World cup hii 2010

World cup hii 2010

Shedafa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2008
Posts
802
Reaction score
175
World cup iliyopita 2006 kulikuwa na mgawo wa umeme wa kufa mtu, sijui world cup hii itakuwaje. Nakumbuka ilikuwa nihame nilipokuwa ninaishi siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano lakini nikaminya, kwa sababu nilipokuwa nahama angalau kulikuwa na nafuu kidogo ya mgawo kuliko nilipokuwa nahamia. Niliminya hadi mashindano yalipoisha ndio nikahama. Sijui safari hii itakuwaje, sijui tutapata bahati ya kuiona bila zengwe!
 
umeme utakuwepo fulltime au umesahau kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi?wazime umeme wanajitaka hawajitaki?
 
Mh, ndugu yangu. Wanaweza kuzima bila ya wasiwasi, wanamuogopa nani?. Tena washakwambia kuwa watashinda kwa kishindo, wala si kwa ajili ya mazuri walioyafanya ila hatuna ujasiri huo!
 
umeme utakuwepo fulltime au umesahau kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi?wazime umeme wanajitaka hawajitaki?


Wanaweza kuzima umeme na bado wakashinda ushindi wa Tsunami uliochanganyika na wizi mkubwa wa kura. Kama unaisubiri World Cup kwa hamu kuu basi ujipigepige ili uwe na generator yako au uwe na plan B ya wapi utaennda kuangalia mechi hizo ambapo hata kama umeme hautakuwepo basi kutakuwa na umeme wa generator.
 
Back
Top Bottom