Tuseme ukweli tusipende majina makubwa bila kuangalia mchango wao na ushiriki wao kwenye hii timu. Prince Boateng, kwa muda mrefu aliomba kujiuzulu kwenye timu ya taifa ya Ghana, ila alivyoona Ghana inakaribia kufuzu akarudi tena, na hata ile mechi ya kwanza ambayo waliibomoa Misri hakucheza alikuwa benchi na mechi ya pili kule Misri alianzia benchi.
Essien mchango wake naye umekuwa mdogo kwa hii timu, na nani asiyejua kwamba amechuja kias kwamba god father wake Mourhino aliamua kumtema.
Gyan naye anachezea jina, aliamua kufuata hela kucheza ligi za umangani na kukimbia changamoto za ligi za ulaya na hasa alipokuwa EPL, na si ajabu kiwango chake kimeshuka.