Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Kwann hakudai risiti,na yeye anamakosa pia.ili hiyo kesi iwe nzuri kwake angerudi kudai risiti,hapo kama walimuibia lazima angewakomoa, wangetafuta njia ya kubalance.
 


Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati alinusurika kupigwa risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa kwa sababu za kipolisi) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa mgogoro mzito eneo hilo,

Tukio hilo lilijiri muda wa saa tano usiku Juni 12, mwaka huu ambapo mlinzi wa "sheli" hiyo almanusura amfyatulie Wolper risasi baada ya kutokea sintofahamu kati ya Wolper na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.

“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale 'sheli' akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).

“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.

“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” alieleza shuhuda wa mkasa huo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, mgogoro mzito uliibuka eneo hilo baada ya msichana huyo kumjia juu msanii huyo ambaye hakukubali, ndipo Wolper akaamua kumvaa mdada huyo na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.

Baada ya purukushani hiyo ya muda mrefu ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.

“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” alieleza shuhuda huyo na kuongeza

Kuona hivyo Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.

Wolper alipotafuta kuzungumzi kadhia hii alikiri kutokea kwa tukio hilo.

“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda fulani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.

Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”

“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.

“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.

Source: Bongo Movie
Mnatafuta kiki tu, sasa risasi imepigwa wapi hapo! Peleka gazeti la sani.
 
Sifa nyingine zinaweza kukuponza hivi hivi,hawa machangu wakipata jina tu mjini wanakuwa na jeuri sana.
 
Nawashangaa sana mnaoponda mafuta ya elfu 20, kwanza inategemea kwa wakati huo ana kiasi gani mfukoni, siyo mda wote mtu anakuwa na fedha nyingi taslimu, hata mm binafsi mda mwingine nakosa hela mfukoni naweka mafuta ya elfu 10, nasogea benk ku withdraw, msikariri maisha

Hata hawa wasanii wenyewe hawana hizo fedha mnazodhani wanazo, ni wananchi wa kawaida kabisaaa
 
raha ya JF kila member ana ndinga yake. Hata mimi.
Si wote JF tuna magari, wewe mbona huna ....... na pia usikariri kwa kudhani kuwa na gari ni kuwa na pesa nyingi, ila NI KITU MUHIMU KTK MAISHA YA KAWAIDA. ( Na ndio maana inchi zilizoendelea kumiliki gari ni RAHISI mno kuliko kumiliki nyumba)
 
Nawashangaa sana mnaoponda mafuta ya elfu 20, kwanza inategemea kwa wakati huo ana kiasi gani mfukoni, siyo mda wote mtu anakuwa na fedha nyingi taslimu, hata mm binafsi mda mwingine nakosa hela mfukoni naweka mafuta ya elfu 10, nasogea benk ku withdraw, msikariri maisha

Hata hawa wasanii wenyewe hawana hizo fedha mnazodhani wanazo, ni wananchi wa kawaida kabisaaa
Mafuta unaweka kwenye toyo au daladala?
 
Mnatembelea magari msiyoyaweza kuyahudumia, unatembea na gari geji empty mpaka inakula mafuta ya reserve, halafu unawaka Na kielfu ishirini chako.
We rofa haukua na haja ya kukopy uzi mzima na kutuumiza macho bwege weee
 
Angepigwa tu!, Tz kuna watu wengi sana tunafika mil 50 hadi sasa. Huyo tungemuimbia "Haleluya ooh sanah, kwa dakika kumi alafu tungemsahau tukaendelea na majukumu ya kila siku". anyway Atafia mahali pengine km hatabadili tabia yake
 
Kweli super star Bongo ni Msemo halali,mtu una Mark x cc 3000 unaweka mafuta ya buku 20? Hayo si mafuta ya kuweka kwenye bajaji?
 
Si wote JF tuna magari, wewe mbona huna ....... na pia usikariri kwa kudhani kuwa na gari ni kuwa na pesa nyingi, ila NI KITU MUHIMU KTK MAISHA YA KAWAIDA. ( Na ndio maana inchi zilizoendelea kumiliki gari ni RAHISI mno kuliko kumiliki nyumba)
Kaka mbona umeghadhabika? Mbona nimesema na mimi nina gari.
 
Back
Top Bottom