Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Lizzy sometime inaboa bana kuchunguzana maana nikianza kukuuliza maswali mengi utaaanza kuniambia mbona unanichunguza sana
Ila it is better to have aclear picture ya mtu ambaye unaenda kukaa nae sehem au kumvua nguo usije ingia ukakutana na mtu ameweka kisu kiunoni
Sio interview hii useme kila mmoja anakuja na kinotebook kimejaa maswali bali mnajenga urafiki ambao utazaa kufahamiana vizuri.
Nna marafiki zangu wa kiume ambae nawafahamu vizuri sana..kama wamewahi kucheat...kama wana watoto...kama wapo na wazazi wenzao au la...kama sio kwanini....kama wamewahi kuoa....wanywaji au wanatumia sigara/bangi....ukaribu na familia zao...yote haya sio kwasababu niliwakalisha chini na kuwauliza ila kwasababu tumejenga ukaribu kiasi cha kuwa tayari kumegeana sehemu kubwaya maish yetu.Na mimi hua nawaambia ukweli hata kama ni mchachu sababu siwi na mawazo ya ANANITAKA ili nijipake sukari asikimbie.Matokeo yake tunafahamiana vizuri hivyo hata siku akinitaka/nikamkubalia kila mmoja atakua anajua mwenzake ni mtu wa aina gani.