My friend, unajaribu kutenganisha sikukuu mbili zenye uhusiano wa moja kwa moja kibiblia na kihistoria. Ngoja nikusaidie:
Pasaka ya Wayahudi ndiyo msingi wa Pasaka ya Wakristo. Pasaka ya Wayahudi (Passover/Pesach) ilianzishwa ili kuadhimisha wana wa Israeli kuokolewa kutoka katika utumwa wa Misri. Sasa kumbuka, kilichowaokoa ni damu ya mwana-kondoo. Hii ilikuwa kivuli au symbol ya damu ya Yesu Kristo kama “Mwana-Kondoo wa Mungu” (Yohana 1:29)
Ili ujue kuna connection kati ya Pasaka ya Wayahudi na Pasaka tunayosherehekea sisi, soma Mathayo 26:17-19, Marko 14:12-16 na Luka 22:7-20. Maandiko hayo yanaelezea jinsi Yesu mwenyewe alivyoisherehekea Pesach.
Picha hiyo ya Tel Aviv inaonyesha Wayahudi wakila Seder. Yesu alikula chakula cha Pasaka (Seder) pamoja na wanafunzi wake. Hii ndiyo tunaita "The Last Supper."
Katika tukio hilo, alitumia mkate na divai, akaanzisha Agano Jipya akisema "huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu... hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi... fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu..."
Hapo Yesu aliunganisha Pasaka ya Wayahudi(Pesach) na Pasaka mpya tunayosherehekea leo ambayo katika baadhi ya tafsiri za Biblia, neno lililotumika ni Easter. Christian Easter is the fulfillment of Jewish Passover.
Kumbuka tena, neno “Easter” halipo katika maandiko ya awali ya Kigiriki. Neno la asili ni Pascha (Πάσχα) = Passover
Tafsiri nyingi hutumia “Passover”
Kwa hiyo kuitenganisha Pasaka ya Wakristo na hiyo ya Wayahudi ni kutokujua asili yenyewe ya Pasaka.
Narudia tena: Wayahudi wanaadhimisha ukombozi kutoka katika utumwa wa Misri kupitia damu ya mwanakondoo. Na Wakristo wanaadhimisha ukombozi kutoka katika utumwa wa dhambi kupitia damu na kifo cha Yesu Kristo na kufufuka kwake. Hayo ni mambo mawili yenye uhusiano mkubwa.
Paulo anasisitiza katika 1 Wakorintho 5:7 akisema:
"...kwa maana Kristo, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu."
Halafu usisahau, Israeli wapo Wakristo pia na makanisa ya Wakristo wanaofanya maadhimisho ya Pasaka ya Agano Jipya kila mwaka. Kwahiyo sio sahihi kufikiri kwamba Pasaka ya Kikristo haijasherehekewa Israeli.
Dada yangu unafahamu kuwa unaejenga naye hoja huyu mimi niliwahi kuwa Myahudi kidini? yaani Judaism?
so huwezi kuniambia kitu kuhusu Uyahudi..
kwakuwa mnatumia agano la kale moja Ni kweli kuwa kiroho kuna muunganiko, lakini unachanganya
theolojia na
uhalisia. Kihistoria, Kanisa lilitenganisha Pasaka na kalenda ya Kiyahudi tangu mwaka 325 AD ili iwe sherehe inayojitegemea.
Kwa Myahudi, Pasaka ni ukombozi wa taifa la israel
kwa Mkristo ni kufufuka kwa mwokozi. Kuziunganisha ni kupuuza maumivu ya kihistoria na tofauti za msingi za kisheria na kikalenda zilizowekwa na mababa wa kanisa ili kutofautisha imani hizi mbili."
Ngoja sasa NIkueleweshe
🙁 huenda hata historia ya pasaka huijui)
"Asili ya neno 'Pasaka' (Pesach) haitokani na kufufuka kwa mtu, bali inatokana na kitendo cha Mungu
kupita juu ya nyumba za Waisraeli na
kuwaua wazaliwa wa kwanza wa Misri. Pasaka ya asili ni tukio la
hukumu na ubaguzi Mungu alihukumu Misri na kuwabagua (kuwaokoa) Waisraeli kupitia alama ya damu. Bila kifo cha wazaliwa wa kwanza wa Misri, kusingekuwa na Pasaka. Kwa hiyo, huwezi kusema ni 'kitu kile kile' bila kukubali kuwa msingi wa Pasaka ni
mauti kwa adui na
ulinzi kwa mteule na wala halitokani na mambo ya ondoleo la Dhambi sijui mwanakondoo azichukuaye dhambi za ulimwengu lah..
naendelea kukuelekeza kuwa katika
Leil Shimurim (לֵיל שִׁמּוּרִים) ndo usiku ambao mungu alipita juu ..
(פֶּסַח) yaani Pesach (Kupita juu / Kuruka (To Pass Over) Kama unavyopiga hatua ndefu kuruka kitu kilichopo chini) na huku wana waisrael wakisherekea Pesach wamisri wao walilia na Makat Bechorot (מַכַּת בְּכוֹרוֹת) pigo la kuuliwa kwa mzaliwa wa kwanza lenyewe.
nimekupa maana yake sijui..
sasa tuache huko ilikuwa inafanyika lini au mpaka sasa hivi inafanyiak lini..
sherehe hizi zinatofautiana kama mwanzo nilivosema kuna
Pasaka (Pesach) Tarehe 14-15 Nisani
Hii ndiyo sherehe kuu. Inaanza jioni ya tarehe 14 Nisani (wakati mwanakondoo anachinjwa) na kuingia tarehe 15 Nisani (usiku wa chakula cha Seder). hii ni Kukumbuka ukombozi wa Waisraeli kutoka utumwani Misri na jinsi mauti "ilivyopita juu" (
passed over) ya nyumba zao.
soma Kutoka 12 (mstari 1–14) hii ndo amri ya kwanza ya pasaka na kuteuliwa mwezi Wa nisani kuwa mwezi wa kwanza kupita miezi yote na kuteuliwa tarehe 14 kuwa sikukuu..
inayofuata baada ya pasaka huwa ni
Sikukuu ya Mikate Isiyochachwa (Chag HaMatzot) Tarehe 15-21 Nisani Mara nyingi Nyinyi ndo mnaichanganya na Pasaka, lakini kibiblia hii ni sherehe inayofuata mara baada ya usiku wa Pasaka na hudumu kwa
siku saba. Wayahudi hawaruhusiwi kula kitu chochote chenye chachu (
chametz) kwa siku hizi saba. Huu ni ukumbusho wa jinsi walivyoondoka Misri kwa haraka bila muda wa unga wao kuumuka (
Kutoka 12:15-20).
sasa sikukuu ya mwisho ndo huwa ni
Sikukuu ya Malimbuko / Mavuno ya Kwanza (Yom HaBikkurim)
Hii hufanyika ndani ya juma la Mikate Isiyochachwa (kawaida ni siku ya kwanza baada ya Sabato ya kwanza ya Pasaka). na ndo hapa watu wenye mafunzo Kutoa mganda wa kwanza wa mavuno ya shayiri (
barley) kwa Mungu kama shukrani (
Mambo ya Walawi 23:10-11).
nikukumbushe pasaka sio siku moja ni package
Mlolongo wa Matukio yaani Pasaka ya asili ni "package" ya sherehe tatu (Pasaka
pesach, Mikate Isiyochachwa
Chag HaMatzot, na Malimbuko
Yom HaBikkurim). Ukisema ni "kitu kile kile," unamaanisha unasherehekea pia siku saba za kutokula chachu?
pasaka haifuatwi na kufunga siku arobaini kama mnavyofanya sijui kama nimeeleweka?
nimeona umesema Pasaka yaani "EAster' ni utimilifu wa pass over..
"Easter" ni utimilifu wa "Passover" na neno la asili ni
Pascha. Hapa ndipo anapokosea kihistoria:
ukisema hivyo tu najua hujasoma historia vizuri rudi kasome Mzozo wa Quartodeciman Katika karne za kwanza, kulikuwa na mgogoro mkubwa (Quartodeciman controversy) kuhusu ni lini Pasaka isherehekewe. Wakristo wa Mashariki walitaka ifuate tarehe ya Kiyahudi (14 Nisan), lakini Kanisa la Magharibi lililikataa hilo....
kwenye Mkutano wa Nicaea (325 AD) Kanisa liliamua rasmi
kutenganisha Pasaka ya Kikristo na kalenda ya Kiyahudi. Walitaka sherehe ya Kikristo isiwe na utegemezi kwa Wayahudi. Hivyo, leo Pasaka ya Kikristo na ya Kiyahudi mara nyingi haziangukii siku moja.
kuna hoja umenifanya nicheke saana kwamba "Israeli kuna Wakristo pia." Hili ni kweli, lakini ni
asilimia ndogo sana (chini ya 2%), kwahiyo Unapozungumzia "Pasaka ya Israeli" kama taifa, unazungumzia
Pesach. Huwezi kuchukua sherehe ya watu milioni 7 (Wayahudi) na kuifunika na imani ya watu laki 1.8 (Wakristo wa Israeli). Ni sawa na kusema Krismasi ni sherehe ya kitaifa nchini Saudi Arabia kwa sababu tu kuna wageni Wakristo kule...
au Sherehe za dini ya shinto zikifanyika Tanzania ni sherehe za kitaifa wakati hata asilimia 2 hawafiki... Usisahau pia kuna wabudha na washinto tanzania ila hwana athari yoyote