Leo ni siku ambayo haiendani na timu ya Brazil ,nyota zakaskazini zinaonekana kuiinamia timu hiyo na kuipa mzigo mkubwa katika patashika ya leo Brazil itaelemewa vibaya sana, na kuonekana pengine hata haina uwezo wakuvuka duru hili ya mwanzo.
Habari za ndani za timu hiyo ya Brazil ni za kukata tamaa huku wakiwa na wasiwasi mkubwa wa kupoteza mechi ya leo ambayo ni ya mwanzo katika gurupu lake ambalo ni G,shuhuda aliepo karibu na timu hiyo amesema kuwa wachezaji wengi wanaonekana kuchoka na wenye kusononeka wakihofia tukio la kushindwa.
Uswahili wangu unaniambia kuwa hayatashuka magoli chini ya mawili na Brazil haitoambulia kitu,ingawa wanaweza kupata kitu kama penalty itakayopotea kwa kutoka nje au kudakwa au kupanguriwa.
Amini usiamini leo watafungwa mawili kwa yai.