Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Iyo sheli itakua ile ya africana pembeni ya nmb na ndio tabia yao. Ata mimi kuna siku mafuta ya elfu 40 haya kuchukua round
Wacha nipite hapo na vogue yangu .....hii ukiweka wese kwenye dash board inasoma kiwango cha
mafuta kinachoingia
 
Wabongo bwana .. Sasa wanafhani Wolper atarudi tena hapo? Kitu kidogo sana ila kinaweza kuikost biashara.. Then wakiajiriwa wahindi basi malalamisha tele
Mkuu inawezekana hujafanya kazi na wahindi au uliofanya nao hawakuwa wezi, ila wahindi ni wezi na waongo balaa
 
Wanaofanya hivyo ni wafanyakazi mkuu , ambao kwao cha muhimu ni mshahara wao si biashara inaingiza nini.

Wafanyakazi wa ibongo wengi si waaminifu, biashara nyingi sana wanaziharibu wao, hata kama management iko vizuri.
Mkuu Asigwa je hizo management zinawalipa vizuri hao wafanyakazi wao? Lazima tuangalie pande zote mbili
 
Mkuu umetoa taarifa kama movie vile kumbe tukio lina uhalisia,pole sana kwa shemeji yetu.
 
Wizi mwingine wa kipumbavu tu... hawajui hata kama mtu haangalii moja kwa moja atajua matumizi ya mafuta yameendaje kwa safari anazofanya
 
habari hii ni ya kupikwa sababu gani za kipolisi zinazozuia muharifu kutokutajwa....kama ni wizi kweli wamefanya..? mambo mengine hayanihusu....
 
Taja jina la hiyo sheli wanapoibia watu mafuta
 
Hili lidada hata siliamini.... Hivi uibiwe usitaje jina la hicho kituo cha wese?!?!... Lazima itakuwa story ya kutunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…