World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Pole sana Mkuu, kutuliza maumivu meza panadol kisha ulale mapema.

Mkuu timu yangu ilishatoka kitambo, siku hizi nazisapoti tu hizi zilizobaki lakini leo nashangaa matokeo haya yameniumiza sana sijui kwa nini.
 
Uholanzi itashinda ila kwa mbinde na Costa Rica itashinda dhidi ya ugiriki,note my words.
 
Kwa hiyo sala yako tu ya kuwaombea ushindi unastahili kupata passport yao, shuka pale ubalozini na picha ya kuwaombea ushindi lazima watakutunuku kitabu chao lol!!! hahahahaha
Waanze tu kunipa,ila ngoja kesho nitadamkia ubalozini kwao,si ule kama unaenda ubalozi wa Uingereza?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tactics zenyewe kama ndo hizi za Kumnong'oneza Robben ajiangushe ndani ya 18 basi atakuwa bonge la kocha. Holland wameponea chupuchupu mwenyewe unajua. RVP ameshaumia huyo mtegemeeni kurudi december holiday fixtures

Goal la Sneijder ndio limewaua Mexico,hata kama Roben asingepata penati still Mexico wangefungwa hata dakika za nyongeza walishajiona wameshinda

Still unadoubt uwezo wa LVG? In short ameshachua Champions League kitu ambacho Wenger hajafanikiwa
 
Hapa mie mtazamaji wala sina pressure yoyote ila Costa Rica wazuri na Greece wanajituma sana, nayo inaweza kuwa bomba.

Hii kidogo inaweza kuwa entertaining game,7bu hawana jipya,watakamiana tu.
 
Mkuu timu yangu ilishatoka kitambo, siku hizi nazisapoti tu hizi zilizobaki lakini leo nashangaa matokeo haya yameniumiza sana sijui kwa nini.
Aisee yaani ni kweli kabisa,mimi pia Mexico walivyokuwa wanaoongoza kiukweli sikuwa na hamu ya kuangalia match ya pili,hata hamu ya kula ilikwisha,hadi mipango yangu mingine ya kesho niliiona kama haitaenda vile,ila sasa hivi nina nguvu ya ajabu usipime,Pole sana mkuu
 
mbuzi yake kamba tu.

atakimbiakimbia lakini mwisho wa siku lazima afungwe kamba tu.
 
Greece na Costa Rica sitizami sawa na kuwasha tv nikute ligi ya Poland inacheza huo mpira Kama na kunywa chai basi nitasinzia na ki kombe kidondoke Kama Teja. Costa Rica itashinda 2-0 bet!
 
Back
Top Bottom