Wote waliomtukana Shaffih Dauda kuhusu suala la Mo wamuombe radhi haraka sana

Wote waliomtukana Shaffih Dauda kuhusu suala la Mo wamuombe radhi haraka sana

Naomba uweke pia imetumia kiasi gani usijekuta hela hizo zimeishatumika kugharamia timu pia.
Kama faida simba Wamepata musimu huu ila faida imetokana na viingilio vya uwanjani mechi za kimataifa pamoja na mgao kutoka CAF ila ligi ya ndani wote tulio baki tupo hoi taabani.
 
.... mpaka dk hii taarifa ile bado imesimama wima mno! hakuna uongo wala uzushi wowote ule .
Taarifa yake ilisema muda mfupi ujao, mwekezaji wa Simba atatangaza kujiondoa. Wewe unasema taarifa ile imesimama wima, sijui wima upi wakati bado tunaendelea kusubiri huo muda mfupi utimie pale mwekezaji atakapotangaza kujiengua. Kwa kuwa bado hajatangaza kujiengua, taarifa ya Shaffih bado haijasimama, ila tunaiheshimu kwani hakusema huo 'muda mfupi' ni dakika, saa, siku, miezi au miaka mingapi. Bado tunasubiri Mo ajiengue, ndipo tutampongeza na kumuomba radhi Shaffih
 
Wewe huelewagi ndio maana nakukosoaga kila pahala kuanzia kwenye matamthilia yako hadi kwenye uzi wq AFCON.

Simba sports msimu uliopita kwenye mashindano yote imekusanya Billion 5.
Mechi karibu zote zilizohusisha Simba ukiachilia alizocheza uhuru na timu za daraja la kati ndizo hazikuwa na mashabiki wengi zingine zote ziliingiza million 300+ .

Note. Hizi fedha zilikuwa zikinufaisha sana timu za ugenini kutokana sheria mpya za TFF.

Sasa nitajie timu iliyoingiza hata 2 billion msimu uliopita
Duh mbumbumbu fc, kwahiyo hayo mafanikio hayana uhusiano na uwekezaji uliofanywa?
 
Nao wakapiga kelele, wakaziba masiko yao wasitake kusikia alichokisema yule farisayo aliye mwandishi hata saa ilipofika nayo kweli ikachomoza kama miale ya nuru ichomozayo magharibi, ndipo mbumbumbu wote wakapoteana.
Kiromoni 3:9
Na hili ndilo neno la usiku huu
Bwana awe naaaaaaaanyiiiii
😀😀😀😁😁
 
Mimi wala sina tatizo nawewe ila kama umesoma komenti yangu nimesa ukiondoa mapato ya club bigwa barani Afrika simba imekusanya milioni 450+. Pia mambo ya tamthilia achana nayo maana mm pengine ni mutu pekee naye fatilia mambo yote duniani kiasi Kwamba akuna sehemu yoyote unaweza nidanganya kuanzia siasa za ndani,nje, uchumi, michezo na burudani mpaka Utamaduni. Sehemu pekee utaniacha njia panda ni ulonzi full stop.
Nipe mchanganuo wa hizo 450+ milion nami nitakupa mchanganuo wa Bilion 5.

Kwenye michezo na burudani my frendo umekwama hivi navijua kiajabu sana huwezi nishinda hata kidogo
 
Simba njaa hiyoooo mlangoni kwenu kudadadeki. Mlitamna sana na pesa ya MTU, sasa ameamua kusepa zake. Usitukane Mamba kabla ya kuvuka MTO
 
Eti eeee. Sasa mbona sauti ya ng'ombe (Mo) kazi yake kulia lia mitandaoni.
Ameshauriwa afanye hivyo wanachama na mashabiki wote wajue chanzo cha tatizo ili iwe rahisi kumshughulikia mwenyekiti mamluki

Lakini naona kama Yanga mmeuvalia njuga sana mgogoro huu, halafu wala haujafikia stage ya kuitwa mgogoro ni tofauti ya maoni tu
 
Ameshauriwa afanye hivyo wanachama na mashabiki wote wajue chanzo cha tatizo ili iwe rahisi kumshughulikia mwenyekiti mamluki
Ya kweli hayo Ses yaani ni sawa na jambo litokee chumbani kisha muache kuyamalizia huko chumbani halafu muyatoe nje ili watu wa nje wajue. Mmh. Hamuoni kama ndio kuchochea.

lakini naona kama Yanga mmeuvalia njuga sana mgogoro huu, halafu wala haujafikia stage ya kuitwa mgogoro ni tofauti ya maoni tu
😂😂😂 kama mlivyovalia njuga ishu ya bakuli. 💃💃💃💃

Hivyo mtuvumilie tu.
 
Ya kweli hayo Ses yaani ni sawa na jambo litokee chumbani kisha muache kuyamalizia huko chumbani halafu muyatoe nje ili watu wa nje wajue. Mmh. Hamuoni kama ndio kuchochea.

😂😂😂 kama mlivyovalia njuga ishu ya bakuli. 💃💃💃💃

Hivyo mtuvumilie tu.
Hahahaaaa Yanga bana
 
Back
Top Bottom