World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

10445949_10152920447786679_3292596617912856246_n.jpg
 
messi ni mchezaji bora:

Angalia mambo yafuatayo: Jamaa anaweza kubadili matokeo ya mchezo. Tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea mchezaji wa argentina kufunga katika mechi 3 zote za makundi.

Messi anapocheza ni kama mazoezi, hatumii nguvu nyingi,,hana presha na mchezo, he's an artist.

Messi kama zidane, timu nzima inategemea ubunifu wake, hana kelele sana; anaacha miguu izungumze.

Amekosa kuwa mchezaji bora mwaka huu; lakini yeye halalamiki kama ilivyokuwa ronaldo. Anaacha kazi yake izungumze.

Watu wanamchukia; hana neno yeye anafanya kazi tu. Hadi sasa. Messi 4 - 0 c.ronaldo.

Messi atabaki miongoni mwa wachezaji bora kabisa kuwahi kucheza mpira. Yeye ni daraja la akina;
mario kempes, zidane, di stefano, pele, platin, ruud gullit, ronald de lima, diego maradona.;


messi hatari sana ; hasa anapocheza vs timu unayopenda.

swala la uchezaji bora lililalamikiwa na wapigaji kura ambao hawakua wanakubaliana na matokeo. Fifa ilikuwa inacheza mchezo mchafu wa kubadili matokeo ya kura.
 
haaa! halafu miss chagga huwa ni wifi yangu coz ni dadake na chepuko langu, haya nipe muongozo nimsaidie nini, kabla hujajibu naomba nimuhakikishie miss chaga kwamba nitatoa msaada kwa moyo wangu wote

Anauliza kwanini Nigeria inacheza mechi nyingi? Kisa imeingia 16.

Halafu kwanini iingie 16 bora huku imefungwa 3-2 na Messi??
 
Kwangu Messi ni wa Kawaida sana nikimlinganisha na Ronaldo de Lima ambaye amechukua vikombe vyote ulimwengu, dynamic-anaumia mwaka nje akiingia moto zaid ya jana amehama toka club mbalimbali na zote kabeba vikombe huku akiendelea kuwa mtu muhimu kwa timu husika. So ili Messi afike hicho kiwango basi afanye kama Ronaldo de Lima.
My Perception.

Messi anadharauliwa hapo tu, kukaa team moja kama Giggsy.

Inabidi ahame kama CR7 tujue ubora wake ulipo
 
nilikuwa nawashabikia wakati bado sijatoka nje ya bongo. Hawa watu wanadhani wao ndio waafrika pekee wenye akili, wanadharau nyingi lakini washamba tu. Dada zetu (majority) nao wanatuangusha yani kwa wanigeria ni kama kuku mtetea anayechuchumaa hata bila kukimbia kidogo.

wanaijeria hawafai kabisa huku ughaibuni unaulizwa unatokea nigeria unajibu hapana mimi ni mtz wanasema nyie hamna tatizo. Wanaijeria ni matapeli na wamefanya waafrika tudharaulike sana na wazungu.
 
Messi anadharauliwa hapo tu, kukaa team moja kama Giggsy.

Inabidi ahame kama CR7 tujue ubora wake ulipo

Ni kweli ndg. Sikatai kuwa ni mchezaji mzuri lakini si kwa kiwango kikubwa kama Fifa wanavyotuaminisha. Mf Cr.7 katokea mtaani mpaka hapo alipo huku akileta mafanikio katika timu kwa juhudi binafsi zaid tofauti na Messi ambaye kalelewa Barcelona mpaka anazeekea pale. Mwaka huu Messi hajasaidia timu yake ya Barca kubeba hata kombe la mbuzi.
 
anauliza kwanini nigeria inacheza mechi nyingi? Kisa imeingia 16.

Halafu kwanini iingie 16 bora huku imefungwa 3-2 na messi??

ok sawa miss chagga nigeria wamedraw mechi moja, wameshinda mechi moja na kushindwa mechi hii ya jana. Katika kundi lao iran na bosnia wamefungwa zaidi kuliko wao. Maelezo kwa ufupi ni hayo.
 
Last edited by a moderator:

Ingawa mimi si shabiki wake

1. Little magician/soccer genius
Muda wowote anakufunga hasa pale usipopataraji, anajua ku-dribble mpira vizur mabeki wanaijua habar yake

2. Simple player
Hana muda wa kujipodoa sana mfano new hair cut kila baada ya muda mfupi, hakasiriki sana akifanyiwa rafu mpira wake ndo unawanyamazisha watu

Haya yana mtosha sababu si fan wake kiivo

Ila anabaki best player ever hata asipobeba WC mpaka astaafu

#teamCR7 one man army
 
Ni kweli ndg. Sikatai kuwa ni mchezaji mzuri lakini si kwa kiwango kikubwa kama Fifa wanavyotuaminisha. Mf Cr.7 katokea mtaani mpaka hapo alipo huku akileta mafanikio katika timu kwa juhudi binafsi zaid tofauti na Messi ambaye kalelewa Barcelona mpaka anazeekea pale. Mwaka huu Messi hajasaidia timu yake ya Barca kubeba hata kombe la mbuzi.

CR7 anaangushwa na wachezaji vimeo wa Portugal
 
ok sawa miss chagga nigeria wamedraw mechi moja, wameshinda mechi moja na kushindwa mechi hii ya jana. Katika kundi lao iran na bosnia wamefungwa zaidi kuliko wao. Maelezo kwa ufupi ni hayo.

Ngoja aje kukuuliza kwanini makipa wanavaa gloves kama manesi, stay tunned
 
Kwa hiyo Africa tumebakiza team gani mzunguko wa 16 bora?!

Nigeria tu hadi sasa. Ghana wana nafasi endapo Ujerumani itamfunga Marekani na Ghana imfunge ureno ndo Ghana watapita.
 
kimaneno au perfomance?? henderson,coutinho wameifikisha liverpool second place,hao Ozil na ramsey wameshika 4th place kwa kudra za Mungu kumbuka mmesumbuliwa na everton hadi mechi za mwisho mwisho!

Suarez na Sturridge ndo walifanya unayoyasema. Anyway, tusubiri msimu ujao tuone watakachofanya, yaliyopita si ndwele...
 
Inasemekana Muntari na Boateng wamefukuzwa kikosi cha ghana.

Ntakujuza zaidi
 
Mimi hakuna kitu kilichoniuma kama Ghana kunyimwa lille goli 2010 ambalo Suarez alilitoa kwa mkono likiwa limeshaingia.Halafu Suarez alivyoshangilia Gyan alivyokosa Penalt,Mungu yupo kazini huyu Suarez naombea afungiwe kwa ujinga aloufanya jana.
Na waengereza inawauma Hivyo Hivyo kufungwa kwa mkono na Maradona kushangilia ila wengi tungemshangilia Maradona ndio Football.
 
Back
Top Bottom