World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Angetembea na boxer huyu mji mzima.

Sasa tunaposema anamasifa hiyo ndiyo maana yake, yaani kwa bidii tu alizonazo amekua vile sasa akifikia kiwango cha Zidane haitashangaza kila afungapo goli atakua anaonyesha hata nyeti zake zote ya front na ya back, bwahahahaaaaa cr7 si mchezo!
 
Hao wote Ronaldo kawashinda kwa Personal Awards wao wamemshinda kwa kupata Kombe la dunia.

Ndo ihalalishe kuwa mjivuni? Vinginevyo ana bidii sana na anajituma sana na akiendelea hivyo huku akipunguza masifa atafika mbali sana, he has the potential to be a hero.
 
lolote linaweza tokea maaana katika timu za afrika aljeria haikupewa nafasi kabisa kusonga mbele . kwasasa wanajiamini kuwa ndiyo muda na wao kuandika historia

dah mkuu ila hawa jamaa huwa ni wagumu sana asee
 
Umeongea ukweli mkuu. Sisi wabongo hatuwahesabu Wahindi, Waarabu au hata Wabongo mashombe (sijui kuwaita hivi ni political correct au) kuwa ni watanzania wenzetu hata kama walizaliwa na kukulia next door, ingawaje na wao wenyewe sometimes huwa hawajihesabu ni Waafrika/Watanzania hii nimeshaiona kwa Wahindi toka Tanzania walio huku Ughaibuni. Hivi kina Anwar Aziz aliyechezeaga Yanga enzi zile aliwahi kuitwa Taifa Stars? Pia kumbuka tulivyomshambulia yule miss Tanzania wa asili ya kihindi kuwa halipresent sura za mademu wa kitanzania. England wanachofanya kinaweza kuwa kinakwendana na Policy yao kitu kinachoweza kutafsiriwa kama ubaguzi au haki kulinganisha na nani anayetafsiri. Hivi Ekoku(mtangazaji wa TV) si alibadilishaga uraia toka Nigeria kuwa England akitegemea kucheza World Cup 1994 afu England wakashindwa kukwalifai au alikuwa Mnigeria mwingine?
ndomana utaona mbunge wa Kihindi mwenye Uraia wa Tanzania anashambuliwa na wakati anasaidia kijiji kuliko sie weusi Utasikia sio Mtanzania halisi mambo haya yangekuwa Marekani watu wangepiga Kelele ubaguzi tunaona kwa Walatino wa Kimarekani ila sie hatuoni Kama kuna ubaguzi mpaka afanyiwe mweusi. tanzania lazima ikazanie football kwa rangi zote ila tu mchezaji awe wamaana tusisumbuke sana Yanga na Simba zenye kuharibiwa wachezaji na wafazili Wenye pesa za kuchezea wanawapa wachezaji pesa za ovyo akija Taifa stars ovyo.
 
Ratiba Kamili Ya 16 Bora:

Juni 28.
Brazil V Chile
(saa 1 usiku)
Colombia V Uruguay
(saa 5 usiku)

Juni 29.
Uholanzi V Mexico
(saa 1 usiku)
Costa Rica V Ugiriki
(saa 5 usiku)

Juni 30.
Ufaransa V Nigeria
(saa 1 usiku)
Ujerumani V Algeria
(saa 5 usiku)

Julai 1.
Argentina V Uswis
(saa 1 usiku)
Ubelgiji V Marekani
(saa 5 usiku)
 
Mtoa uzi ni mtu ambaye hajui mpira; ila ni mshabiki wa matokeo tu. Kwa nini asijadili kuporomoka kwa soka la Ulaya?
England, Spain, Portugal wote wametoka raundi ya kwanza...

Huu ni uchambuzi wa kitoto sana. Hasa ukizingatia JF HOME OF GREAT THINKERS.
Kuhusu timu za ulaya ntaleta mtazamo wake...huu ni mtazamo kuhusu nchi za africa na sola la africa umesoma uzi vizuri great thinker..?
 
Kumbe wewe huwa huangalii mpira:
Ghana wamefunga magoli 4 kwenye kombe la Dunia mwaka huu; Wafungaji wa magoli hayo ni:
1.Asamoah Gyan = 2.
2. Andre 'Dede' Ayew = 2.

Niambie sub gani aliyeingia na kufunga goli. Acha uzushi wewe.

Kuhusu timu za AFRIKA kutolewa; si ajabu hata za ULAYA zimetolewa, tena nyingi tu.
1.England
2.Bosnia
3.Italia
4.Urusi
5.Ureno
6.Hispania
Kama umeangalia kwa umakini gyan asamoh amekusa magoli ya wazi mangapi mwaka huu..mimi nimeona magoli mawili mechi ya matatu mechi ya ureno na goal moja mechi ya ujerumani na hajaanza leo kukosa magoli ambayo yanaicost ghana..!!
 
Wakuu salama?kwa wale mashabiki wa mpira nina imani mmepata burudani ya kutosha kwenye mashindano haya tangu yaanze tar.12.June.aidha wengi wetu tumehuzunika kwa kutolewa kwa timu zetu za Afrika katika hatua ya makundi.Zipo sababu zilizosababisha kutolewa kwa timu hizo ktk hatua hiyo,ikiwepo uamuzi mbovu wa marefa.zilizofuzu kuingia 16 bora tuendelee kuzitakia mafanikio zivuke hatua hiyo na kuingia Robo Fainali.
Hebu tuangalie Timu hizi 16 katika nyanja ya kitakwimu katika mabara zilikotoka ikilinganishwa na idadi ya timu zilizokuwa kwenye makundi kutoka kwenye Mabara hayo:
BARA IDADI YA TIMU : ZILIZOINGIA 16 BORA %
SOUTH AMERIKA 06 05 83%
NORTH & CENTRL AMERICA 04 03 75%
EUROPE 13 06 46%
AFRICA 05 02 40%
ASIA & AUSTRALIA 04 00 00%
32 16
Kwa takwimu hizi,upo uwezekano mkubwa wa kombe hili kubaki aidha Amerika ya Kusini au Amerika ya Kati na Kaskazini.Nini maoni yenu Wakuu?
Nawasilisha.
 
Nahisi kama safari ya Brazil katika mashindano haya inafikia tamati kesho.
 
jamani napenda kujua mshindi wa kwanza Group A kati ya Brazil na Mexico!! PLZ
 
Kuanzia 16 bora,timu hubadilika kiuchezi,nategemea kuiona brazil tofauti kabisa na iliyo bora...
 
...tanzania lazima ikazanie football kwa rangi zote ila tu mchezaji awe wamaana tusisumbuke sana Yanga na Simba zenye kuharibiwa wachezaji na wafazili Wenye pesa za kuchezea wanawapa wachezaji pesa za ovyo akija Taifa stars ovyo.
Kabla ya kwenda mbali sana... Kuna mdosi gani hasa hapa Tz anacheza football? Wahindi wa Tz waliwahi kuwepo sana kwenye timu za Taifa kwenye michezo Kriketi na hockey, ambayo ilikuwa ni nadra kukutana na Mtz mbantu!

Na hata michezo hiyo ilipoanza kuwajaza Wtz wabantu, ilianza kufifia na sasa ipo hatarini kutoweka kabisa!
 
In world cup 2014 round 16 scheduled to start on Saturday, continental representation is as follows: -

AMERICA : Represented by 8 countries

EUROPE : Represented by 6 countries

AFRICA : Represented by 2 countries

Can you predict, world cup winner will come from which continent? AMERICA, EUROPE or AFRICA?
 

Attachments

Back
Top Bottom