Ngoja uone wanafiki watakavyo kandia sasaππ
Jina la Yesu, mapepo yanapata taabu
Ujio wa Yesu Kristo ndio ulioibadili Dunia.
Mwenyewe alisema:
"Kwa hiari yangu niliutoa uhai wangu ili niweze kuupokea tena". Hii ina maana alikuwa na uwezo wa kutoutoa uhai wake. Aliutoa uhai wake ili kuwathibitishia wanadamu jinsi alivyowapenda, ndiyo maana kabla hata watu kufikiria kuwa angekamatwa na kufa msalabani, aliwaambia:
"Hakuna upendo unauzidi huu wa mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake", tena akasema, siwaiti ninyi watumwa, bali rafiki zangu, mkiyatenda hayo niliyowaamuru.
Lakini kuonesha ukuu wake, na kwamba alijifanya mtu, siku ya kuondoka kwake Duniani, alisema:
Yohana 5:17
"Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako." , akithibitisha kuwa alikuwepo hata kabla ulimwengu haujaumbwa.
Tena Yesu anasema kuwa hata kabla ya Ibrahim, Yeye alikuwako.
Yohana 8:58
"Kweli nawaambieni, kabla ya Abrahamu kuwako, mimi niko"
Tumwombe Yesu Kristo Bwana wetu awajalie ufahamu wale wenye hamu ya kumtumikia.Mungu wa kweli, lakini wamepotoshwa na mafundisho ya uwongo, tukiomba kwaajili ya ndugu zetu Wayahudi waliomkataa Yesu Kristo Masiha ili wamkiri Kristo. Na ndugu zetu waislam wanaomwona Kristo kama mwanadamu sawa na manabii wa kale waweze kuujua ukuu wa Kristo aliyejifanya mwanadamu ili tu awafikie wanadamu, japo hakuwa mwanadamu. Wakishajua kuwa Kristo alijifanya mtu, na kwamba neno lake ni la mwisho, watayatafuta maagizo yake katika kila jambo. Ili wauishi upendo wake. Waislam, kama walivyo wakristo wanaamini Yesu Kristo atarudi tena, tofauti ni kwamba, wakati wakristo wakizingatia maelezo ya Kristo kuwa atarudi kuwahukumu walio hai na waliokufa, waislam wanaamini atarudi tena kuja kukalia kiti cha mfalme Daud na kuutawala Ulimwengu mzima.
Lakini Yesu mwenyewe anasema, "nimepewa na Baba, mamlaka yote, Duniani na mbinguni", hivyo atarudi kama Bwana wa hukumu.