Candyscorpion
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 763
- 780
Hahahajhaha humu hmna wasugua kwato lol!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mnatafuta kiki tu, sasa risasi imepigwa wapi hapo! Peleka gazeti la sani.
Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati alinusurika kupigwa risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa kwa sababu za kipolisi) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa mgogoro mzito eneo hilo,
Tukio hilo lilijiri muda wa saa tano usiku Juni 12, mwaka huu ambapo mlinzi wa "sheli" hiyo almanusura amfyatulie Wolper risasi baada ya kutokea sintofahamu kati ya Wolper na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.
“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale 'sheli' akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).
“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.
“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” alieleza shuhuda wa mkasa huo.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, mgogoro mzito uliibuka eneo hilo baada ya msichana huyo kumjia juu msanii huyo ambaye hakukubali, ndipo Wolper akaamua kumvaa mdada huyo na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.
Baada ya purukushani hiyo ya muda mrefu ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.
“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” alieleza shuhuda huyo na kuongeza
Kuona hivyo Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.
Wolper alipotafuta kuzungumzi kadhia hii alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda fulani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.
Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”
“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.
“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.
Source: Bongo Movie
Hata angeweka ya 2500 si ni yake huwezi mpangia bajeti alikuwa anadai haki yakeYani mafuta ya 20 anapga kelele kama kapoteza madolali. Ustaa kaz kwel
Hahahaha mwambie wewWe mama una kwere wewe, pengine hata baiskeli huna humu unajifanya huwezi kuweka mafuta ya elfu 20.
Nina sehemu zangu wanazo kubali hiyo kitu.Kuna kipindi hii ya kuweka kwenye idumu ilizuiliwa.
Vipi siku hizi wanaruhusu tena??
Si wote JF tuna magari, wewe mbona huna ....... na pia usikariri kwa kudhani kuwa na gari ni kuwa na pesa nyingi, ila NI KITU MUHIMU KTK MAISHA YA KAWAIDA. ( Na ndio maana inchi zilizoendelea kumiliki gari ni RAHISI mno kuliko kumiliki nyumba)raha ya JF kila member ana ndinga yake. Hata mimi.
Mafuta unaweka kwenye toyo au daladala?Nawashangaa sana mnaoponda mafuta ya elfu 20, kwanza inategemea kwa wakati huo ana kiasi gani mfukoni, siyo mda wote mtu anakuwa na fedha nyingi taslimu, hata mm binafsi mda mwingine nakosa hela mfukoni naweka mafuta ya elfu 10, nasogea benk ku withdraw, msikariri maisha
Hata hawa wasanii wenyewe hawana hizo fedha mnazodhani wanazo, ni wananchi wa kawaida kabisaaa
Mafuta unaweka kwenye toyo au daladala?
We rofa haukua na haja ya kukopy uzi mzima na kutuumiza macho bwege weeeMnatembelea magari msiyoyaweza kuyahudumia, unatembea na gari geji empty mpaka inakula mafuta ya reserve, halafu unawaka Na kielfu ishirini chako.
Kaka mbona umeghadhabika? Mbona nimesema na mimi nina gari.Si wote JF tuna magari, wewe mbona huna ....... na pia usikariri kwa kudhani kuwa na gari ni kuwa na pesa nyingi, ila NI KITU MUHIMU KTK MAISHA YA KAWAIDA. ( Na ndio maana inchi zilizoendelea kumiliki gari ni RAHISI mno kuliko kumiliki nyumba)