pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Alafu hao hao Word Bank wameshusha 'estimates' za ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka huu, kutoka 6% ya hapo awali Januari hadi 1.5%, baseline. Tukitumia takwimu zao za GDP mwaka jana 2019, Kenya @ $99B na Tz @ $62B ukuaji wa uchumi wa Kenya @1.5% utakuwa sawa tu na wa Tz @2.5%, maanake sote tutakuwa tumeongeza approx. $1.5B kwenye uchumi. [emoji1] Alafu tayari uchumi wa Kenya umekua kwa 4.9%, Q1 2020. Yaani kwa ufupi hawa majirani tunawapiga chenga, chobo na mabao, wao wakiwa uwanjani wameloa jasho hadi kwenye kwato na sisi tukiwa kitandani tukivuta blanketi, huku tukikoroma na kumwaga ute.