World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Unashangaa ubisho wa kibongo? Sasa subiri kifo kuu ianze uone jinsi wachawi (wachezaji wetu) watakavyokuwa wanaiga wachezaji waliokuwa kwenye World Cup. Yaani truly nonsense!

Ile staılı ya Cr7 ya kunyoa ıtaıgwa saana katıka VPL
 
Mbona hapa kwenye TV inasema ni Belgium vs South Korea, hiyo Kenya imekujaje? Yaani hii ni sawa na kumuita Obama Mkenya wakati hana issue yeyote na Kenya.
Origi Baba yake ndio Mkenya yeye kazaliwa Belgium wakati baba yake kashakuwa Raia wa Belgium sasa Kuwa Mkenya inatokana wapi? Kenya Wana Dual Citizenship? Sio Kama ni Hater ila ukweli tu tuwe sawa na kutokea mtu tukasema Model Yule anadamu ya Kitanzania Mama yake au Baba yake ila si Mtanzania.
 


Mbona baloteli anasema yeye mtaliano wakamwambia hakuna mtaliano mweusi au ni tetesi tu?
 
Angalau 40% ya timu za CAF zimevuka .. ni sawa tu na asilimia za timu za UEFA zilizovuka.
 
Mbona baloteli anasema yeye mtaliano wakamwambia hakuna mtaliano mweusi au ni tetesi tu?
Hayo Matatizo ya Wataliano wakubali wasikubali ni Mtaliano Kama kazaliwa Italy au kashakuwa Raia akifunga goli ubongo wao unakuwa Blind baada kumuita Mario wanaumia Marioooooooo! Kwa furaha ila kosa moja watamsakizia yeye sababu mweusi wanasahau kumuita Mario wanaumuita BABATUNDE! Ila still haibadilishi Origi sio Mkenya hata angekuwa wazazi wake ni Watanzania si Mtanzania Kama Raia wa Nchi nyengine ila ni Mdunia au Msayari angekuwa Mkenya angeenda kuchezea Kenya na Kina Wanyama!
 
Labda amekosea kdg ila algeria wanatutia moyo kwa kweli

Nikweli. Mie niliwafuatilia sana katika mechi za friendly walishinda mechi nyingi sana ambazo ziliwapandisha mpaka wakawa timu namba 1 kwa Africa na wakamshusha Ivory Cost.
So nilihisi watapita round hii ya makundi.
 

Yeah ni kweli yaani mwenzewe aji proud hasa mtaliano ofcoz he's italian hata wambague he belong there alafu anajotuma sana na timu inamtegemea
 
Kubadilika bado sana ila Mjerumani ni timu nzuri ila nao Policy zao Mjerumani waliozaliwa Kama wale waturuki na polish wamezaliwa Kule Kule ujerumani England kavuka ujue mjamaica Africa itachukuwa muda ambaye hajazaliwa England sijui Kama itatokea.
 
Nikweli. Mie niliwafuatilia sana katika mechi za friendly walishinda mechi nyingi sana ambazo ziliwapandisha mpaka wakawa timu namba 1 kwa Africa na wakamshusha Ivory Cost.
So nilihisi watapita round hii ya makundi.

Mahodari sasa kwa kweli wametupa uso africa
 
Ni kweli Portugal bado...nilikuwa namkumbuka tu Eusebio!

Ile timu imekufa sana yaani ronaldo haonekani kabisa bwana ronaldo ya ukweli walikua nayo brazil enzi hizo robert carlos na wengine wakali timu ilikua moto wa kuotea mbali ila kina marcelo nao wanajitahidi
 
Urusi nje! Nimefurahi sana! England, Italy, Spain, Portugal...wote waliwahi kuwa mabingwa lakini safari hii walie tu!

Portugal walikuwa mabingwa mwaka gani? Hebu nikumbushe mkuu.
 

Nijuavyo mimi Kenya hawana Dual Citizenship according to wakenya wanavyosema. Mimi nimemwita Origi Mkenya kama kejeli fulani hivi maana wabongo huwa tunawatambua wachezaji wenye wazazi wa Kiafrika kama waafrika. Juzi juzi kuna watu niliwasikia wakiwahesabu kina Benzema, Zidane kama wa-Algeria japokuwa walizaliwa Ufaransa na kukulia Ufaransa. Kitu kingine sisi wabongo tulivyo hutasikia mtoto wa Kibongo aliyezaliwa nje ya bongo mfano UK,Marekani nk akihesabika ni raia wa nchi aliyozaliwa bali ni Mtanzania sababu wazazi au mzazi wake ni Mtanzania.
 
Mbona hapa kwenye TV inasema ni Belgium vs South Korea, hiyo Kenya imekujaje? Yaani hii ni sawa na kumuita Obama Mkenya wakati hana issue yeyote na Kenya.

Hahaha hata wakenya wanamhesabu Obama ni mkenya mwenzao, au umesahau walivyoshangilia ushindi wa Obama na kumlaani kwa nini alikataa kutembelea "kwao kenya"(wakimaanisha Kenya ndo Obama anapotoka)? Mkuu nilivyomuita Origi ni mkenya ni kuendeleza tabia yetu ya kuhesabu watoto waliozaliwa na wazazi wa Kiafrika nje ya Afrika kuwa wanatoka nchi wazazi wanapotoka. Sikuwa serious kuwa jamaa ni Mkenya, najua kuwa Kazaliwa Belgium kama kina Benteke,Lukaku,Dembele nk. Wewe kama una mtoto nje ya Bongo mtoto wako akirudi Bongo jamii itamhesabu ni mbongo japo kazaliwa nje. Hutawahi sikia mtoto wa Mtanzania aliyezaliwa Marekani akaitwa Mmarekani mweusi, watakwambia Mmarekani gani wa Kingoni,Kihaya,Kisukuma,Kizaramo nk. Ndo wabongo tulivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…