Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

• Kampeni yake chafu dhidi ya Tanzania yakwama.

• Benki ya Dunia yaidhinisha Mabilioni ya fedha za kusaidia Elimu alizotaka Tanzania inyimwe.

Saa chache zilizopita Benki ya Dunia kupitia Bodi ya Wakurugenzi Watendaji ya Chama cha Maendeleo ya Kimataifa (IDA) imefanya maamuzi ya kihistoria ya kuruhusu mkopo wa Dola za Marekani Milioni 500 utolewe kwa Tanzania kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu ya Sekondari baada ya mjadala mrefu uliochukua miezi zaidi ya mitatu.

Uamuzi wa Benki ya Dunia umezima kampeni ya kidhalimu iliyofanywa na Mwanasiasa mpuuzi Zitto Kabwe aliyeandika barua kwenda benki hiyo akitumia nembo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka Tanzania inyimwe mkopo huo bila kujali athari zake kwa wananchi hasa wanyonge na maskini.

Zitto Kabwe akishirikiana na mabeberu wanaomfadhili alifanya uharamia kwa kuchochea uongo kuwa Tanzania inakandamiza wanafunzi wa kike kwa kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito ilihali anajua kuwa sio kweli na kuna utaratibu ulio wazi wa watoto hao kupata elimu kupitia programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima, Mpango wa Elimu kwa walioikosa na vyuo mbalimbali.

Hili ni pigo jingine baya sana kwa Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakiichonganisha na kuichafua Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Kitamaifa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa bila kujali athari ambazo wananchi wanazipata kutokana na kuinanga Tanzania ama kukwamisha miradi mikubwa na washirika wa maendeleo.

Katika safari ndefu ya mjadala ambao ulianza tangu Januari mwaka huu wa 2020, Benki ya Dunia imepiga chini msimamo wa mabeberu waliotaka Tanzania inyimwe fedha hizo baada ya kuingizwa mkenge na Zitto Kabwe.

Watu wengi wanaweza kujiuliza kwa nini Zitto Kabwe na wafadhili wake walikuwa wanashupalia Tanzania inyimwe fedha hizo? Ukweli ni kwamba Zitto na wadhalimu wenzake hawakuzuia fedha hizo kwa sababu ya kupigania wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shule kama wanavyodai, bali walishupalia Tanzania isipewe fedha hizo baada ya msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kukataa kukopeshwa fedha ambazo zingeingizwa nchi kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na miradi ambayo haina matokeo kwa wananchi ili baadaye zitumike kwa maslahi ya siasa za upinzani na sio wananchi.

Kwenye hili, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedali Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli inastahili pongezi za dhati kwa msimamo thabiti usiyoyumba na ushindi mkubwa dhidi ya kibaraka Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakipiga tripu kwenda mabeberu hao kufanya kampeni ya kuiangamiza Tanzania eti wakitaka kuiondoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.

Kongole Rais Magufuli, hongera Watanzania wote kwa ushindi huu mkubwa. Zitto Kabwe na washirika wake washindwe na walegee.

Sasa Tanzania itapata Dola za Marekani Milioni 500 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 135 kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu ya Sekondari, kuboresha mazingira ya elimu kwa wasichana na kuinua ubora wa elimu kwa wasichana na wavulana.

Mkopo huu ni wa gharama nafuu na sio fedha za bure. Watanzania watazilipa, lakini sasa watalipa fedha ambazo zinakopwa na kuelekezwa kuwasaidia mamilioni ya Watoto wa Tanzania na sio kwenda kwenye NGO na miradi ya kupitisha fedha zinazokwenda kwa wachumia tumbo akina Zitto Kabwe na washirika wake.

Tunaamini Serikali ya Tanzania itatoa mchanganuo wa fedha hizi zinakwenda wapi na zitawanufaishaje Wanzania.

Kila la kheri Watanzania na pole sana Zitto Kabwe kwa kuangukia pua katika mchazo huu mchafu. Tambua kuwa Mwenyezi Mungu husimama na wenye haki na katika hili amesimama na Watanzania wenye haki na Rais wao mpendwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

Taarifa hii haina uhusiano na siku ya Wajinga Duniani. Ni ukweli mtupu na inapatikana katika tovuti mbalimbali za Kimataifa. Waweza kuisoma hapa kwenye tovuti ya Benki ya Dunia yenyewe [emoji1428][emoji1428] New Financing to Make Secondary Education Safer, Better, and More Accessible for Tanzanian Girls and Boys

Mwl. Damas Masele MPJ
Mkufunzi Mstaafu.
31 Machi, 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie naomba na kwenye tume huru wafanye hivi kudadadek
 
Kwani ni UzitO wa KabwelA pekee ndio alitaka warudi shule hao vipepeo,

Je kama ni mama samia,ndiye aliyemshauri!? Wajua nini!?

Acha kumsifia huyo Kikaragosi wa Ujerumani....
Mwenye siasa za kukurupuka na kujionyesha..
Mkishanasaga huwa mnahangaika sana... ALiyesema wazi ni Zitto, kama kuna mwingine aliesema mafichoni hata wewe utamjuaje? KWENYE UKWELI MSEME
 
Alichotaka Zitto hakijafanikiwa, usipotoshe watu. Zitto kaabika kwa Mara nyingine tena
Aliyeaibika hapa ni nani ?! Yule aliyeapa kule simiyu kwamba hawezi kusomesha wazazi, au huyu aliyepigania wakubaliwe kuendelea na masomo baada ya kuzaa ??!!. .



Odhis *
 
Baada ya sarakasi za kuzuia watoto wa kike waliopata ujauzito kutorudi shule, sasa ni ruksa wanafunzi hao kurudi kuendelea na masomo baada ya kujifungua. ASANTE ZITTO, umewakomboa watoto wa Tanzania.View attachment 1405624

Bila jitihada za Mh. Zitto, wasichana hao walikuwa wanaenda kukosa fursa hiyo muhimu ya elimu. Asante pia KABUDI kwa kupeleka taarifa ya mkuu huko WB
View attachment 1405625
Serikali imeendelea na msimamo wake. Hoja ya serikali imebaki kuwa zipo changamoto zinazopelekea mabinti kupata mimba ambapo katika kukabiliana nazo rasilimali fedha zinahitajika hivyo watoe mkopo huo. Mwisho wa siku ikakubali!

Kipande mlicho kiweka hapo ni cha zamani benki ya dunia ikisema itaendelea kujadiliana na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau ili mabinti wapatapo mimba wasisitishwe masomo pamoja na kutoa elimu juu ya mila na desturi hasi dhidi ya mabinti wanaopata mimba wawapo shule.

Kiufupi Zitto na wenzake wamepigwa KO!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Taarifa Ni kuwa serikali imeiambia Benki ya dunia Sera ya kufukuza wanafunzi wajawazito siyo ya Tanzania. Hata hivyo pesa itaanza kutolewa baada ya uchaguzi was oktoba 2020 kufanyika. Pesa itatolewa kwa mafungu mpaka tathimini ya hela ya awali waridhike
Siyo ya Tanzania, ila inafanya kazi Tanzania..!!
 
Alichotaka Zitto hakijafanikiwa, usipotoshe watu. Zitto kaabika kwa Mara nyingine tena
Hivi wanaccm nani kawaroga?? Serikali imekubali masharti ya Zitto kwa asilimia 100
Na imepiga goti mbele ya wanaharakati
 
Baada ya sarakasi za kuzuia watoto wa kike waliopata ujauzito kutorudi shule, sasa ni ruksa wanafunzi hao kurudi kuendelea na masomo baada ya kujifungua. ASANTE ZITTO, umewakomboa watoto wa Tanzania.View attachment 1405624

Bila jitihada za Mh. Zitto, wasichana hao walikuwa wanaenda kukosa fursa hiyo muhimu ya elimu. Asante pia KABUDI kwa kupeleka taarifa ya mkuu huko WB
View attachment 1405625
Msipotoshe watu wapi wameandika kuwa serikali imekubali hayo masharti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe alikuwa anatafutwa MSHINDI? Binafsi naona MSHINDI ni yule aliyepata sio yule aliyeshawishi zisitoke
Kama matakwa ya Zitto yamezimgatiwa basi ni win win situation!
1.Pesa itatoka baada ya uchaguzi
2.Watoto watakaojifungua kupewa fursa

Hizo ndiyo zilikuwa ni hoja za Zitto na kimeeleweka!
 
Serikali imeendelea na msimamo wake. Hoja ya serikali imebaki kuwa zipo changamoto zinazopelekea mabinti kupata mimba ambapo katika kukabiliana nazo rasilimali fedha zinahitajika hivyo watoe mkopo huo. Mwisho wa siku ikakubali!

Kipande mlicho kiweka hapo ni cha zamani benki ya dunia ikisema itaendelea kujadiliana na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau ili mabinti wapatapo mimba wasisitishwe masomo pamoja na kutoa elimu juu ya mila na desturi hasi dhidi ya mabinti wanaopata mimba wawapo shule.

Kiufupi Zitto na wenzake wamepigwa KO!

Sent using Jamii Forums mobile app
Fedha zonatoka lini?Kama baada ya uchaguzi inamaana hoja mojawapo ya Zitto imepenya kuwa Serikali isipewe fedha hizo kabla ya uchaguzi!

Hilo la kama wamekubaliana kwa masharti gani inabidi tusubiri taarifa kamili,sema serikali nayo ina usiri sana,haiwezi kuweka wazi masharti hayo!
Either way,Zitto deserve credit!
 
Yaani leo makamanda hatujafurahishwa na hii habari kabisa.
Makamanda watakua wanamuonea wivu Mh.Zitto Kabwe maana wao walishindwa kumtetea mtoto wa kike spate elimu .Wakati mwingine Mh.Zitto anafanya mambo mazito kuliko wote waliopo Ikulu aisee.
 
MATAGA baada msifu zitto mnamnanga kwa tarifa yenu zitto kawafunua vibaya na mkawa wapole mkakubali kilichopingwa

“SEQUIP’s design strives to give pregnant girls and young mothers a better chance to complete their education,” said Caren Grown, Senior Director of the Gender Group at the World Bank. “The Bank has stepped up its work to create a new generation of education programs that emphasize safe school environments for girls and boys, including measures that reduce gender-based violence, corporal punishment, bullying, and other forms of violence in and around schools. It gives girls better quality choices and opportunities for completing their secondary education.”
 
Back
Top Bottom