World Bank: Tanzania ya 4 Afrika kwa nchi zenye madeni makubwa ya IDA

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Screenshot 2024-09-05 221136.png
Kwenye repoti ya fedha ya Benki ya Dunia inayoishia June 2024 inaitaja Tanzania kama nchi ya 4 kwa nchi zenye madeni makubwa ya IDA. IDA ni taasisi iliyo chini ya benki ya Dunia ila wao wanajikita kwenye nchi 75 masikini zaidi Duniani ikiwemo Tanzania. Mikopo ya IDA hua ni nafuu sana na inalipwa kwa muda mrefu zaidi kuliko mikopo ya benki ya Dunia.

Kwenye orodha hiyo ya nchi inayoongoza kwa Afrika ni Nigeria ikifuatiwa na Eithiopia, Kenya na kisha Tanzania imiwa inadaiwa Dola Bilioni 11.7 ama Trilioni 31.6.

Soma Pia: WB: Nchi 5 zinazokopa zaidi Mikopo ya riba nafuu kupitia dirisha la IDA. Tanzania ya 3

Unaweza kusoma mwenyewe.
 
World bank wavumilivu sana aise mpaka trillion 31.6 alafu bado wametulia tu.
 
...Wacha waisome namba eee... sisiemu mbele kwa mbele🎶🎵🎶🎵
 
Kwenye repoti ya fedha ya Benki ya Dunia inayoishia June 2024 inaitaja Tanzania kama nchi ya 4 kwa nchi zenye madeni makubwa ya IDA. IDA ni taasisi iliyo chini ya benki ya Dunia ila wao wanajikita kwenye nchi 75 masikini zaidi Duniani ikiwemo Tanzania. Mikopo ya IDA hua ni nafuu sana na inalipwa kwa muda mrefu zaidi kuliko mikopo ya benki ya Dunia.

Kwenye orodha hiyo ya nchi inayoongoza kwa Afrika ni Nigeria ikifuatiwa na Eithiopia, Kenya na kisha Tanzania imiwa inadaiwa Dola Bilioni 11.7 ama Trilioni 31.6.

Unaweza kusoma mwenyewe.
Tena kwa mtego huu wa China!
Maana serkali inakopa lakini haifanyi vitu vya maana vya kubadili uchumi!
Ni makelele tu ya uchawa na uchambuzi uchwara wa akina Mkumbo na Kafulila ndo unaotegemewa!
Kusema kweli hali ni mbaya sana! Mpaka Samia condoke madarakani hali itakuwa ya kutisha sana!
 
Maskini hakopeshekiii....
Ukiona nchi inakopa jua ni tajiri na inauwezi wa kulipa hata kwa gharama ya wananchi wake....
 
Mchumi huyu wa Dunia aliwahi kuonya watu kua makini na matumizi ya serikali. Kwamba Duniani hakuna kitu kinaitwa bajeti fedha hazijatosha, hakuna. Serikali siku zote itatafta namna ya kupata pesa ya kutumia kwa njia yoyote kati ya hizi, kupandisha kodi, kukopa ama kuchapicha fedha zaidi lakini lazima wapate fedha za matumizi.

Sasa shida iko kwenye hayo matumizi, ni yapi, ya magari ya v8, ya huduma za kijamii kama shule, barabara, elimu, nk ama ya anasa. Wewe mwananchi ndio utalipia hayo matumizi upende usipende kwa hizo njia 3.
 
Kwenye repoti ya fedha ya Benki ya Dunia inayoishia June 2024 inaitaja Tanzania kama nchi ya 4 kwa nchi zenye madeni makubwa ya IDA. IDA ni taasisi iliyo chini ya benki ya Dunia ila wao wanajikita kwenye nchi 75 masikini zaidi Duniani ikiwemo Tanzania. Mikopo ya IDA hua ni nafuu sana na inalipwa kwa muda mrefu zaidi kuliko mikopo ya benki ya Dunia.

Kwenye orodha hiyo ya nchi inayoongoza kwa Afrika ni Nigeria ikifuatiwa na Eithiopia, Kenya na kisha Tanzania imiwa inadaiwa Dola Bilioni 11.7 ama Trilioni 31.6.

Unaweza kusoma mwenyewe.
Kinachoniuma ni kwamba kwenye ripoti ya CAG hakuna mtu anaewajibishwa.
 
Wale vijana wa mama anaupiga mwingi hutowaona hapa
 
Back
Top Bottom