World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

Asante sana Preta , mie mwenyewe JF brodas nimependa sana jinsi walivyokuwa wanalichambua soka mpaka imepelekea nizidi kuwa shabiki mkubwa wa hii kitu..Ingawa Argentina na Brasil walinitoa nyongo kidogo ndo mambo ya game haya.
Sina budi kuwapa Spain pongezi zao.
Sikutegemea kwenye mashindano makubwa kama haya kuna mambo ya utabiri kama wa shekhe Yahya
Du Pweza kazua blaa
 
Hivi huyo jamaaa ilikuwaje lakini? ama ndo mzuka kama yule kijana wa Bongo kumkumbatia kaka?
 
tatizo ni kwamba nitatokaje usiku kuanzia leo........!
i wish kama WOZA ingeunguruma hata miezi sita

kuna mtu kaniaga anakwenda kuangalia closure na ni lazima akaangalie kwenye big screen...jamani jamani ni wapi hii inafanyika
 
Preta na wewe acha kutia chumvi. Ushindi wa kisho wapi bana!
Mi nilikuwa nashabikia Wadachi. Niliudhika!
 
haya sasa WC ndo hivyo tena imekwisha pongezi kwa spain kuondoka na ushindi!
swali!!!!!!!je wale waliokuwa wakiaga majumbani mwao kwenda kuwatch WC kwenya big screen for the whole month kumbe waenda kwenye mingo zao itakuwaje??????
 
Thanks preta. It was a memorable WC with new style among all " Vuvuzela " All the best to New WC Champion 2010 Spain esp... goalkeeper- he did a wonderfull job !!! Thank to the Spain Couch, Fans and the host - S.A.
 
Ni pongezi kwa timu nzima ya Hispania, kocha Vicente, na kwa namna ya pekee sana nahodha wao Iker Casillas. Jana Casillas katuonyeshwa kwamba form is temporary but class is permanent. Mwanzo wa mashindano hakuwa katika form lakini kadili mashindano yalivyokuwa yanaendelea kaonyesha kwamba yupo daraja la juu na katika fainali katuonyesha hilo!!! Que viva Espana
 
Yes indeed, once upon time he was also in another wrong team - Man U!
 
asante sana japo siku Brasil walitolewa nilishindwa kuvumilia nikamtandika mtu ngumi...but all in all tumemaliza salama na ninategemea kukutana tena na wewe 2014 huko Brasil
I hope alikuwa shemeji... teh teh teh teh...!
 
timu bora imekuwa bingwa,wanastahili kwa kweli mana waliweka rekodi ya mechi 35 mfululizo kutopoteza,viva spain na kocha wao mwenye mafanikio ambae real madrid walivyomfukuza ikawa kama laana kwao na kupoteza dira wamebeba kombe moja tu toka aondoke la ligi kati ya yote waliyoshiriki,viva vicente del bosque,in you and spain of iniesta,xavi we trust
 
inaenda na ukweli kauli yako,kweli iniesta na xavi wanamsaidia sana huyu messi,ronaldo ni mzuri zaidi ya messi
Labda nianzishe Ubishi mpya.. Nilipokuwa Bongo,kila mtu alinambia Messi is the best player duniani na wakamlinganisha na watu kama Pele,Maradona na Zidanne - nikabisha sana na kusema kweli ni mchezaji bora lakini hana daraja hilo hata kidogo. Kwa uhakika mimi namweka Iniesta, Kaka, Xabi na Robbin kundi moja na Messi.

Tena ukiniuliza mchezaji bora duniani kati yao nitasema Xabi mbele ya Messi.
Je, bado wapo wanaoamini huyu Sunday Juma wa Baca ni mchezaji bora kiwango cha kina Pele?

Baada ya habari, Hakika finals hizi zimenipa picha kubwa sana ya wachezaji wengi ambao kusema kweli sikuwawekea maanani sana siku za nyuma kama Foulan, David Villa, Muller na hakika vijana wetu Gervinho, Gean, Annan na Prince.
 
He inspired his team alot. By the look of things, he seriously meant business. Bahati mbaya nawapa hawa jamaa lakini siyo Ghana wala timu yoyote ya Africa. Mambo hayakuwa upande wao ingawa walijituma sana.
 
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza washabiki wote, mliokuwa mnaishabikia Spain katika hii WC iliyomalizika rasmi leo kwa ushindi wa kishindo. Ni furaha sana wanajamii tulijumuika pamoja katika mchakato wote hadi kufikia fainali. Binafsi ningependa kuwashukuru wakaka wote kwa company mliyotupatia wadada wachache tuliokuwa tukishiriki katika mchakato huu...mlituonyesha upendo na hamkutukwaza...big up to you all....luv ya......:kiss: :kiss: :kiss: :kiss:
Yaani natamani kila siku tungekuwa na WC finals, pamoja na baadhi yetu timu zao vipenzi kupigwa bao mapema lakini tulifurahia sana mashindano haya. Naomba tujiandae 2014 badala ya kuiangalia kwenye TV tufanye mkakati ili tuwe ndani ya RIO ili tuweza kutoa ushuuda uliokamilika.
 
Huyo pweza 40 yake itafika siku akija kutabiri Simba na Yanga.
Ndo atajuwa kuwa Bongo waganga wanaheshimika kuliko makocha.

Lakini yoote 9 bali huyo Pweza kaondoa radha ya Mechi na ya mashindano kwa sisi tunaojuwa mpira.

Lakini kwa wakurupukaji amekuwa kivutio kwao.
 
Back
Top Bottom