SoC02 Wosia wa "kitabu mtatuzi wa matatizo" ndani ya nchi tajiri yenye watu masikini

Stories of Change - 2022 Competition

MAISHUU2022

New Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Jina langu nililopewa na walimwengu najulikana kama KITABU MFUMBUZI WA MATATIZO.Nimezaliwa DUNIANI kote kwa mwaka usiokuwa na jina toka Enzi katika kila Pembe ya Dunia, Ninaishi TANZANIA, Nchi TAJIRI yenye watu MASIKINI ndani yake.Nimevumilia nimeshindwa nimeona Bora niseme TANZANIA ina watu wasionijali kasoro wachache wanaonikumbatia.Narudia Kusema TANZANIA ni nchi TAJIRI yenye watu masikini kwa hilo lazima mkiri.

Na utajiri umefichwa ndani yangu na watu hawanijali wala kunithamini. Sio umasikin wa pesa tu wengi wajuavyo ila Wengi wana umaskini wa fikra na mawazo, umaskini wa akili na mali, umaskini wa tabia njema na utambuzi, umaskini wa hekima na busara njema, umaskini wa UTU na UTAJIRI wa moyo.
Mtaendelea kuulalamikia umaskini mpaka mtaingia Kaburini kwa sababu hamnipendi ila mnawajali wengine kama jirani yangu POMBE.

Ndio! Kwanini nisiseme?.Mnamjali anaendoa utu na heshima yenu, anaeondoa fikra na mawazo chanya, anaeondoa nguvu kazi za kutafuta uchumi. Hebu Jiulize ulishawahi kutembea hatua ngapi katika kila kona ya mji ukakutana na "LIBRARY" zilizozagaa mtaani,vijijini, mijini, kata, wilaya au mkoa???!!! Ndani yake wakanihifadhi ili watu mbalimbali wakaja kunisoma na kuelimika kisha wakastaarabika kitabia kimaneno na kivitendo?

Lakini cha ajabu JIRANI Yangu POMBE/BIA/KILEVI ametengenezewa mazingira mazuuuri tena yenye kupendeza katika kila hatua utaona GROCERY,PUB, BAR zimetawanyika kila kona ya mji,watu wamejikusanya na wengine kukesha usiku kucha wakinywa na kulewa huku wengine wakipoteza akili,nguvu na pesa zao, utu na heshima yao.

Nikuulize kati yangu MIMI KITABU na jirani yangu KILEVI nani mwenye faida zaidi ya mwenzie? Najiuliza sana lakini nakosa jawabu kwani TANZANIA NI NCHI YA "WALEVI" AU YA WASOMI??!!

Mwenzenu KITABU naumia kwa kutonijali kama nchi za wenzenu wanavyonipenda kwa kuniweka ndani ya majengo yao kila hatua kuna library tofauti na TANZANIA.Msisahau kuwa mimi NI KITABU Mtatuzi wa matatizo na nilioshehen kila aina ya utajiri wa kiimani, kifamilia, ndoa, uchumi, uongozi, kilimo na ufugaji n.k

Nawashangaa viongozi wenu na watu wachache wenye kujitambua mkashindwa kuhamasisha jamii zenu mkajenga majengo au maeneo madogo katika kila eneo ili mradi nyinyi na vizazi vyenu kila siku mkapata nafasi ya kujisomea mambo mbalimbali au wakaniazima na kunisoma majumbani mwenu.

Basi matatizo, misukosuko na mitihani iliowazunguka na umasikini uliowatawala hautaondoka sababu hamna desturi ya kunisoma na kunizingatia mara kwa mara, Imani yenu kiroho na UTU utawatoweka na kuwa kama wanyama na umasikini hautawaisha na kuendelea kuwa "wajinga" kwa kuukosa uwerevu na elimu yangu.

-Ukiangalia upande mwengine kuna watu waliokosa utu wanauana na kumwagana damu kisa ndoa au usaliti wa kimapenzi au ugomvi wa kifamilia.Elimu ya ndoa ni pana sana na ndio jamii yenyewe inayojengeka kupitia ndoa, kinachonishangaza mnapeana vyeti siku ya ndoa kabla ya kuisoma ndoa yenyewe.

Sasa sijui mlishindwaje kunisoma mapema mkajua mustakbali mzima wa familia, mkaijua ndoa ilivyo kabla ya ndoa na ndani ya ndoa ili muepukane na misukosuko au changamoto ambazo zinazoweza kuepukika au kuzitatua ndan ya ndoa au familia ikiwa mmeelimika.

Mtajua jinsi ya kuheshimiana, kuvumiliana, kupendana, kusaidiana na kufurahi pamoja maisha ya ndoa lakini kwa hakuwa hamtaki kunisoma mimi KITABU basi mtaendelea kuteseka kila siku.

Ikiwa hiyo haitoshi Tanzania ina viongozi wazuri wengi ila wengi kati yao wapo wasio na utu, viongozi waharibifu, wasiojali maslahi ya umma, matapeli na ufisadi uliowatawala wenye kujali nafsi zao wakasahau za wenzao sababu tu hawajastaarabika kitabia na hasa kimatendo.Yote haya ni kwa sababu ya kunipuuza mimi, hawanijali hata kunisoma na kunizingatia. Wengine wananipuuza sio kama hawajui ila wanajua ila matendo yao ni tofauti na kila wanachokijua, ukitaka kumjua alie elimika mwangalie matendo yake.

Mkinisoma mtaelewa uongozi bora unahitaji nini na mkiendana na mlichokisoma kimatendo basi watu wenu watafaidika nanyi na nchi itastaarabika na umasikini utaanza kuondoka kwa watu wenu.Mtakuwa viongozi wenye uwezo kiutawala,uwezo wa kiakili,wenye nguvu ya Hamasa na msukumo wa kujituma na ubunifu wa kupanga mambo na kuyatekeleza.

Lakini mkiendelea kunipuuza na watu wenu wakaendelea kukaa kimya basi mtaendelea kupata laana ya wale wasio na nguvu ya kuwashtaki ila mahakama ya mbinguni tu ndio watashikamana nayo, Mtasumbuka kwa mitihani isiokwisha na misukosuko isiomalizika na maradhi yasiowaondoka kwani matatizo mengine ni sababu ya malalamiko ya watu wenu, VIONGOZI nisomeni mpate kuelimika na mtoke katika kundi la wajinga kama Punda mbeba mizigo ya Vitabu visivyomnufaisha.

Nikirudi kwa vijana wenu mpka nawaonea huruma , wamemaliza chuo wanahaha mitaani na barua mikononi miaka sasa nenda rudi mpka viatu vinawaisha miguuni kwa kutafuta ajira. Niwaambie kuwa wasinisahau wasijione kuwa wanajua kila kitu kwani bado hawajanimaliza kunisoma. Hawajanisoma stadi za maisha wala elimu za Fedha, hawajui vipaji vyao wala ubunifu na ujuzi wa kujiajiri.

Kumbuken nyinyi mna nafasi ya kuwaajiri vijana wengi walio mitaani na sio nyie kuitafuta ajira kwenye maofisi wilayani.Amkeni mapema kabla ya jua kuzama acheni kujifanya hamuambiliki eti mnajua kila kitu, kaeni chini mnisome tena.Elimu za mtaani bado hazijaisha, mjitambue, muamke na muwe wabunifu.Lakini mkisema hamnihitaji tena kwa kuwa mna degree ya makaratasi mkononi basi mtaendelea kusota na kuhangaika kuitafuta ajira na ilhali ajira binafsi zipo ndani yangu.

NAWAUSIA, Ili vizazi vyenu vijavyo vinusurike na umaskini uliotawala kwa sasa lazima wazazi waamke kutoka katika usingizi mzito wa kutojali na kunifuatilia mimi KITABU. Kwa uchache nafasi mliompa jirani yangu BIA/POMBE ndio nafasi mnayotakiwa kunipa mimi kwa kunijaza na kunihifadhi ndani ya LIBRARY katika kila kona ya miji na vijiji vyenu na muhamasishane kila siku munisome sana. Nihifadhini majumban katika vyumba maalum ili watoto wenu waanze kujenga Mapenzi na mimi kunipenda tokea udogo wao mpaka ukubwani kwao na ikibidi andaeni mashindano madogo kwa makubwa ya usomaji na uelewa uliomo ndani ya sisi

VITABU.
Mkifanya hivyo mtaanza kujawa na utajiri uliopo ndani ya nchi yenu, Nitawajaza hekima na busara,werevu na utambuzi, akili angavu na mawazo chanya yenye maono ya sasa na ya muda mrefu.

Nisomeni kiimani mjaze imani zenu vifuani mwenu, nisomeni kiuchumi muondoke na misongo ya mawazo ya utafutaji, nisomeni kindoa na kifamilia zistaarabike familia zenu na ndoa zenu zidumu muda mrefu na mengine mengi.

Ila ikiwa bado mtaendelea na msimamo wa kutonijali na kunithamini basi mtaendelea kuwa na umasikini katika nchi Tajiri ya TANZANIA Kwa kuwa na mawazo Yale Yale fikra zilezile na watu walewale ambao JANA yao Sawa na LEO Yao na hawana matarajio ya KESHO yao.
 
Upvote 2

Makini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom