Mimi siyo shabiki wa England, lakini naweza kumtetea Rooney kwa wale wanaomponda, haswa wanazi wa Loserfools.
Rooney kachezeshwa out of position, unategemea nini! Steve G kachezeshwa kwenye nafasi yale, lakini hakuleta impact kubwa kwenye timu. Cha ajabu, hakuna anayemponda Steve G!!
Hakuna ubishi, Rooney ndiye mchezaji star kuliko wote wa England; timu inafaa ijengwe kupitia kwake, kama Italia walivyofanya kupitia Pirlo. Rooney anapaswa akipige namba 10! Anafaa awe ndiye bosi pale; freekick anapaswa apige yeye, lakini hakupewa hayo.
Unategemea nini kama ukimchezesha kama namba 11 au 7! Pamoja na Raheem kukipiga vizuri jana, namba 10 alipaswa kukaa Rooney, Raheem angekipiga namba 11 ama 7. Rooney pia hakupewa uhuru wa kucheza anavyotaka, ndiyo maana analaumiwa kwa kushindwa kumsaidia Baines! Duh!
Anyway, ya England niwaachie
#teamEngland
Mimi ni
#teamBrasil #teamPortugal na
#teamGhana