LED TV Vs Plasma TV
i.)Unene
- LED TV huwa nyembamba mara nyingi chin ya nchi moja ,Plasma TV huwa chini ya nchi 1.2 .
ii.)Matumizi ya umeme
- LED TV hutumia umeme kidogo ukilinganisha na Plasma TV.
iii.) Ukubwa wa kioo
- LED TV hii huenda hadi nchi 90 na huanzia nchi yoyote ambayo kiwanda kinataka ,Plasma TV yenyewe huanzia nchi 42 hadi 65 Panasonic wana model kubwa hadi inchi 152.
iv.)Muda wa kuishi(Life span)
- LED TV hii huenda hadi masaa 100,000 , Plasma TV hii huenda kati ya masaa 20,000 hadi 60,000.
v.)Gharama
- LED TV hii ipo juu kidogo ukilinganisha na Plasma TV.
vi.)Angle kwa mtazamaji
- LED TV yenyewe hutegemea sana na jinsi mtazamaji alivyokaa ule muonekano(brightness and color) wake wa screen hubadilika kulingana na mtazamaji angle aliyokaa ,Plasma TV yenyewe muonekano hubaki vile vile hata kama mtazamaji atabadili angle ya utazamaji.
vii.)Uwiano wa mwanga(contrast ratio)
- LED TV uwiano wake sio mzuri sana kama ilivyo kwa plasma tv hii hutoa mwanga mweupe mkali lakini pia hutoa miale mweusi inayong'aa ambayo humfanya mtazamaji awahi kuchoka macho anapotizama tv yake hasa kwenye chumba cha giza ,Plasma TV hii hutoa miale mweusi yenye giza na mweupe iliyofifia ambayo mara nyingi humfanya mtazamaji kuwa comfortable zaidi haiumuuzi macho anapoangalia tv na kwenye mwanga mkali plasma tv hautaona vizur kwenye mwanga hafifu hii ndiyo yenyewe macho yanachelewa kuchoka.
viii.)Uzito
- LED TV zenyewe ni nyepesi ukilinganisha na Plasma TV ambazo ni nzito.
ix.)Unene wa kioo(screen)
- LED TV kioo chake ni chembamba ,Plasma TV kioo chake ni kinene.
x.)Matumizi ya energy
- LED TV hutumia energy kidogo ukilinganisha na Plasma TV.
xi.)Watengenezaji(kampuni)
- LED TV hutengenezwa na makampuni yote ya TV ,Plasma TV hutengenezwa na Panasonic,LG,Samsung.
xii.) Ufanyaji kazi katika mazingira magumu
- LED TV chini ya nyuzi joto 50f contrast hupungua ,Plasma TV urefu wa futi 6500 huathiri Ufanyaji kazi wake kwa sababu ya gesi iliyopo ndani husumbuliwa na kufanya itumie nguvu ya ziada inapofanya kazi.
xiii.)Teknolojia inayotumia
- LED TV hii hutumia diodes ambazo hutoa mwanga ambapo baadhi ya hiI mianga huzuiliwa na liquid crystals ambazo huwa zipo kwa wima au mlalo na kuunda picha au taswira halisi ambayo hutokea kwa kioo na mtazamaji kuweza kuona ,Plasma TV hii taswira hutengenezwa kwa kutumia phosphors ambapo vyombo vidogo/tiny vyenye plasma huwekwa katikati ya sheets mbili za glass na kuzalisha mwanga wa ultraviolet kwa kioo kwenye maeneo ya phosphor ambazo huglow na kutengeneza picha ambayo sisi tunaiona.
xiv.)Ubora wa sauti
- LED TV kwa vile nyembamba hata speaker zake huwa ni ndogo ambapo hutoa sauti isiyo na ubora ukilinganisha na Plasma TV.
xv.)Umaarufu
- LED TV zenyewe zinajulikana sana na watu wengi hutumia hizi , Plasma TV zenyewe sio maarufu sana kwa watu wengine hata hawajui kama zipo mfano tu hapa Tz kama zipo basi zinahesabika lakini pia hizi ni maarufu sana kwa kuwa na size kubwa ya kioo/screen.