WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,810
Reaction score
6,599
Soma hoja za WWF hapa kwenye linki https://wwf.fi/mediabank/10039.pdf.

Je wewe uko upande upi na kwanini?

=======

WWF is one of the world’s largest and most experienced independentconservation organizations, with over 5 million supporters and aglobal network active in more than 100 countries.

WWF’s mission is to stop the degradation of the planet’s naturalenvironment and to build a future in which humans live in harmonywith nature, by conserving the world’s biological diversity, ensuringthat the use of renewable natural resources is sustainable, andpromoting the reduction of pollution and wasteful consumption

The Stiegler’s Gorge Hydropower Dam Project

The Stiegler’s Gorge project is being planned in the Selous Game Reserve. This paper providesbackground and analysis of the actors and risks involvedin the project, aiming to help WWF developan informed opinion on the project. This report is the result of an analysis of the literature availableand draws on extensive research carried out bythe lead author, Barnaby Dye1.

It was based on JoergHartmann(2012)’s Stiegler’s Gorge Briefing for WWF who also advised on this document.
 

Attachments

Environmental imperialism

The same applies na wale wanaopinga project ya Barabara Serengeti. As a matter of fact waliweza kuwarubini (?) au kuwapa pesa owners wa Jamiiforums kiasi threads za kupinga project ya Serengeti zikaweka sticky na kupewa vipaombele humu jamii forums.

Mind you, this forums is supposed to be non partisan and neutral kwenye issues mbali mbali lakini tazama hizo threads za sticky utadhani sote humu watoto hatuna akili ya kujua ambo mbala tuwe preached upon na akina JF na watu wao wa DSTV

BTW...

HQ za hizi eco terrosists organisations zinazipinga miradi ya maendeleo Tanzania ziko Nairobi Kenya


Go figure
 
Watulie, Magufuli amesema EIA itafanyika baada ya ujenzi, Yani ni sawa na kumtia mimba msichana halafu baada ya kujifungua unamwambia mkapime kama mna ngoma. 🙄.

All in all wafunge midomo yao hii ni ardhi yetu na tunauwezo wa kuifanyia tunachotaka tunasema ni "Sovereignty of the state"
 
Hawa WWF wakafie mbali!, kwa sababu uamuzi kuhusu Mradi huu, umeishafikiwa, hivyo uhamasishaji wa mjadala huu ni too little too late!.

Hoja za msingi za WWF ni hizi

  1. Mradi huu utaathiri Selous Game Reserve ambayo ni moja ya World Heritage Sites hivyo ujenzi katika eneo hili utaathiri ecology ya Selous kwa kuathiri mazingira, yatakayoathiri uchumi na maisha ya watu, hoja hii inakuwa defeated na manufaa ya Mradi huo ukilinganisha na athari za Mradi huo, manufaa ni makubwa mara 1000 kuliko athari!.
  2. Eneo litakalotumika ni kilomita za mraba 1,200km2, hivyo kulifanya kuwa bwawa kubwa kuliko yote eneo la Afrika Mashariki, hivyo litakausha maziwa madogo madogo yote ya jirani, litaathiri utalii, na kukomba fertility yote ya Ardhi ya eneo hilo hadi kwenye Delta ya Rufiji Delta, hivyo kuua samaki, na kuathiri uvuvi wa Kamba samaki na kamba koche unaotegemewa ka watu 200,000 wa eneo hili, pia hoja hii inapigwa chini kwa hoja kuwa Tanzania tuna maeneo mengi ambayo ni waste land, what is km za mraba 1,200?. Hao watu 200,000 watakaothiriwa na Mradi huo ni nini ukilinganisha na Wamasai wanaishi ndani ya eneo la hifadhi ya Loliondo ambao hawaruhusiwi kulima, bali wanalishwa bure?. Kwa vile faida za Mradi ni kubwa, serikali inaweza kuwaambia watu hao 200,000 wasilime na badala yake watalishwa bure maisha yao yote, hivyo Mradi uendelee!.
  3. Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!, Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo, kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa, to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.
  4. Mradi huo utaazuia tani milioni 16.6 za virutubisho vya Ardhi kwa mwaka, hivyo kusababisha mmomonyoko wa Ardhi kwenye Delta ya Rufiji, hii pia sio hoja, kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania, shughuli za kibinaadamu kama uchimbaji wa madini, unaleta athari kubwa zaidi za kimazingira na kusababisha sio tuu mmomonyoko Mkubwa wa Ardhi, bali kutuachia mahandaki mengi na makubwa Zaidi kuliko hizo tani milioni 16.6 kwa mwaka, hivyo Mradi utaendelea!.
  5. Hoja kuwa Mradi huo utaathiri sio tuu Mbuga ya Selous, bali pia Delta ya Rufiji na Bonde la Mto Kilombero, hapa tena tunaangalia faida za Mradi na kulinganisha na athari za kimazingira, then faida za Mradi ni kubwa kuliko athari!, Mradi utaendelea!.
  6. Hawa wazungu na wana mazingira ni watu wa ajabu sana, nakumbuka walivyotucheleweshea Mradi wa Kihasi kwa ajili tuu ya vyura wa Kihansi hadi Marekani walipokubali kuwahamisha vyura hao hao kuwahifadhi nchini Marekani, kisha kuwarudisha ndipo Mradi ukapitishwa!, yaani vyura walikwamisha mradi muhimu, ujinga huu walimfanyia Nyerere na Mwinyi, lakini kwa Magufuli, watagonga mwamba!.
  7. Hata Mradi wa Kamba Samaki kwenye Delta ya Rufiji, ulikwamishwa na wanamazingira kwa hoja kuwa Mradi huo utaathiri hifadhi ya miyombo!, what is miyombo compared to manufaa ya kiuchumi?.
  8. They can just go to hell, kama katiba ya Tanzania imekanywagwa for the expense ya maendeleo, rais Magufuli aliruhusu tuachane na na hizi EIA katika kupushi Tanzania ya Viwanda, hivyo sasa hapa ni kazi tuu, hakuna cha mazingira, world heritage wala cha nini, Tanzania tunataka Umeme wa kutosha kuendeshea Tanzania ya viwanda!
Hoja zote hizo ni katika kulinda kitu kinachoitwa the sovereignty of our nationalism kwamba Tanzania ni ya Watanzania, tuna uhuru wa kupanga mambo yetu kwa manufaa yetu bila kuingiliwa na mtu mwingine yoyote, hivyo hawa WWF, wasituingilie!.

Lakini on the other hand, kiukweli kabisa japo mimi sio mchumi, lakini sera za uchumi za serikali ya Magufuli ni sera za ajabu sana!.
  1. Huu Mradi wa Umeme wa Stglers Gorge ulizungumzwa tangu Enzi za Nyerere na haukutekelezwa kutokana na hixo hizo environmental concerns na mpango wa Tanzania Power System Master Plan (2016 update), umeonyesha Mradi huu ndio the last option kama miradi mingine mikubwa itashindikana, Mradi wa priority ni Umeme wa kutumia gesi, lakini sasa Magufuli kaingia, mara ghafla hatuzungumzii tena Mradi wa Umeme wa gesi, sasa Mradi huu ndio kipaumbele!, kipaumbele for what?.
  2. Japo ni kweli, the cheapest power generation projects ni hydropower projects, lakini Tanzania hatujifunzi tuu, kutokana na global warming na mabadiliko ya tabia nchi, kuendelea kutegemea Umeme wa maji ni very unpredictable, Richmond ilisababishwa na hii over dependency on hydropower, hivyo kulipotokea ukame, kilichotukuta sote tunakijua!, sasa gesi tunayo tena ya kutosha, na Umeme wa gesi, japo ni expensive kuliko hydro ni cheap kuliko diesel generation, kwa nini tusijikite kwenye gesi yenye uhakika, tunataka kuzamisha matrilioni ya Fedha kwenye pata potea nyingine ya kutegemea mvua?.
  3. Maajabu ya uchuni wa Magufuli pia yapo kwenye kuishadadia sana hii SGR, kama tumekuwa na reli mbili ya meter gauge ya Kati na Tazara, zote zina under perform, tumeanzisha bandari kavu ya Isaka ili ipokee mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC, lakini haifunction na reli ya kati ipo, tena hadi eneo la ICD ya Rwanda watu wanalima tuu mahindi!, hii SGR italeta miujiza gani?.
  4. Uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo Tanzania ya kweli ya viwanda, ni Tanzania ya agro processing industries, tunahubiri Tanzania ya viwanda, bila kuinua sekta ya kilimo, hivyo viwanda ni malighafi gani ya kuendesha Tanzania ya viwanda kama sekta ya kilimo ni totally neglected, Magufuli yuko bize kununua ndege na kujenga miundombinu, what has ndege, barabara za juu kwa juu, uwanja wa ndege wa Chato, na hii SGR has to do with sekta ya kilimo?.
Mimi bado nasisititiza, Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT

Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136!

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi?

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi?.

P
 
Tanzania ni ya watanzania.

Ni upuuzi mtu kukaa Washington alafu atupangie watanzania namna ya kutumia rasilimali zetu!

Hawa jamaa hawatutakii mema. This is imperialism at its best.

Yani wanaguswa zaidi na nyumbu wa Sealous kuliko watanzania mamilioni ambao wanaishi gizani?

Ni upumbavu zaidi kuwasupport hawa jamaa!

Trump anasema "America first", na sisi tunasema Tanzanians first!
 
SISI CHADEMA TUNKUBALIANA NA WWF KWANI HIZO PESA TUKIZIWEKA KWENYE UMEME WA GASI MBONA HIZO UNITI TUNAZIPATAT TU AU WEWE P UNSEMAJE?KWANZA HUAJFANYA RESEARCH KAMA MWANAHABARI NGULI
"sisi CHADEMA"

wewe ni msemaji wa CHADEMA?
 
WWF wana logic ila katika hili watuache tu maana umeme tunauhitaji sana kuliko wanavyodhani.

Hatuwezi kuchagua vyura badala ya umeme, naelewa ecology but kwa hapa watuache tu maana tushateseka sana
 
Back
Top Bottom