X Vs Y

X Vs Y

Tubular Tyre Vs Tubeless Tyre

- Tairi yenye tube ni aina ya tairi ambayo upepo hujazwa kupitia kitundu maalum cha tube ambacho kimeunganishwa na hiyo tube ambayo hukaa katikati ya tairi la nje na rim wakati Tairi isiyo na tube yenyewe haina tube so upepo hukaa katikati ya rim na tairi yenyewe.

- Tairi ya tube yenyewe pancha yake hutokea kwa haraka upepo huisha fasta sana na wakat mwingine huweza poteza balance kwa dereva akiwa kwenye mwendo wakat Tairi isiyo na tube yenyewe pancha ikitokea upepo hutoka taratibu na humsaidia dereva kusimama kwa urahisi zaidi.

- Tairi ya tube yenyewe ni nzito wakat Tairi isiyo na tube ni nyepesi.

- Tairi ya tube haina gharama ukilinganisha na Tairi isiyo na tube yenyewe ipo juu kwenye gharama ya manunuzi.

- Tairi ya tube yenyewe gharama ya kuitunza ipo juu mfano pancha hutokea mara kwa mara wakati mwingine sio lazima kitu cha ncha kichome ule tu msuguano wa tair na rim tube hupata tabu sana na mwishowe huvujisha hewa ukilinganisha na Tairi isiyo na tube yenyewe pancha hutokea mara chache zaid.

- Tairi ya tube haiko comfortable kuna wakati mwingine unakuta ile pressure ya tairi haipo sawa tairi nzima inapishana ukilinganisha na Tairi isiyo na tube yenyewe ipo comfortable zaid na hata kwenye speed kali chombo cha moto kinakuwa kipo stable kutokana na ile faida yake ya tairi nzima kujaa upepo na ndiyo maana huwezi kuta mfano gari za formula one zinatumia Tairi ya tube .

- Tairi ya tube hutumika na vyombo vichache vya usafir ukilinganisha na Tairi isiyo na tube.

- Tairi ya tube kwa vile nzito hivyo mafuta huongezeka kidogo kutumika tofauti na Tairi isiyo na tube yenyewe kwa vile nyepesi basi mafuta huenda kidogo.

- Tairi la tube huchukua muda mrefu sana kuziba pancha mpaka utoe tube ya ndani uanze kutafuta pancha tofauti na Tairi isiyo na tube yenyewe huchukua muda mchache kuziba pancha na ni fasta tu ukishaiona unatumia ile gundi yake ya kuzibia basi umemaliza.
FB_IMG_1646921026379.jpg
FB_IMG_1646921141049.jpg
FB_IMG_1646921093195.jpg
 
Pikipiki yenye 125cc Vs Pikipiki yenye 150cc

- Kwa kifupi sana na kwa lugha nyepesi kadri CC(Cubic Centimetres) inavyozidi kuwa kubwa ndivyo chombo cha moto kinakuwa na power kubwa,speed kubwa na mtikisiko mdogo unapokuwa kwenye mwendo mkali(speed kubwa) bila ya kusahau mafuta pia yanaenda sana.

- Cubic Centimetres tunayozungumzia hapa ni ule ujazo wa silinda(cylinder) wa injini ambapo combustion(mchanganyiko wa mafuta na hewa ambao hutoa joto) ndiyo hutofautiana ukubwa kadri namba zinavyopanda ndivyo nayo inaongezeka ukubwa , cc kubwa inauwezo mkubwa wa kuhold hewa na mafuta na hatimaye engine kuweza kutoa power kubwa na torque ya chombo husika.

- 125cc injini yake ina tumia mafuta machache na pia gharama yake ipo chini ambapo ni kinyume na 150cc.

*yote ya yote inategemea unataka pikipiki kwa ajili ya matumizi yapi kwa sababu zipo bike [emoji605] za hadi 6200cc kama ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida tu hata 100cc inatosha sana pia inategemea na mfuko wako wa pesa maana kuna pikipiki gharama zake ziko juu magari yenyewe yanapigwa bao *
FB_IMG_1647023766349.jpg
FB_IMG_1647023654790.jpg
 
Dell inazingua kiongozi bora hata hp

Kwanza ina moto sana utasema pasi pamoja na kuwa na feni nyuma kuliko hata hp


Kwenye game sasa hasa pes graphics mbaya kichizi sometimes Ina scratch ukute Hapo specifications zote za kusupport game husika zipo ram ya kutosha ,icore ,window iko vizuri ila hp ukiweka game unateleza


Betri zake zinaisha haraka labda uki type unaweza tumia kwa 3hrs ila ukiangalia movie dooh imekata mazima na betri ikiisha ndio basi tena zote utakazobata utatumia saa moja yaani kiufup inanyonya sana betri hp betri masaa hadi matano ucheze game uangalie movies iko poa sana


Ila kwenye spear ndio naikubali ikiharibika mfano keyboard spear kupata ni rahisi mnooo tofauti na hapo

Nunua

Hp ,na Lenovo .




Talking with my own experience
 
Dell inazingua kiongozi bora hata hp

Kwanza ina moto sana utasema pasi pamoja na kuwa na feni nyuma kuliko hata hp


Kwenye game sasa hasa pes graphics mbaya kichizi sometimes Ina scratch ukute Hapo specifications zote za kusupport game husika zipo ram ya kutosha ,icore ,window iko vizuri ila hp ukiweka game unateleza


Betri zake zinaisha haraka labda uki type unaweza tumia kwa 3hrs ila ukiangalia movie dooh imekata mazima na betri ikiisha ndio basi tena zote utakazobata utatumia saa moja yaani kiufup inanyonya sana betri hp betri masaa hadi matano ucheze game uangalie movies iko poa sana


Ila kwenye spear ndio naikubali ikiharibika mfano keyboard spear kupata ni rahisi mnooo tofauti na hapo

Nunua

Hp ,na Lenovo .




Talking with my own experience
Thanks for sharing mambo kama haya sasa
 
Xbox Vs Playstation (PS)

-Xbox mmiliki ni Microsoft corporation ,PS mmiliki wake ni Sony Interactive Entertainment.

- Xbox ni kifaa cha kuchezea game ukiwa zako nyumbani tokea mwaka 2001 ,PS ni kifaa cha kuchezea game ukiwa nyumbani kwako tokea mwaka 1994.

- Xbox hutoa games zao pamoja na PC version nikamaanisha kuwa unaweza kuzicheza kwenye PC bila kutumia nguvu ya ziada PS wapo tofauti.

- Xbox wanaofa games chache free ukilinganisha na PS wenyewe wanaofa game nyingi zaidi free.

- Xbox haisapoti VR wakati PS inasapoti na ipo compatible na VR headset (Virtual Reality) na PS Plus.

- Xbox yenyewe ni nzito 2.9 hadi 3.81kg wakati PS yenyewe ina 2.1 hadi 3.3kg.

-Xbox na PS wote walitoa model mpya November 2020 ambapo Xbox walitoa Xbox series ambayo ni simple na kama box flan hv muonekano wake ambapo inachukua nafasi kubwa tofauti na PS 5 nyembamba ina umbo jembamba na inavutia ambayo huchukua nafasi ndogo.

- Xbox matoleo yao waliyotoa ni Xbox, Xbox 360, Xbox One, Xbox One S, Xbox One X, Xbox Series S, Xbox Series X wakati PS matoleo yao waliyotoa ni PlayStation, PlayStation 2, PlayStation 3, PlayStation 4, PlayStation 5, PlayStation Pro.

-Xbox ina wapenzi wachache na kuna wengine wengi tu hawajawahi kuona Xbox console hata moja ,PS ina wapenzi wengi zaidi kifupi wengi hutumia PS ndiyo wameizoea zaidi.

Xbox na PS zote ni consoles nzuri zina tofauti ndogo sana inategemea na muhusika anapendelea games za aina gani hasa maana wote wana games kali hizi zote ni kampuni kubwa Microsoft Vs Sonyi
FB_IMG_1647439819713.jpg
FB_IMG_1647439733615.jpg
FB_IMG_1647439864480.jpg
 
Sleeping [emoji99][emoji99] Vs Napping [emoji42]

- Sleeping ni kitendo cha mwili kupumzika baada ya uchovu wa siku nzima ili uweze kurudi katika hali yake ya awali uamkapo huchukua muda mrefu ambapo unashauriwa masaa 8 na mara nyingi inakuwaga usiku ila napping ni kupumzika pia ila huwa ni kwa muda mfupi na mara nyingi huwa mchana kuvuta nguvu ya kuendelea na kazi.

- Sleeping iwe nzuri na tamu mtu anatakiwa alale kitandani au sehemu yoyote ambayo ataona inamfaa kwake mahali palipo tulia penye utulivu ila napping yenyewe hata kwenye benchi au kiti hufanyika.
FB_IMG_1647695442087.jpg
 
DSTV vs Azam TV

- DSTV ni mkongwe kwenye hizi mambo tokea miaka ya 1995 wakati Azam TV yenyewe ni ya juzi tu hapa miaka ya 2013 hivi

- DSTV hii ni kampuni ya South Africa wakati Azam TV yenyewe ni ya hapa hapa Bongoland kwetu hata kwa mguu unaenda.

- DSTV yenyewe ina channels nyingi za HD tofauti na Azam TV.

- DSTV gharama za kununua dish [emoji341] ziko chini wakati Azam TV yenyewe gharama zake zipo juu hata bei ya antenna [emoji687] ipo juu kuliko bei ya kununulia dish la DSTV.

- DSTV Ina gharama kubwa sana kwenye vifurushi vyake ukitaka kuona channels zote za DSTV inabidi ujipange lakini Azam TV yenyewe gharama zake za vifurushi zipo chini mtanzania anao uwezo wa kulipia hata kile kifurushi cha juu kabisa japokuwa kuanzia mwezi wa 4 wanapandisha bei ila hawapandishi bei kubwa sana mfano kifurushi cha elfu 20 kitakuwa elfu 23.

- DSTV ina channels nyingi sana za nje na michezo mingi pia ya kila aina wakat Azam TV nayo inayo channels chache za nje na za michezo zipo japo huwez fananisha na DSTV sema kinachompa kiburi Azam TV ni ile karata aliyocheza imemlipa vibaya mno kuona hapa hapa Tanzania kuna soko na watu wapo kwa kutoa kipaumbele hapa kwanza na kubwa zaidi kujitosa mazima kuonesha ligi kuu ya bongo (NBC PREMIER LEAGUE) ambapo DSTV alifanya kosa ambalo atajuta hadi basi kuidharau ligi ya Tanzania na kuona hela hamna sasa hivi anaitaman sema ndiyo hivyo ameshachelewa.

- DSTV mmiliki ni multichoice wakat Azam TV ni billionaire Saidi Salim Bakhresa.

- DSTV walikuwa wanajiona keki sana kipindi hicho ila sasa hv ukitaka dish wanakuletea hata nyumbani kwako bila shida yoyote ile DSTV sasa hivi mpinzani wake wa kibiashara ni Azam TV na ndiyo maana sasa hivi naye anajitahidi kuweka vipindi vya kibongo mfano wakawarudisha original comedy japokuwa bado watu hawajaipokea kivile kama enzi zile sasa hivi ukiweka hiyo original comedy na kombolela ya Azam TV wadau watacheki kombolela kwanza ikiisha ndiyo watakuja kwenye original comedy.

- DSTV ni mkongwe sawa sikatai wanasema aliyetangulia ametangulia tu ila akae vizuri mambo yanaenda kwa kasi sana kwa sababu Azam TV ni ya juzi ila wanakuja vizuri sana wamejipanga sasa hivi wameingia hadi south afrika na akiendelea hivi ipo siku dish za DSTV zitakuwa za kuhesabu kama enzi zile wenye DSTV ni watu wenye hela tu ila sema safari hii itakuwa kinyume DSTV hana ishu tena ,
FB_IMG_1648217720861.jpg
FB_IMG_1648217680707.jpg
FB_IMG_1648219879996.jpg
FB_IMG_1648219901576.jpg
 
Saa ya mshale(analog watch) Vs saa ya kukonyeza(digital watch)

i.) Analog ni za kitambo tokea miaka hiyo 1656 na ni maarufu zaid ya digital.

ii.) Digital unaweza kusoma saa hadi usiku bila shida kabisa tofauti na analog.

iii.) Analog yenyewe huvutia zaidi kuvaa mbele ya watu kwenye matukio na pia watu wazito wazito hupendelea zaid kuvaa analog tofaut na digital yenyewe huvaliwa na kila mtu.

iii.) Digital cku hizi zimeendela sana kama smart watch ambayo ina vitu vingi tofauti na kuangalia saa tu peke yake tuseme ni kama komputa ndogo kama vile unaweza piga simu,pokea meseji,kusoma mapigo ya moyo ufanyapo mazoezi na vingine vingi.

iv) Digital huwa ni rahisi kuharibika wino tu ukizingua mfano ukiiangusha basi imeisha hiyo lakini analog yenyewe huwa ni ngumu sana sio rahisi kuharibika unaweza kuta babu yako anayo na anaitumia hadi leo tokea enzi zake za ujana huko amenunua.

v.) Digital ni rahisi kusoma muda sekunde moja tu inatosha kusoma saa ila analog yenyewe sio rahisi kihivyo na wengine hawawez kusoma.
FB_IMG_1649950885767.jpg
FB_IMG_1649950817421.jpg
 
MRI Vs CT Scan

- MRI kirefu chake ni Magnetic Resonance Imaging wakati CT Scan kirefu chake ni Computed Tomography.

- MRI tekinolojia hii hutumia mawimbi ya redio(radio waves) na sumaku wakati CT Scan hutumia mionzi ya X-rays.

- MRI hutumika kuchunguza maungio ya mifupa,akili,viwiko,enka,matiti,moyo na mishipa ya damu.joints wakati CT Scan hutumika kuchunguza mivunjiko ya mifupa,uvimbe,kumonita kansa na kutafuta mivujo ya damu ndani ya mwili.

-MRI inavyofanya kazi yenyewe kunakuwa na constant magnetic field and radio frequencies ambayo kwenye fat(mafuta) na molecules za maji ya mwili wako then radio waves zinasafirishwa kwenye receiver ya mashine ambapo hutafsiriwa kwa picha ambayo sasa daktar anaweza itumia kuona na kujua shida ni nini pia utatakiwa kutulia wakati ukifanyiwa na utapewa headphones kwa ajili ya kukukinga na sauti zinazozalishwa kwenye mashine maana hutoa sauti.

-CT Scan yenyewe inavyofanya kazi utaambiwa ujilaze kwa meza halafu hiyo meza ndiyo itakuwa inatembea kwenye CT scan ili kupiga cross-sectional picha ndani ya mwili wako na baadaye daktar ataichukua na kucheki shida ni nini.

- CT scan hutumika zaidi ya MRI pia gharama yake ipo chini so wengi huweza kulipia na kufanya hichi kipimo na pia kipo fasta.

-MRI yenyewe ipo vizuri zaidi kwenye ubora wa kutoa details za picha kulinganisha na CT Scan.

-kama tujuavyo hakuna kisichokuwa na madhara hata panadol ina madhara yake zote mbili zina madhara kwa mtumiaji na hutofautiana kulingana na aina ya picha unayopigwa na eneo husika la hiyo picha inapopigwa tukianza na CT Scan madhara(risks) yake ni huweza kumdhuru mtoto/watoto ambao bado hawajazaliwa,kuna dozi kidogoo sana ya mionzi(radiation) na huweza kumsababishia mteja reaction kutokana na zile dyes zinazotumika ,MRI risks zake ni kama vile kusababisha reactions kama mteja ana chuma ndani ya mwili kwa sababu yenyewe hutumia sumaku,sauti kubwa inayoweza kupelekea ishu kwenye usikivu,joto la mwili kuongezeka inapotumiwa kwa muda mrefu na claustrophobia(hii ni hofu na woga uliopitiliza unayozalishwa na mgonjwa au mteja pale anapokuwa ndani ya mashine ya MRI tunajua kuwa mashine yenyewe inafanana na space).

N.B; zote mbili hutumika kupiga na kukamata picha mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu kwa kumsaidia daktar kujua shida hasa ni nini kwa mgonjwa na pia zina madhara madogo kwa mtumiaji zote humsaidia daktar na yeye ndiye atakayeorder ni ipi ufanyiwe kulingana na case yako ilivyo.
IMG_20220416_160215.jpg
FB_IMG_1650114013688.jpg
FB_IMG_1650113886350.jpg
 
Supercars Vs Hypercars

- Supercars ni zile gari ambazo ziko na best performance, tekinolojia na muonekano mzuri zinaweza zisiwe na hivi vyote vitatu na bado ikawa supercar wakati Hypercars zenyewe ni zaidi na lazima ziwe na hivyo vitu vitatu hapo juu vyenye ubora wa hali ya juu zaidi.

- Hypercars zote ni supercars ila sio supercars zote ni Hypercars.

- Mara nyingi Hypercars huwa na horse power 900+++ ila supercars huwa na horse power hata chini ya 800.

- A supercars kama vile Audi R8/Gallardo/AMG SLS/Ferrari 599 , Hypercars kama vile Pagani Huayra/the Bugatti Veyron/the Enzo.

- Hypercars ni supercars ambazo zipo kitofauti zaidi gharama yake pia ipo juu na kubwa zaidi huzalishwa kwa idadi maalum hutengenezwa chache na kibongobongo hadi unakufa unaweza usiione ana kwa ana kwa macho mawili.

FB_IMG_1650718141704.jpg
FB_IMG_1650718428066.jpg
 
AK-47 VS M16

- AK 47 ni bunduki ya Soviet wakat M16 ni ya mmarekani zikitumika tokea miaka ya 1960.

- AK 47 mtengenezaji ni Kalashnikov (formerly Izhmash),Tula Arms Plant, TsNIITochMash,Zastava,Norinco, Arsenal Arms ArmaLite, Bushmaster, Colt, GM, H&R, FN wakati M16 inatengenezwa na ArmaLite, Bushmaster, Colt, GM, H&R, FN, Remington.

- AK 47 iliundwa 1947 ,M16 mwaka 1957.

-AK 47 inauzito wa 4.78kg na 30 round magazine(10.5lb.) ,M16 yenyewe ni 3.6kg na 30 round magazine(7.9lb).

- AK 47 risasi yake ina uwezo wa kusafiri 710m/s na Ina uzito wa 7.9gram ikiwa na uwezo wa kupenya 74cm ,M16 risasi yake ina uwezo wa kusafiri 990m/s na Ina uzito wa 3.6gram ikiwa na uwezo wa kupenya 36cm.

- AK 47 ina urefu wa 87.0cm na range yake ni 350mita ,M16 99.0cm na range yake ni 460mita iko more accurate.

- AK 47 ina uwezo wa kupiga mizunguko 600 kwa dakika ,M16 ina uwezo wa kupiga mizunguko 700 hadi 950 kwa dakika.

- Matoleo ya AK 47 ni AK-47, AKS-47, RPK, AKM, AKMS, AK-74, RPK-74,
AK-100 series, AK-12 , na matoleo ya M16 ni AR-15,M16,XM16E1, M16A1, M16A2, M16A3, M16A4, M4, M4A1, M27, Colt 9mm SMG.

- AK 47 ni maarufu duniani zaid ya M16 ikiwa zimetengenezwa na kuuzwa zaidi duniani kote ,M16 yenyewe ni kinyume chake si maarufu kiivyo.

- AK 47 ikiwa na urefu wa barrel 40.6cm na kipenyo cha sight kikiwa ni 37.8cm ,M16 ikiwa na urefu wa barrel 50.8cm na kipenyo cha sight kikiwa ni 50.0cm.

- AK 47 inatengenezwa kwa steel na mbao ,M16 inatengenezwa kwa aluminum badala ya steel na fiberglass badala ya mbao na ndiyo maana ni nyepesi zaidi.

- AK 47 ilivyo ni straightforward ,M16 iko advanced kidogo.

- AK 47 iko vizuri sana kwenye mapigano ya karibu karibuhaikutenhenezwa kwa mapigano ya mbali iko poa sana kwenye mita 200 hapo japokuwa hadi 400mita itapiga tofaut na M16 hii ipo vizuri hata kwenye mapigano ya mita 400 hadi 500 hapo.

- AK 47 ni rahisi kutumia hata kuifanyia service ni rahisi ni ngumu na inadunda kwenye hali zote vumbi,mchanga twende huwa haijam kizembe na hapa ndipo inapopendwa zaidi ina sehemu nane ambapo kwa mzoefu hii bunduki anaweza kuifungua na kuirudishia tena hata akiwa amefumba macho tofauti na M16 inahitaji matunzo zaidi.

- M16 ina options nyingi unaweza kuweka attachment mbali mbali japokuwa AK 47 nayo sikuhizi wameboresha unaweza kuweka baadhi ya attachment na kuifanyia iwe bora zaidi
FB_IMG_1651314236329.jpg
FB_IMG_1651314210425.jpg
FB_IMG_1651314264558.jpg
 
Back
Top Bottom