World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

Mi niko kwenye abood,naelekea moro,endeleeni ku2pa up2dates wakuu
 
Shukran Dark City kwa kuanzisha hii thread.

Wimbo wa taifa wa Mexico unapigwa kisha Wa-Sauzi..patakua hapatoshiii!!!

Mimi Bafana Bafana kama kawa!

Obuntu kwa jioni ya leo yupo upande wa Mexico
 
Vuvuzela zimelipuka tena wimbo umeisha sasa tusubiri mtanange wenyewe
 
Obuntu kwa jioni ya leo yupo upande wa Mexico


Mhhh, mimi nataka ku-enjoy match. Kwa hiyo nitabaki katikati ila kama SA wakishinda itakuwa poa kwani itaongeza utamu wa mashindano!
 
Nimefurahi jinsi SA walivyojaa kushangilia match.

Blatter keshatoa hotuba yake fupi na sasa Zuma anaongea kufunugu mashindano ya 2010.

Je SA watamudu kuwepo kwenye match nyingine kwa wingi namna hii?


Hata mimi nimefurahi sana na pia hupenda sana kuzisikia nyimbo za Taifa kabla ya kindumbwendumbwe kuanza rasmi. Nawaombea sana RSA washinde leo itakuwa bomba sana.

 
Carlos Pereira amepooza sana - he might be unsure of what lies ahead of him -

We are about to kick off - Vuvuzela lakini ni balaa - Inanikumbusha kelele za Q-Bar

Mpira umeanza
 
Na mpira umeanza swali ni nani atakuwa wa kwanza kufunga goli katika fainali hizi ?
 
What a miss - Dosantos ! Amebaki na kipa

South wameponea chupuchupu
 
Beki ya South bado haijatulia - I can see a goal coming in the next few minutes!

Ab-T (right?)
 
Mexico wanaonekana kuonana shambulio lingine la hatari lakini mpira unaokolewa
 
Back
Top Bottom