X ameninunia!!!

Mapenzi siyo vita wewe binti.
 
Linda moyo wako kuliko vyote uvilindavyo maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima!
 
Nyie mtarudiana tu, mpo kwenye mitihani ya kawaida tu
Hapana mkuu, kinachotufanya tuwe karibu ni ndugu wa pande zote mbili. Wamezoeana hata likitokea jambo lolote lazima wajumuike, imekua kama mimi na x tumeunganisha undugu af wenyewe tunagombana.
 
Jambo lako dogo sana,kwavile unamawasiliano na ndugu zake,wewe wape ndugu zake mzigo wa ex wako,then wakatie Umeme na maji.
Katika ugomvi wetu miiko yetu ni kwamba hakuna kuhusisha ndugu zetu kujua kuwa tumekorofishana au kufanya jambo ambalo litawafanya wao wahisi. Mfano mzigo akiniambia niwape ye atajua atawaambia nn na mi nitawapa bt nikitoa bila ye kujua nampa ndugu yake itakua shida so kama mwenyewe hautaki basi nitaacha kabatini hadi atakapojisikia kumuomba mtu amchukulie.
 
Acha kusumbua watu
Ye ndiye msumbufu, hana misimamo. Kama akiamua tuwe na ugomvi forever mi sina tatizo, akiamua tuchukuliane kama marafiki wa kawaida sana naona sawa but shida anataka special care kama nilivyomcare akiwa my boyfriend. Nikikataa ananuna, nikimchunia anakunywa pombe ananitafuta, mi na yeye nani msumbufu!
 
Kama hapokei sim si umwache? Ama wataka kuwa kama ulivyo conclude?
Nimemuacha but nashangazwa na tabia za kitoto za namna hii, mtu mzima lazima ujue kusema nataka ili na lile kama huwezi kunyoosha maelezo alaf unanuna tu, ni tatizo
 
Hivi inakuaje unakua na mazoea na ex wako jamani...loh!! Me hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…