Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Headlines za magazeti ya uingereza vp yanasemaje kuhusu [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Suarez]#Suarez [/URL] ?
italy wameonewa
Headlines za magazeti ya uingereza vp yanasemaje kuhusu #suarez ?
Wakuu Victoire, Katavi, BAK, Escardo-bird, Mnyakatari, omujubi, chebi, s.crony, mabesela na kiluvya, nimefuatilia majadiliano yenu kuhusiana na kiwango cha timu za Afrika kwenye World Cup na yamenigusa hasa kujua kuwa kumbe tupo wengi tunaoumia kuona team zetu zikiboronga.
Kuna mambo mawili-matatu nimeyaona kwa upande wangu,
Wachambuzi wengi wa soka wanakubaliana kwamba soka la Afrika limekua technically and physically kwa level ya kimataifa, sehemu ambayo bado ni wachanga ni mentally.
Na hilo ndio tumeliona sana kwenye hii michuano, kuanzia kwenye poor decision making, kupigana, ubinafsi/umimi, kukosa umakini/lack of concentration kama game ya Ghana Vs USA, Ivory Coast Vs Greece, n.k yote haya kwa mtazamo wangu yanatokana na uchanga wa wachezaji wetu up stairs.
Na hili kwa kiasi kikubwa linatokana na waafrika kupenda njia ya mkato, wachezaji wetu hawakukua wakijengwa kisaikolojia zaidi ya kiufundi na ubavu. Wamarekani kama anavyosisitiza Malafyale kila siku, wamewekeza mamilioni ya pesa kwenye shule za soka na taratibu tunaanza kuona matunda yake. Wenzetu wanawajenga wachezaji wao katika hizo aspects tatu, sisi tunategemea vipaji tu.
Jingine ni nguvu ya pesa hasa kwa wachezaji wanaocheza club kubwa za ulaya, wakivaa jezi za team za mataifa yao wanakua kama wamelazimishwa tu, hawana muamko wowote wa kupigania nchi zao kama wanavyofanya wakiwa ulaya, yaani msukumo wao ni pesa tu hakuna uzalendo wala nia ya dhati kupigania nchi zao. kikosi kizima cha Ivory Coast ni mfano wa hili.
Nigeria ilipata mafanikio kwenye kombe la mataifa huru ya Afrika baada ya Keshi kuwapiga chini mastaa kibao wanaocheza ulaya na kujenga team na wachezaji wa ndani na wale wasio na majina makubwa ndio mpaka wamefika hapa or else wangekua kama Senegal tu ya kina Demba Ba. Na kuna mdau katoa mfano wa Cameroon ya kina Roger Milla ya 1994
La mwisho ni siasa tu za ndani ya nchi husika, serikali zinatenga muda ya rasilimali kiasi gani kuendeleza huu mchezo au tunasubiri mpaka team iwe kwenye maji ya shingo ndio rais wa nchi anasema atawapa mapesa na other material things? Au kwenda kuleta makocha wa kigeni kwa pesa lukuki za walipa kodi ili waje kufanya miujiza (njia za mkato)? Na pia role ya CAF, pesa wanazopata, za ndani na za nje kutoka FIFA na mashirika mbalimbali, je zinakua distributed fairly? Au baada ya 10% zilizobaki zinaishia North and West Africa? Kwanini makocha na mastaa wa soka wa ulaya wakija Afrika wengi wanaishia huko? wakija kwetu ni kutembea tu, miradi yote wanasapoti iko west Afrika? CAF hawawezi kulikwepa hili.
Ni mtazamo wangu tu wakuu, lakini bila kuaddress haya mambo, bado tutaendelea kuwa jamvi la wageni kwenye World stage, hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio na kama tumejifunza kitu basi tutakumbuka kuwa "a short cut is often a wrong cut"
cc: Kibunango
Aiseeh hata mimi kimeniuma sana yaan bora hata saivi jana niliumia sana afu ata bora wangefungwa kikawaida yaan penalty kwa dk 91 afu ilitolewa kiajabu ajabu tuu.