mdundo ngoma sana
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 1,002
- 955
super star na mafuta ya twentee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba lifti ukitoka town niko hapa upanga babyMi mwenye kwenye Altezza yangu siwezi kuweka mafuta ya kimasikini hivyo. Mafuta ya 20,000? Not me.
Upanga ipi? Mi nafanyia kazi Posta mpya.Naomba lifti ukitoka town niko hapa upanga baby
Mafuta ya 20
Bongo ustaa mgumu
Upanga ipi? Mi nafanyia kazi Posta mpya.
Hapa parking ya Chibu dangoteUpanga ipi? Mi nafanyia kazi Posta mpya.
Na oryx oil Tanzania zamani kulikuwa na gapco sijui kama ipo
Mnatembelea magari msiyoyaweza kuyahudumia, unatembea na gari geji empty mpaka inakula mafuta ya reserve, halafu unawaka Na kielfu ishirini chako.
Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati alinusurika kupigwa risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa kwa sababu za kipolisi) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa mgogoro mzito eneo hilo,
Tukio hilo lilijiri muda wa saa tano usiku Juni 12, mwaka huu ambapo mlinzi wa "sheli" hiyo almanusura amfyatulie Wolper risasi baada ya kutokea sintofahamu kati ya Wolper na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.
“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale 'sheli' akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).
“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.
“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” alieleza shuhuda wa mkasa huo.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, mgogoro mzito uliibuka eneo hilo baada ya msichana huyo kumjia juu msanii huyo ambaye hakukubali, ndipo Wolper akaamua kumvaa mdada huyo na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.
Baada ya purukushani hiyo ya muda mrefu ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.
“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” alieleza shuhuda huyo na kuongeza
Kuona hivyo Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.
Wolper alipotafuta kuzungumzi kadhia hii alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda fulani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.
Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”
“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.
“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.
Source: Bongo Movie
Naomba kufahamu iwapo mafuta hamna kwenye kisima kama pump inaweza kuwashwa na mtu akafanya kama amekuuzia mafuta kumbe umelipia hewa maana inawezekana kutokujua kwangu nimeshalizwa sana.Wakiona mtu anakuja na kidumu wanakasirika sana, baadhi ya wahudumu vituoni ni wezi balaa hasa nyakati za usiku, mwanzo nilifikiri wanaume ndio wenye tabia hii chafu lakini siku hizi hata wanawake/wasichana wamekwisha ingia kwenye wizi huo.
Usiku chunga sana, wakati mwingine kituo kinaweza kuwa hakina mafuta lakini wahudunu na walinzi wanakaa hapo kuzuga tu, ukija wanajidai wanakuwekea mafuta kumbe kwenye kisima hakuna kitu!!
Siku moja niliwahi kwenda kituo cha mafuta pale Tabata relini, zamani OilCom - hawa walikuwa ni wezi kweli kweli, niliingia kituoni nikamkuta binti na mlinzi , mwazo nilishituka kidogo baada ya kuona hakuna gari hata moja inajaza mafuta pale, binti alikurupuka kutoka alipokuwa amejibanza akanielekeza kwenye mojawapo ya pumps nikampatia elfu thelathini za kujaza mafuta, baadae nikaondoka kupitia barabara ya Dampo kwenda Magomeni - kufika Kigogo nikaona gauge haijapanda kufikia kiwango ninacho kijua mimi, nikalazimika kwenda kituo cha Mafuta cha Magomeni kujaza mengine tena!!!
Kesho yake asubuhi nikawahi kituo cha Mafuta cha Tabata na kwenda kulalamika kwa mmiliki wa kituo, nilishangaa mmiliki alipo niambia kwamba kituo hicho kilishiwa mafuta kabla ya saa kumi na mbili jioni, hivyo usiku wote kituo kilikuwa hakina mafuta, mmiliki alikuwa muungwana akanirudishia pesa zangu na kuwashughulikia wahusika wa kisa hicho. Hivyo kuweni makini sana mnapokuwa vituoni.
Naomba kufahamu iwapo mafuta hamna kwenye kisima kama pump inaweza kuwashwa na mtu akafanya kama amekuuzia mafuta kumbe umelipia hewa maana inawezekana kutokujua kwangu nimeshalizwa sana.
Zaidi sana nitajuaje kama mafuta hamna kwenye kisima ili nisiingizwe mkenge?
Asante!
Source bongo movie? Aaah ni nilijua kweli, kumbe ni muendelezo wa upuuzi wao. Sasa gari lililozima kwa kuishiwa mafuta alirudi nalo vipi sheli, alilibeba? Kisha baada ya kuona kimenuka akatoka tena nduki na gari, mafuta ya 20000? Fuel gauge ya mark X ni mdebwedo hata ishindwe kusoma kuwa kuna wese limeongezwa? Ama huyu Wolper ni ****** kiasi ashindwe faham km anaibiwa hadi aende, arudi?