World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Hawa Costa Rica vipi tena wanapandaje wote wakati wapo wachache uwanjani na wanaonekana wamechoka kulinganisha na Greece
 
namuona Paulo Wanchope anawahamasisha vijana wa Costa Rica.

Mkuu huyu jamaa alitisha 2006 hasa mechi ya ufunguzi na Germany japo walilala 4-2 lakini alitupia hizo 2 peke yake kama sikosei.
 
Ukiwa unashambuliwa kama hivi dakika tatu zinaonekana kama kumi.
 
Reactions: BAK
Mkuu huyu jamaa alitisha 2006 hasa mechi ya ufunguzi na Germany japo walilala 4-2 lakini alitupia hizo 2 peke yake kama sikosei.

Jamaa alikuwa kifaa cha Derby County enzi za 90s mwishoni.
 
Muda wa mikwaju umewadia. Costa Rica wamejitahidi hata kama wakitolewa.
 
Pressure kwenu #TeamCostaRica msisahau kuminya kende na nanihii 🙂🙂 ili Wagreece wasizione nyavu, kila la heri.
 
Predictions??????? Naona Wagiriki wanaonekana kama wana uhakika na kipa wao kuzuia penati, tusubiri tuone isije ikawa kama England vs Argentina 1998 all over again.
 
Muda wa lawama umefika sasa.

Muda wa kutosahauliwa pindi ukosapo penati ya ushindi, kila mtu anamkumbuka Baggio kukosa penati ya mwisho, lakini hatukumbuki aliyefunga penati ya mwisho ya Brazil 1994
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…