World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

I. coast ni zaidi ya tembo, km nyangumi vile..... ila km una BP usiangalie mechi km hizi, unaweza ku"R.I.P" bila kupenda hahahahaha....
Hahahahaha kweli aisee nakumbuka mimi kama timu naipenda nikiona inazidiwa nilikuwa naenda kulala,ili nikiamka nikute matokeo,kweli aisee unaweza pata heart attak hivi hivi
 
Leo nipo na Wafaransa, labda na Equador. Hao argentina siwezi kuwaona maana muda mbaya na kesho job mapema.
Hayo maagentina yanacheza na vibondeni South Africa, hivyo matokeo yashajulikana kabla mechi kuchezwa.
 
Leo nipo na Wafaransa, labda na Equador. Hao argentina siwezi kuwaona maana muda mbaya na kesho job mapema.
Toka juzi nilifululiza,jana nikashindwa kuangalia I.Coast na Japan,leo nitaangalia ya France tu,Hao kina Merci nitasoma matokeo kesho,Yaani kumbe watu wa marekani na south america ndo huwa wanapata taabu hivyo?Toka 1998 kombe halijachezwa kwao.Huwa wanateseka sana na masaa aisee ngoja na sisi mwaka huu tusikilizie
 
Germany
Portugal
Ghana
United States

Sijui wenzangu mna maoni gani maana nikitazama hili kundi ni gumu kuliko makundi mengine. Ngoja tusubiri
 
Tokea fainali za kombe la dunia mwaka 2010,,siwapendi kabisa Uruguay,hasa huyo Suarez!
 
View attachment 164948 Uruguay hoi kipindi cha pili kwa Costa Rika View attachment 164949

Mabingwa wa kwanza kunyakua kombe la dunia Uruguay wameshindwa kufurukuta kipindi cha pili baada ya Costa Riko kusawazisha katika kipindi cha pili na kuongeza mabao mawili ya ushindi na kuifanya kuondoka na point zake tatu safi. Kutangulia sio kufika kama ilivyotokea kwa Barazil mechi ya ufunguzi.

Candid Scope hiyo costa riko ni kiswahili cha Costa Rica au mie ndo nimebugiii.....

Uruguay bila "goli kipa" wao wa akiba Louis Suarez hawana kitu....
 
Last edited by a moderator:
Candid Scope hiyo costa riko ni kiswahili cha Costa Rica au mie ndo nimebugiii.....

Uruguay bila "goli kipa" wao wa akiba Louis Suarez hawana kitu....

Wewe umeelewa nini? Ukiambiwa waswahili husema nchi ya Brazili, lakini wazungu husema Brasil kuna makosa? Kuna timu katika kombe la dunia toka Afrika nchi iitwayo Ivory Cost? Lakini kinachojia kwenye vyombo vya habari inaandikwaje? Katika dunia hii kuna wanaoitamka Tansania wakati waswahili unaelewa ni Tanzania na hatushtuki tukijua labda ni shauri yalafunzi au mfumo wa sila katika lugha zao. Hata Tanzania nako kuna kiswahili na viswahili vingi. Nenda Ntoni kwa Njomba Nzee Nkapa utakoma ubishi hata usahau kula samani NCHANGA wewe, baa! Njomba sifanye nchezo wewe. Geukia kule kwa wapoma utakuja kukutana na ile "kura tumekura sasa bado kulala! Nenda Kilimanjaro ukiitwa babangu inadhihirisha ni babake kweli au namna ya tafsiri ya kikwao? Kama hujaelewa endelea na mada nyingine.
 
Germany
Portugal
Ghana
United States

Sijui wenzangu mna maoni gani maana nikitazama hili kundi ni gumu kuliko makundi mengine. Ngoja tusubiri

Ktk hili kundi huyu ndo mgumu lakini hao wengine ni wali mbogamboga
 
Daaa Costa rica yenye wakazi million nne imewasumbua sana Uruguay wengi walitegemea hitakuwa match nyepesi kwa Uruguay.
 
Nadhani anamuongelea Wayne Rooney hapo

Daaah hongera sana buluda kwa kutupunguzia kelele, wale three lions ni kama timu yangu niipendayo yenye makazi pale mazalio ya mmbu ipo magazetini zaidi kuliko uwezo.

Ila mi nipo moodyless kwenye haya mashindano toka nipokee kipigo cha jibwa koko kisichotegemewa.
 
Daaah hongera sana buluda kwa kutupunguzia kelele, wale three lions ni kama timu yangu niipendayo yenye makazi pale mazalio ya mmbu ipo magazetini zaidi kuliko uwezo.

Ila mi nipo moodyless kwenye haya mashindano toka nipokee kipigo cha jibwa koko kisichotegemewa.

Pole sana Mpwa na ahsante kwa pongezi, hao so called 3 lions wakikutana na Buluda huwa wanageuka na kuwa three kittens.
Pirlo kawapa somo jingine jana.

Ng'ombe hata akonde vipi hawezi kufanana na mbuzi, najua mtarudi na hasira zote kama mbogo aliyejeruhiwa.

Hiyo team ya hapo kwenye mazalia ya mbu najitahidi kuisahau kidogo mpaka watakavyojirekebisha.



M
 
Moments to remember so far.. ImageUploadedByJamiiForums1402836966.503338.jpg
 
Mimi siyo shabiki wa England, lakini naweza kumtetea Rooney kwa wale wanaomponda, haswa wanazi wa Loserfools.

Rooney kachezeshwa out of position, unategemea nini! Steve G kachezeshwa kwenye nafasi yale, lakini hakuleta impact kubwa kwenye timu. Cha ajabu, hakuna anayemponda Steve G!!

Hakuna ubishi, Rooney ndiye mchezaji star kuliko wote wa England; timu inafaa ijengwe kupitia kwake, kama Italia walivyofanya kupitia Pirlo. Rooney anapaswa akipige namba 10! Anafaa awe ndiye bosi pale; freekick anapaswa apige yeye, lakini hakupewa hayo.

Unategemea nini kama ukimchezesha kama namba 11 au 7! Pamoja na Raheem kukipiga vizuri jana, namba 10 alipaswa kukaa Rooney, Raheem angekipiga namba 11 ama 7. Rooney pia hakupewa uhuru wa kucheza anavyotaka, ndiyo maana analaumiwa kwa kushindwa kumsaidia Baines! Duh!

Anyway, ya England niwaachie #teamEngland

Mimi ni #teamBrasil #teamPortugal na #teamGhana
 
Back
Top Bottom