Wolper amwangukia Mkongo

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
BAADA ya hivi karibuni kumchana laivu Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa Kongo, Mwami Rajabu, staa wa Bongo Movies , Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kumwangukia jamaa huyo na kumuomba msamaha.

Kikizungumza na Risasi Mchanganyiko , chanzo makini kilidai kwamba baada ya gazeti ndugu na hili kuripoti habari ya Wolper kumchana Mkongo huyo huku akidai hana hadhi ya kuwa naye , wiki iliyopita alionekana kwenye Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki jijini Dar ambako ndipo alipofikia mwanaume huyo.

Kiliendelea kueleza kwamba mwanadada huyo alifika hotelini hapo kwa ajili ya kumuomba msamaha Mkongo na alikuwa akifanya jitihada kubwa ili asamehewe kwa kumtumia mwanamuziki wa FM Academia , raia wa Kongo, Patcho Mwamba amuombee msamaha.

"Nimemuona Wolper akiwa na huyo Mkongo kwenye hoteli hiyo aliyofikia ambapo kilichompeleka ni kuomba msamaha kutokana na maneno aliyozungumza kwenye gazeti ," kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo kutoka kwa chanzo, kwanza alitafutwa Patcho Mwamba aliyedaiwa kusumbuliwa na Wolper akimtaka amuombee msamaha kwa Mkongo huyo ambaye ndiye aliyemuunganisha naye ambapo alikuwa na haya ya kusema : "Siyo kweli kwamba Wolper anaomba msamaha mpaka sasa , kwani ameshasamehewa na wako vizuri kabisa kwani siku ile gazeti lilipotoka tu usiku wake tulikutana na Mkongo wakayamaliza ."

Kwa upande wa Mkongo alipoulizwa kuhusiana na habari hiyo alisema ni kweli Wolper alikuwa hotelini hapo akiomba msamaha huku akisema kwamba hakuwahi kuzungumza maneno kama hayo yaliyoandikwa gazetini hivyo aliamua kumsamehe.

Mkurugenzi wa Mwami Foundation , raia wa Kongo, Mwami Rajabu . "Nilimsamehe na sasa sisi ni marafiki wa kawaida tu siyo kimapenzi kwa sababu mimi nina mke na watoto sita na ninamuogopa sana mke wangu halafu hapa Tanzania sijaja kutafuta wanawake bali nimekuja kwa ajili ya biashara lakini nawashangaa hawa wasanii wa kike kunipakazia kwamba mimi nina uhusiano nao.

"Ipo siku nitafunguka mengi na watakoma kumendea waume wa watu , " alisema Mkongo .

Kujibu tuhuma hizo , Wolper alisema : "Watu wanasema sana lakini hakuna anayejua mimi na Mwami tukoje , kama ni bosi wangu au ni
bwana wangu. Labda kama mtu aliniona nasalimiana naye akadhani nilikuwa naomba msamaha. Hakuna kitu kama hicho."


GlobalPublishers
 

Attachments

  • 1414567757829.jpg
    52 KB · Views: 2,493
Watu wana roho ngumu jamani!!!Eti huyo ndiye anayegombewa.....shida hizi!

we!..hawamgombei yeye,wanagombea pesa zake bana!sura yake unataka kupigia picha!???..hehehehehe

(asante mpo wanawake wenye mtazamo tofauti na huu!)
 
we!..hawamgombei yeye,wanagombea pesa zake bana!sura yake unataka kupigia picha!???..hehehehehe

(asante mpo wanawake wenye mtazamo tofauti na huu!)

Hahahaaa kweli wanagombea pesa...mjini pagumu sura sio deal..pesa ndio kila kitu
 
Wolper alienda hapo double tree tena kuomba kugongwa na kurudiwa ila mkongo alichuna hakuja kuongea nae. Tena alimwambia kwa mara nyingine amheshimu kwani ana mtu wake. Siku hiyo Wolper alijipigisha mipicha anakunywa moet na caption ya raha jipe mwenyewe kumbe alikuwa anapunguza stress za kutoswa
 

Njoo kule bas, utamu wote unaimaliza, aya ebu nifuate kule whatsapp maana presha imepanda binamu
 

hahahaaaaaaaa
kaazi kweli kweli
 

Shoga na wewe mbea balaaa.
Hizi hot hot unazitoa wapi?
Na wewe unabeeeba box.
hizo picha nliziona jamani looo nikajua kaamua kumbe anapunguza uchungu wa kutoswa.
"Usitukane mamba kabla hujavuka mto"
 
Njoo kule bas, utamu wote unaimaliza, aya ebu nifuate kule whatsapp maana presha imepanda binamu

Hivi binamu moet ndo kinywaji eksepensivu cha mabongo movie.....
Mbona wakinywa savanna na heineken hawatudolishii.
Inauzwa sh ngapi?
 
Shoga na wewe mbea balaaa.
Hizi hot hot unazitoa wapi?
Na wewe unabeeeba box.
hizo picha nliziona jamani looo nikajua kaamua kumbe anapunguza uchungu wa kutoswa.
"Usitukane mamba kabla hujavuka mto"

Hahaha box in Dawa amu. Hujui siku hizi umbea uko vidoleni? Ukisutwa ujinga wako. Tumehamia digital idara ya umbea nayo haikubaki nyuma. Alafu hela nasikia anahonga kabwana Mdogo flani hivi
 
Last edited by a moderator:
Hahaha box in Dawa amu. Hujui siku hizi umbea uko vidoleni? Ukisutwa ujinga wako. Tumehamia digital idara ya umbea nayo haikubaki nyuma. Alafu hela nasikia anahonga kabwana Mdogo flani hivi

Yaaani hela za kunywea moet ni za mwingine na hapo kamfata mwingine....
Kama ni hivi bora uendelee kubeba box shoga na mie niendelee kupinda mgongo....
Wolper analeta nyodo mbele ya boss wake anayempa jeuri insta...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…