Wosia wa Hayati Magufuli ”Mtanikumbuka” Unatimia

Wosia wa Hayati Magufuli ”Mtanikumbuka” Unatimia

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
"Siku moja mtanikumbuka, najua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya, kwa sababu nime 'SACRIFICE' MAISHA YANGU kwa ajili ya Watanzania maskini" ~ Hayati. John Magufuli (RIP).

Ingawa najua kuna lile kundi lililojaa sumu, kwa machungu ya kukaa vijiweni baada ya kukumbwa na "Panga" la JPM kwenye vyeti fake, ajira hewa, utumbuzi majipu, uchaguzi 2020.
Mtaendelea kutukana .... ila "UKWELI" Utaendelea kusimama mahala pake bila kutetereka.
Na Kwa mgao huu wa kulazimishwa....

Hayo maneno yanazidi kusikika masikioni mwa wengi. Na yataendelea kusikika zaidi kadri siku zinavyozidi kusonga mbele taratibu. Wao wanalamba "ASALI" wananchi tunalambishwa "SHUBIRI"

Sasa Mabwawa ya hydroelectric yanafunguliwa kwa kuhujumiwa kama zamani,
Ili tu walioko kwenye mfumo waendelee kuleta utitiri wa miradi ya umeme kwa 10%.
Ili tu waendelee kupata 10% kwenye makampuni yanayouza majenereta makubwa kwenye taasisi kama mabenki na viwanda.

Ili tu waendelee kupata 10% kwenye upatu wa mradi wa gesi ya LNG-Mtwara unaonadiwa kimataifa.

Ili tu waendelee kupata 10% kwenye uwekezaji mpya nishati ya upepo na Solar.

Ili tu waendelee kuneemeka na 10% ya uuzaji Mafuta kwenye majenereta ya IPTL mpya.

Tunawaona na Tunawapimia.

Alamsiki!
FB_IMG_1666597826291_remastered.jpg
 
Magufuli alikua Rais wa kweli. Alilipenda taifa na watu wake. Hakuwa mkamilifu ila alikua mwaminifu katika uzalendo wake. Inaumiza sana namna alivyoondolewa lakini inatia moyo kwamba kumbe inawezekana. Tusonge mbele yajayo yanafurahisha. Hawa mafala wachache wanaoipindisha nchi ni kitambo kidogo watabaki historia, hatutowasikia tena kisiasa. Taifa hili haliwezi kurudi kule tulikotoka, hii ni dhahiri na itakua.
 
L
Magufuli alikua Rais wa kweli. Alilipenda taifa na watu wake. Hakuwa mkamilifu ila alikua mwaminifu katika uzalendo wake. Inaumiza sana namna alivyoondolewa lakini inatia moyo kwamba kumbe inawezekana. Tusonge mbele yajayo yanafurahisha. Hawa mafala wachache wanaoipindisha nchi ni kitambo kidogo watabaki historia, hatutowasikia tena kisiasa. Taifa hili haliwezi kurudi kule tulikotoka, hii ni dhahiri na itakua.
Let's Hope for the best !!
 
Naamini ule Uchaguzi angefuata haki leo hii bungeni tungekua na wabunge WANAOWEZA KUHOJI sarakasi hizi,alifanya unyama wa hali ya juu kuiba mamlaka ya wananchi mchana kuepe bila huruma na kinyume cha katiba. Wabunge wenye kuhoji alifyekelea mbali ushindi wao na Wengine walitiw nguvuni mawakala wao. Hili ndilo linafanya mnalalamika kuhusu JPM ninyi wapenzi wake .badala ya kuusimamia ukweli mnaleta tantalilaaa humu.Nchi inakua nzuri kunapokua na upinzani. Angalia sasa mnajipiga fimbo matakoni wenyewe wakati fimbo mlizitaka wenyewe. Safari ijayo mhubiri siasa safi sio ujinga ule wa 2020.
 
Kwani kwenye miaka yake mitano haukuwahi kuushuhudia ujame zaidi ya huu.
Lakini umeme ulikuwa moto chini bila shida.
Why now!

Unadhani hatakuwa tunaona umeme kukatika kipindi cha dhalimu? Rejea vizuri kipindi cha kampeni za uchaguzi kuanzia july 2020 kulianza kuwa na mgao mkali wa umeme, na akawa anajifichia kwenye ujenzi wa bwawa SG. Acha wahuni wafanye yao maana aliondoa nguvu ya wananchi kuhoji, akatengeneza kizazi za kusifia, matokeo yake ndio hawa chawa waliojaa ili watoke kimaisha.
 
Back
Top Bottom