World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Mjerumani kaweka heshima kubwa kamtandika Brazil na Argentina barani kwao! Sio kitu rahisi lazima Hongera tuwape hata Kama wengine hatukutaka ashinde ila Mjerumani kaonyesha Extra Time anaziweza,Fujo anaweza, counter attack anaweza, kukaba anaweza na hawakupendelewa na Refa.
walijua itakuwa Kama ndugu zao Holland..
 
Mkuu Ronaldinho my opinion kila mtu ana zake, kwangu hakuwa effective ni kulinganisha na Messi ndani ya Barca mara nyingi alikuwa ni mchezaji aliyekuwa ana hug mpira zaidi ya kubring team into the play kama Messi anavyofanya. Ameondoka Ulaya akiwa na miaka 30 tu, kacheza ulaya kama miaka 9 in total.

Mh! Kweli kila mtu na opinions zake..kacheza miaka 9 Ulaya katika timu 3 huku akifunga magoli zaidi ya 100 katika timu hizo, halafu unasema hakuwa effective?! Halafu nitajie mchezaji wa kibrasil aliyecheza Ulaya zaidi ya miaka 14! Hao ndio zao, Ulaya wanaenda kutafuta pesa, ikipatikana tu, wanarudi kucheza samba kwao...

Kwani hadi sasa hujasema mchezaji effective anakuwaje? Effective kwa vigezo vipi? Ebu nisaidie katika hili kwanza..
 
Then again. Messi kafanya nini ktk World Cup hii kupewa the Golden Ball? Kuna wachezaji waliwika katika haya mashindano kuliko Messi. Fifa sometimes wana lose credibility.

FIFA under Blatter has lost credibility..
 
Halafu kwanini wamempa manuel neuer golden glove wakati magoli alikuwa anaokoa kwa miguu????kama golden boot kapewa mfungaji bora basi neuer wangemtengenezea hata golden socks
 
majina ndio yanatizamwa hasa kimatangazo Adidas wamefurahi kwa mengi na FIFA!. Pengine hata mchezaji Ghana au Algeria alitakiwa kupata ila anatizamwa Star Mfano FIFA wameshindwa kuumiza kichwa Young Player kapewa Pogba japo nampenda dogo na namuona mkali ila Pogba hakutakiwa kupewa Award kuna Players Colombia walikuwa wapate.

Kwani Messi anavaa ADIDAS? Pamoja na pesa kufanya haya mashindano kuwa mazuri lakini pia pesa inaharibu sana. Kuna wachezaji wengine walistahili kupata hii TUZO kuliko Messi, mfano wangempa RVP au Robben pamoja na ku-dive kwake ningekubaliana na FIFA hapa wamechemsha sana. Katika mashindano haya nilijaribu kumwangalia huyu Pogba lakini sikufurahishwa naye labda in future, kuna young players waliowika kuliko Pogba kama toka Costa Rica, Colombia.
 
Karibu sana everlenk, huu uzi ulikuwa bomba sana tangu mwanzo wa mashindano haya. Ni experience tofauti kuangalia mpira ukiwa na wadau wa JF experience ambayo ilianzishwa rasmi na wapenzi wa teams za EPL. Huu uzi nadhani umeangaliwa na watu wengi sana katika kipindi kifupi cha mwezi mmoja ukilinganisha na uzi wowote ule hapa JF, pia uzi ambao umefika page ya 1172 kwa kipindi kifupi kuliko uzi wowote mwingine hapa JF rekodi ambayo sidhani kama itavunjwa hivi karibuni labda itokee breaking news kubwa sana nchini/duniani ambayo itaitikisa nchi yetu/dunia vinginevyo stats za uzi huu hazitavunjwa mpaka 2018 kule Russia. Hongereni wadau wote ambao mlichangia huu uzi ambao ulitokea kupendwana wapenzi wengi wa soka hapa jamvini ambao walikuwa wanafuatilia mashindano ya Kombe la Dunia.

Asanteni wadau wote humu kwa kampani nzuri sana,mmekuwa marafiki kwangu sina neno,mara nyingi mpira huu nilikuwa nacheki mwenyewe lakini kupitia ninyi nilikuwa najiona kama niko na watu maelfu wamenizunguka, Asanteni sana,tusameheane sana pale tulipokwazana,nawapenda wote,muwe na usiku mwema. Germany oyeeeeeeeeeeee!!!!
 
Last edited by a moderator:
Shukurani sana wadau nashukururu kwa Mara ya kwanza tangu 1998 katika WC sijahama timu mwanzo wa michuano mpaka mwisho hureeee team Germany
 
Then again. Messi kafanya nini ktk World Cup hii kupewa the Golden Ball? Kuna wachezaji waliwika katika haya mashindano kuliko Messi. Fifa sometimes wana lose credibility.

Hayo mawazo yako mgando na chuki dhidi ya messi mpelekee bibi ako huko...


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Rubaman ulisema timu ya Africa itachukuwa kombe la dunia vipi tena au Boateng anawakilisha?. Zile Comment za watu mwanzo Kabisa tungependa kuona utabiri tumekosa wengi angalau umepata ujerumani ila Mie nakumbuka nilisema Kombe litaenda Europe! DonDonald alisema litaenda North America tehtehteh.
 
Back
Top Bottom