Siyo kila anayepinga, bali ni wale wanapinga kichawi kama Zito, Tundu Lisu, nk! Hawa hata kama hawavui nguo usiku kwenda kuloga, ni wachawi wa maendeleo ya nchi yetu! Na bahati mbaya yao...wataendelea kuaibika tu, Mungu azidi ibariki awamu ya tano na nchi yetu, amen!
Kwa kuangalia mjadala huu, alisema wazi kwamba kuzuia watoto waliopata ujauzito ni kuwabagua, na kwahiyo sio sahii WB kutoa mkopo utakaobagua hususani watoto wa maskini!
Now tell me: Hivi unaamini kabisa mtoto angalau wa mtumishi anayelipwa Laki 5 kwa mwezi atashindwa kuendelea na masomo kisa kapata ujauzito?!
Hivi unaamini kabisa mtoto wa mfanyabiashara mwenye uwezo wake anaweza kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari wakati private schools zimejaa kila kona?!
In contrast, hivi unaamini kabisa mtoto wa maskini kule kijijini akipata uja uzito wazazi wake watakuwa na uwezo wa kumpeleka private school kama wanavyoweza kufanya wazazi wengine wenye kipato?!
Ina maana hadi hapo hujaona umuhimu wa hoja ya akina Zitto na Wanaharakati wengine?!
Hilo la Tundu Lissu nimeshaliongea sana hadi naona uvivu kurudia rudia lakini itoshe tu kusema kwamba, dana dana za Acacia zilikuwa nyingi kwa sababu serikali haikutaka kumsikiliza Lissu!!
Wakati hoja ya msingi ya Lissu ilikuwa kama kweli unataka kupambana na multinational companies basi serikali ijiondoe kwanza kwenye mikataba ya kimataifa inayowalinda sana foreign investors kuliko host countries, wafuasi wa Magu waka-twist na kusema TL amesema serikali iki-deal na Acacia tutapelekwa mahakamani huku wakitamba mbona hawatupeleki basi!!
Swali ambalo mara zote nimekuwa nikiuliza bila kupaat jibu ni kipi kitakachowafanya Acacia watupeleke kwenye mazingira yaliyopo!!
Tulisema tunawadai matrioni ya shilingi, hadi kesho hata senti tano haijatoka na HAITATOKA!!
Wenyewe wakaahidi watatoa kishika uchumba cha USD 300M lakini hadi kesho hadi senti 5 haijatoka!! Hii inaweza kutoka lakini itatoka kwa kuangalia masharti waliyoweka jambo ambalo ndilo linafanya hadi sasa wasiwe wametoa hata sent moja kwa sababu hatujatekeleza masharti yao!
Sasa kwanini Acacia walileta danadana zote hizo?! Kwa sababu walijua hatuwezi kuwafanya chochote wakati wanalindwa na Mikataba ya Uwekezaji! Lakini kama serikali ingejitoa MiGA (ambayo pia ni risk), Acacia wasingefanya danadana kwa sababu wangefahamu wasingekuwa na kwa kukimbilia!!