World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Tatizo mkuu Ghana wetu wamepangwa kundi gumu sana hebu fikiria kuna portugal na Germany, Hivi hawa wazungu waliopanga hayo makundi wanatutakia mema kweli? Au kwakuwa wanaogopa moto wa Ghana wa 2010 usije ukawaka tena safari hii?
Labda ujeruman lakini portugal haitishi sana kumbuka hata Ghana wako Vizuri ndo maana wamepangiwa hapo ili kuwapunguza makali ila yote kwa yote nawaombea watutoe kimaso maso
 
Kaka tusubilie mech nyngne ya uholanzi utanipa jibu..spain ufatha mwngi..
Wamejipanga sawa sawa spaini mchezo wao ni ule ule ndo maana hata barcelona siku hizi anapigika vizuri tena ukimbana vizuri gor huwa nyingi kama ulivyoona jana,tusubiri mechi nyingine tuone ila jamaa hawana masihara
 
Mbeleko yenyewe itadunda maana kuna nchi ziko vizuri umesahau south africa 2010 alibebwa mpaka ikashindikana

SA walitolewa uwezo ulikuwa mdogo Brasil ni level zingene zile .Usikarir
 
Hivi hamuifikirii kabisa BELGIUM iliyojaa vichwa kama Hazard,Lukaku,V.Kompany,Fellain n.k au macho ya wengi yako kwa mwenyeji tu? Mi nadhani hii nayo ni moja ya timu za kuangalia kwa jicho jingine
 
Vishabiki vya holland vinafiki...villi kuwa kimyaaaaa vimejificha chimboni Kama michepuko vile kabla holland haijafunga. heeee baada ya holland kufunga vikaibuka Kama dengue from no where kila mtu holland holland....mhh vishabiki maandazi hehehehehe
Very very true
 
Mimi nafurahia Ghana kupangwa kundi la wababe ili kumwezesha kupiga zoezi la kutosha vilevile kumtengenezea mazingira mazuri ya kujipigia vibonde watakaokatiza mbele yake endapo atafanikiwa kupenya hatua hii ya awali. Ni faida kubwa sana kupangwa kundi gumu hatua ya mwanzo ili ukomae kuliko kupangwa kundi mdebwedo ili ubweteke.
 
mkuu humu inaonyesha wengi hawaitakii mema spain ila kufungwa kwa spain leo ndio kunamfanya spain mechi zote ziliobakia anahakikisha anashinda tena kwa magoli mengi spain anapita bila wasi toa shaka

Uko right
 
matokeo jaman jana mechi ya chile nmeishia njiani wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…