Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Mod Msiunganishe huu Uzi tafadhari.
Kutokana na kile nilichokiona jana kuhusu Diamond na Wizara ya Habari,Sanaa na Utamaduni kumuandalia kikao Diamond na timu yake inadhihirisha waziwazi kuwa wasanii wa Bongo fleva hawana umoja.
Hivi karibuni mtakumbuka kuwa kumetokea upepo wa kufungiwa nyimbo za wasanii hao wa muziki lakini aliyejitokeza na kupiga kelele zilizowachoma BASATA na Waziri Muhusika,ni Diamond peke yake huku wasanii wengine wakijitenga na kusemea pembeni huku msanii kama Nay wa Mitego muda mfupi baada ya tamko la Waziri Mwakyembe na TCRA juu ya alichokisema CEO wa WCB,Diamond akapost kijembe kwa Diamond kwa mipasho kama ya Kina Isha mashauzi ...."Pale unapojifanya mjuaji" maneno yaliyo ambatana na picha ya katoto kamebanwa na mti akimaanisha Diamond kujifanya mjuaji kwa kumpinga shonza hadharani kumemfanya abanwe na Serikali."
Post ile ya Nay imeonyesha us.nge wa wasanii wa bongo fleva....wivu....chuki. .woga....utegemezi yani wanasubiri wasemewe na mtu kwenye haki zao au wanafurahia pale mwenzao anapokuwa kwenye wakati mgumu.
Mwisho kabisa Diamond atabaki kuwaonyesha njia wasanii wenzake kwa kila kitu,sasa ujuaji na kelele zake zimesaidia mpaka kupelekea serikali kumuandalia kikao maalumu cha upatanishi,wakati wengine wakiendelea kulialia pembeni.
Wito kwa Wasani:Msisubiri mtu aje awasemee mnapoonewa shikaneni mikono piganieni haki zenu,hakuna wa kuisemea sanaa yenu isipokuwa nyie wenyewe sio mpaka UVCCM waje kuwasemea la sivyo mtazidi kuonewa na kuona kama Diamond anapendelewa vaeni ujasiri,tumieni vipawa vyenu kukemea mabaya mnayotendewa...ila mkiendelea na vichuki,viwivu na woga wenu sitoshangaa kuona mnaendelea kuburuzwa...mtakuja kushangaa na siku Clouds watakapokuja kukaa meza moja na Diamond na kufikia muafaka huku nyie mkiendelea kulipwa laki mbili kwenye show za Fiesta.
Ni mimi Chinga One wa Jamii Forum.