World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

BsH-n9HCEAAQqPJ.png
 
Tujuane mapema jamani....TeamHolland


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Tupo tupo mkuu na roho zetu ngumu.dah,sijui itakuwaje leo.sijaiona sana Argentina tangu hii michuano ianze,hivyo sijui tunakutana na nini leo,nasikia watu tu wanaimba messiah,messiah!tutakutana na huyo messiah huko huko ground,kama mbwai na iwe!Holland akipigwa leo,itakuwa mwisho mchungu kwangu kwenye WC hii,manake Italy,England,Ghana,Brazil,Japan,zote out,kabaki mdachi tu,daah!
 
everlenk ,huyu kiumbe anatafuta wa team mess mpeni ushirikiano wangu.

leo mim tutaonana home ukishinda itabidi nikusaidie kushagilia japo nitakuwa upande wa holland.

Hahahahaha!!! Pamoja sana,mechi tamu na ngumu kuliko jana.
 
Last edited by a moderator:
Tuseme tu ukweli ujerumani hawatishi kihivyo,hata jana wala hawakucheza mpira wa nguvu kwamba ndo ukaleta mabao yale,nguvu waliyotumia kucheza na France au Ghana ingetumika jana nadhani mabao yangekuwa 90 maana kila dakika ingekuwa ni goli, Brazil jana hawakuwa teamwork kabisa beki mbovu,wakapanikii wakawa hawawezi tena ukiangalia goli la 2-5 lililovyoingia ilikuwa ni ajabu sana hata kimanzichana shule ya msingi wasingefanya hivyo.

Achana na habari za Mkoloni, naona leo upo team ya ushindi Argentina, halahala tu usije na gundu kama la Katavi
#TeamArgentina
 
Last edited by a moderator:
Angalia tu hiyo pole isije ikakurudia mwenyewe Mkuu

Leo unaondoka unahesabu tiles za nyumba yako swahiba wangu.ngojea uone teh teh!usiweke panadol hapo mezani,weka diclofenac,strong pain killer,Van Persieeeeeee!haya anza kuimba jina hili moja,mbili..kuna looping header nyengine leo teh teh!
 
Hah ha haa! Eti sasa wamehamia team Argentina...loo, mashabiki wa Tanzania kweli hawaeleweki! Wanakimbilia upande ule ule kulikolipuka bomu badala ya kutafuta usalama upande wa pili. Kwa mbali nakumbuka gari la mafuta lilipolipuka barabara kuu ya Tanzania-Zambia, waswahili wakakimbilia eneo la tukio; ngoja wakione cha moto! Hata katika siasa mambo ni hayo hayo; wameng'ang'ania tu hilo gari bovu pamoja na kwamba dereva kapoteza mwelekeo...oh tutatawala miaka 100! Tuna safari ndefu...
 
Leo unaondoka unahesabu tiles za nyumba yako swahiba wangu.ngojea uone teh teh!usiweke panadol hapo mezani,weka diclofenac,strong pain killer,Van Persieeeeeee!haya anza kuimba jina hili moja,mbili..kuna looping header nyengine leo teh teh!

Nakuonea huruma swahiba maana Argentina inahitaji tu Messi kuwa at least 50% fit kumnyonyoa kuku/kaburu kabla ya kumchinja, leo bahati ya kupiga penati hamtaipata, kama Mkoloni tunamaliza biashara ndani ya dk 90
 
Back
Top Bottom