Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 8,000
- 16,414
Kutakuwa na Xiaomi 16, 16 Pro na 16 Pro Max, yani kama iPhone
Xiaomi 16 na Xiaomi 16 Pro zitakuwa na vioo vyenye ukubwa sawa na Xiaomi 16 Pro Max itakuwa kubwa zaidi na ndio itakuwa na best specifications.
Simu zote tatu zinakuja na 100W charger, hii ni tofauti na Xiaomi 15 na 15 Pro za mwaka jana ambazo zilikuja na 90W charger.
Pia zitakuja na processor mpya ambayo Qualcomm wanatarajia kuizindua hivi karibuni "Qualcomm Snapdragon Elite 2" na Xiaomi ndio imekuwa kampuni ya kwanza kutangaza kuwa itatumia chipset hiyo kwenye simu zake.
Hata hivyo Xiaomi inatarajiwa kuachia simu hizi tatu kwa China pekee kwa mwaka huu, kisha huenda mwakani waka release Global version, hivi ndio wanavyofanya
Xiaomi ndio kampuni yangu pendwa ya simu, na kampuni hii ya Kichina inazidi kukua kila kukicha. Wana simu nyingi nzuri kuanzia low end, midrange hadi flagship na simu zao nyingi ni ngumu, durable, high quality na zina very good specifications.
Hata hizi flagship tatu zinazokuja ni lazima zitakuwa among the best flagships in the world