 'geto' kuna sehemu kasema mshamba hawezi kuelewa
 
mi simjui huyo sholo mwamba..ila kama yupo bas Single moja ya Man fongo imehit kuliko album ya sholo
Basi huna sababu ya kubishania usichokijua mkuu, tunaofuatilia vizuri singeli kabla hata haijatoboa kwenye media tunajua mwamba Geu ndio fundi wa hizi kazi. Kama humjui sholo naweza kukutumia ngoma zake kuanzia panya, sayona, sina msaada, sembe tembele, geto na kadhalika, na za huyo man fongo kama ile hauna, tekenya na kadhalika afu ulete mrejesho hapa
 
Weka tena tunamageto,tunamageto

We mwamba nna geto langu

We ndani zuri, we mlangoni kuna msuli
 
In Fwakti Man Fongo anapotezwa na wengi tu, pamoja na Mtoto wa Mama Shamte, Dogo Nigga na kadhalika.

Mkuu sidhan hata kama unaemtajia anajua hawa watu, maana inaonekana wazi sio mfuatiliaji mzuri wa hizi ladha. Pale S kide mtoto wa mama shamte aka mdogo ake dangote au sharobaro wa kwanza kuvaa singlendi ya mikono mirefu na ngoma kali kama Mbagala, huku Dogo Nigga (simela) na migoma kama mida ya kubeti, toroka uje na kadhalika. Man fongo wa kawaida sana
 
miziki yao haifanani hata chembe.....Wizkid ni level nyingine.
 

sasa wewe unauliza swali na kujijibu mwenyewe....
 
Unampeleka Messi Portugal, unadhani atashangiliwa zaidi ya CR7?
 
eti wizkid ft man fongo au man fongo ft chris brown
mambo gani haya ya kutiana aibu
kwanza ndio wewe au sio wewe ?
Umerudi lini huku
kwanini ulipotea ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…