Wow! Tazama watu walivyosherehekea kufufuka kwa Mfalme wa wafalme!

Wow! Tazama watu walivyosherehekea kufufuka kwa Mfalme wa wafalme!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Huku na kule duniani, nderemo, vifijo, shangwe na milio ya nyimbo za sifa vinasikika! Mioyo ya watu imejaa shukrani, na machozi ya furaha yanatiririka kwa kumbukumbu ya ushindi wa Mfalme wa wafalme.

Yesu ndiye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana! Alishuka kutoka mbinguni kwa unyenyekevu, akabeba dhambi za ulimwengu, akamwaga damu yake na kufa msalabani kwa ajili yetu. Lakini mauti haikuweza kumshikilia. Siku ya tatu alifufuka kwa utukufu, akithibitisha kuwa yeye yuko juu ya kifo na mauti. Hii ndio sababu mamilioni ya watu kote duniani wanasherehekea kila mwaka kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Mfalme wa Wafalme - Yesu Kristo (Ufu 19:16).

Mwenye macho haambiwi: "Tazama..."

Italy2.jpg
Mexico.jpg
New York City2.jpg
Philippines.jpg
Philippines2.jpg
Romania.jpg
Spain.jpg
Thessaloniki.jpg
France.jpg
Greece.jpg
Greece2.jpg
Italy.jpg
 
Friend zone...

Kwanini utaki kuniita tena rafiki....
😭😭😭😭😭😭
Hutaki tena vya zamuuuuuu
 
Ngoja uone wanafiki watakavyo kandia sasa😁😁

Jina la Yesu, mapepo yanapata taabu

Ujio wa Yesu Kristo ndio ulioibadili Dunia.
Mwenyewe alisema:
"Kwa hiari yangu niliutoa uhai wangu ili niweze kuupokea tena". Hii ina maana alikuwa na uwezo wa kutoutoa uhai wake. Aliutoa uhai wake ili kuwathibitishia wanadamu jinsi alivyowapenda, ndiyo maana kabla hata watu kufikiria kuwa angekamatwa na kufa msalabani, aliwaambia:
"Hakuna upendo unauzidi huu wa mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake", tena akasema, siwaiti ninyi watumwa, bali rafiki zangu, mkiyatenda hayo niliyowaamuru.

Lakini kuonesha ukuu wake, na kwamba alijifanya mtu, siku ya kuondoka kwake Duniani, alisema:
Yohana 5:17
"Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako."
, akithibitisha kuwa alikuwepo hata kabla ulimwengu haujaumbwa.

Tena Yesu anasema kuwa hata kabla ya Ibrahim, Yeye alikuwako.
Yohana 8:58
"Kweli nawaambieni, kabla ya Abrahamu kuwako, mimi niko"
Tumwombe Yesu Kristo Bwana wetu awajalie ufahamu wale wenye hamu ya kumtumikia.Mungu wa kweli, lakini wamepotoshwa na mafundisho ya uwongo, tukiomba kwaajili ya ndugu zetu Wayahudi waliomkataa Yesu Kristo Masiha ili wamkiri Kristo. Na ndugu zetu waislam wanaomwona Kristo kama mwanadamu sawa na manabii wa kale waweze kuujua ukuu wa Kristo aliyejifanya mwanadamu ili tu awafikie wanadamu, japo hakuwa mwanadamu. Wakishajua kuwa Kristo alijifanya mtu, na kwamba neno lake ni la mwisho, watayatafuta maagizo yake katika kila jambo. Ili wauishi upendo wake. Waislam, kama walivyo wakristo wanaamini Yesu Kristo atarudi tena, tofauti ni kwamba, wakati wakristo wakizingatia maelezo ya Kristo kuwa atarudi kuwahukumu walio hai na waliokufa, waislam wanaamini atarudi tena kuja kukalia kiti cha mfalme Daud na kuutawala Ulimwengu mzima.

Lakini Yesu mwenyewe anasema, "nimepewa na Baba, mamlaka yote, Duniani na mbinguni", hivyo atarudi kama Bwana wa hukumu.
 
Friend zone...

Kwanini utaki kuniita tena rafiki....
😭😭😭😭😭😭
Mbona unajihukumu mwenyewe?
Hebu soma Yohana 15:14
"Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza."
Halafu uniambie Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema hivyo.
 
Huku na kule duniani, nderemo, vifijo, shangwe na milio ya nyimbo za sifa vinasikika! Mioyo ya watu imejaa shukrani, na machozi ya furaha yanatiririka kwa kumbukumbu ya ushindi wa Mfalme wa wafalme.

Yesu ndiye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana! Alishuka kutoka mbinguni kwa unyenyekevu, akabeba dhambi za ulimwengu, akamwaga damu yake na kufa msalabani kwa ajili yetu. Lakini mauti haikuweza kumshikilia. Siku ya tatu alifufuka kwa utukufu, akithibitisha kuwa yeye yuko juu ya kifo na mauti. Hii ndio sababu mamilioni ya watu kote duniani wanasherehekea kila mwaka kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Mfalme wa Wafalme - Yesu Kristo (Ufu 19:16).

Mwenye macho haambiwi: "Tazama..."

View attachment 3568026View attachment 3568027View attachment 3568028View attachment 3568029View attachment 3568030View attachment 3568031View attachment 3568032View attachment 3568033View attachment 3568034View attachment 3568035View attachment 3568036View attachment 3568037
Asante kwa taarifa
 
Back
Top Bottom