Ya Adani na Wachina: Hii ndiyo sababu kuu inayofanya Wanasiasa wetu wawachukie Wazungu

Kwa huu uzi wako tayari huyo adani ameshakuwa na hatia, kwa ushahidi upi usiotiliwa shaka kwamba habari yako ina ukweli mtupu ndani yake?.

Tatizo la taasisi nyingi za afrika tija inakuwa ni ndogo na sababu zipo nyingi sana. Ukiona wanasiasa wanakimbilia nje kutafuta taasisi za kigeni ujue hizi za kwetu zina matatizo mengi.

Wizi mwingi, nidhamu ndogo kazini, urasimu mwingi, badala ya taasisi kurahisisha maisha ya kijamii inakuwa ni sehemu ya kero zinazokwamisha kupiga hatua.

DPW kaleta tofauti pale TPA hivi sasa bandari yetu inaongoza kwa tija katika ukanda huu wa afrika, tulipokuwa sisi wenyewe tunaiendesha kila siku tulizoea kusoma habari za wateja kuelekea Kenya na Msumbiji wakiikimbia bandari iliyojaa upigaji wa kila aina.

Tambua kwamba wanasiasa na udhaifu wao wa miaka na miaka, wanalo lengo jema kutafuta wawekezaji wa kigeni.
Mwafrica siku akifanya jambo lake kwa weledi, haki, umakini, uzalendo na ukweli, dunia itakuwa imekwisha,.kuanzia mtawala mpaka chini.
 
Umeongea kweli mtupu kwa njia rahisi ambao viongozi wengi wa kiafrica hawataki wanaowaongoza waujue , hongera sana mkuu , ninaomba tupate wachangiaji wengi ili tuone tunaweza ondokana na hii kadhia kwa namna gani .
 
Inaongoza katika ukanda huu wa afrika, kwa maana ya afrika mashariki.
Unaposema ukanda wa Africa hapo unamaanisha Africa nzima.

Turudi kwenye hii afrika mashariki. Kivipi tunaongoza kwa tija afrika mashariki? Wewe umejuaje tunaongoza kwa tija? Umesoma reports ukaona hivyo au umejuaje? Hapo ndio nataka nielewe. Naomba reports zinazosema hivyo kutoka chanzo credible
 
Pamoja na yote Mzungu ni mtu aliyenyooka sana!

Mzungu kawekeza sana kwenye suala la utawala bora ambapo kupitia utawala bora amejenga Taasisi na mifumo imara sana zinazosimamia mambo na kuhakikisha yanaenda bila shida.

Kunyooka huku kwa Mzungu ndiko kumefanya sasa aanze kupoteza sana Africa. Hii ni kwa sababu Viongozi wa Afrika wanapenda sana Rushwa. Kupenda Rushwa kwa Viongozi wa Afrika ndiko kumefanya kwa sasa bara la Africa kuongoza kwa uwekezaji wa Wachina na Wahindi.

Mchina na Mhindi ni watu wanaoamini kuwa ili jambo lake liende lazima atoe Rushwa. Endapo siku ikitokea ukafanyika uchunguzi huru wa namna kandarasi za Wachina na Wahindi zinavyopatikana hapa Tanzania na Afrika nawaambia wananchi wetu wanaweza choma nyumba zote za Viongozi wetu sio tu Tanzania bali Afrika nzima.

Waendesha Mashtaka wa Marekani kufungua Mashtaka dhidi ya tajiri wa kihindi Adani ni funzo kubwa kwetu kuwekeza kwenye katiba bora inayojenga na inayosimamia mifumo imara. Mifumo isiyotoa nafasi kwa rushwa na kuhakikisha fedha zote za walipakodi zinatumika kwa maendeleo ya wananchi tu na sio kuwanufaisha wachache.

Hapa Tanzania Adani kapewa sehemu ya Bandari yetu. Huwezi sikia hata siku moja PCCB wakifanya uchunguzi. Na kamwe hatutosikia. Hii ni kwa sababu Adani ameingia Tanzania kupitia Ofisi namba moja.

Sio mara ya kwanza kwa mzungu kuonyesha umuhimu wa Mifumo na Taasisi imara kwenye utawala bora. Tanzania tulishawahi rudishiwa chenji yetu ya Rada baada ya Wazungu kugundua kuwa kampuni zao zilitupiga na wakazibana zikarudisha kweli.

Kuna kipindi Bandarini Wazungu waligundua kuna kampuni zao zilitoa Rushwa kupata tenda za kufunga mifumo ya tehama kwenye Bandari yetu. Ila pamoja na Ile kampuni kubanwa nchini mwao hapa kwetu hatujasikia hadi leo wahusika wakifikishwa Mahakamani.

Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.

Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.

Ipo siku

Lord denning
Qatar
Kweli ni uzi wenye maana lakini wabongo -----------------99.99% mazuzu, unfortunately!
Ukiangalia vile vimashine vya kamari --- Waziri wa Fedha anafurahi hajui ule ndiyo wizi wa dollar----
Rais na Waziri wa fedha wanaenda kukopa mkopo China wanapewa denomination kwa pesa ya kichina wao wana-sign watarudisha kwa Dollar ---------- na Mwigulu anachekaa ---- ati ana PhD!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umeongea kweli mtupu kwa njia rahisi ambao viongozi wengi wa kiafrica hawataki wanaowaongoza waujue , hongera sana mkuu , ninaomba tupate wachangiaji wengi ili tuone tunaweza ondokana na hii kadhia kwa namna gani .
Ukigundua, unadanganywa, unaibiwa, na kutapeliwa na mzungu, mchina, Mhindi, mwarabu na yeyote na bado unawakumbatia, wewe ni maiti inayotembea. Ila mwenye akili na yuko hai atajiondoa katika utumwa huo. Simpendi mweupe yeyote dunia, linapokuja swala la haki, huruma kwa mtu mweusi. Mtu mweusi asipojipambania atabakia punda wa mtu mweupe milele.
 
Pamoja na yote Mzungu ni mtu aliyenyooka sana!

Mzungu kawekeza sana kwenye suala la utawala bora ambapo kupitia utawala bora amejenga Taasisi na mifumo imara sana zinazosimamia mambo na kuhakikisha yanaenda bila shida.

Kunyooka huku kwa Mzungu ndiko kumefanya sasa aanze kupoteza sana Africa. Hii ni kwa sababu Viongozi wa Afrika wanapenda sana Rushwa. Kupenda Rushwa kwa Viongozi wa Afrika ndiko kumefanya kwa sasa bara la Africa kuongoza kwa uwekezaji wa Wachina na Wahindi.

Mchina na Mhindi ni watu wanaoamini kuwa ili jambo lake liende lazima atoe Rushwa. Endapo siku ikitokea ukafanyika uchunguzi huru wa namna kandarasi za Wachina na Wahindi zinavyopatikana hapa Tanzania na Afrika nawaambia wananchi wetu wanaweza choma nyumba zote za Viongozi wetu sio tu Tanzania bali Afrika nzima.

Waendesha Mashtaka wa Marekani kufungua Mashtaka dhidi ya tajiri wa kihindi Adani ni funzo kubwa kwetu kuwekeza kwenye katiba bora inayojenga na inayosimamia mifumo imara. Mifumo isiyotoa nafasi kwa rushwa na kuhakikisha fedha zote za walipakodi zinatumika kwa maendeleo ya wananchi tu na sio kuwanufaisha wachache.

Hapa Tanzania Adani kapewa sehemu ya Bandari yetu. Huwezi sikia hata siku moja PCCB wakifanya uchunguzi. Na kamwe hatutosikia. Hii ni kwa sababu Adani ameingia Tanzania kupitia Ofisi namba moja.

Sio mara ya kwanza kwa mzungu kuonyesha umuhimu wa Mifumo na Taasisi imara kwenye utawala bora. Tanzania tulishawahi rudishiwa chenji yetu ya Rada baada ya Wazungu kugundua kuwa kampuni zao zilitupiga na wakazibana zikarudisha kweli.

Kuna kipindi Bandarini Wazungu waligundua kuna kampuni zao zilitoa Rushwa kupata tenda za kufunga mifumo ya tehama kwenye Bandari yetu. Ila pamoja na Ile kampuni kubanwa nchini mwao hapa kwetu hatujasikia hadi leo wahusika wakifikishwa Mahakamani.

Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.

Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.

Ipo siku

Lord denning
Qatar
Mimi siamini moja kwa moja tuhuma hizi. Hata Elon Musk mzungu wa SA, tulianza kusikia amemsaidia Trump kushinda uchaguzi kwa kutumia/hongo kubwa. Kama angeshinda Kamala ungesikia Elon yuko matatani the same to Adani.
 
Kama Elon Musk katoa Rushwa lazima utakuja kuona anachunguzwa na kufikishwa Mahakamani. Huyo Trump tu ameshachunguzwa mara kadhaa na kufikishwa Mahakamani.

Mtoto wa Joe Biden, Rais wa sasa wa Marekani amechunguzwa na kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma kadhaa tena Baba yake akiwa Rais.

Huu ndo utofauti wa wazungu na sisi waafrika.
 
Unaposema ukanda wa Africa hapo unamaanisha Africa nzima.

Turudi kwenye hii afrika mashariki. Kivipi tunaongoza kwa tija afrika mashariki? Wewe umejuaje tunaongoza kwa tija? Umesoma reports ukaona hivyo au umejuaje? Hapo ndio nataka nielewe. Naomba reports zinazosema hivyo kutoka chanzo credible
Ushushaji na Upakiaji wa makontena kasi yake imeongezeka, muda wa kuhudumia meli moja umepungua.

Malalamiko ya wateja kuhamia bandari za nchi jirani yamepungua sana, mapato ya TRA yameongezeka sana.

Sio mimi niliyesema kuwa ubora wa kazi umeongezeka, ni gazeti mojawapo maarufu la kingereza linalotoka jijini Dar lilikuja na hiyo habari.
 
Huu ni ukweli mtupu. Uwekezaji kwenye Bandari hasa wa DP World umetunufaisha sana!
 
Pamoja na yote Mzungu ni mtu aliyenyooka sana!

Mzungu kawekeza sana kwenye suala la utawala bora ambapo kupitia utawala bora amejenga Taasisi na mifumo imara sana zinazosimamia mambo na kuhakikisha yanaenda bila shida.

Kunyooka huku kwa Mzungu ndiko kumefanya sasa aanze kupoteza sana Africa. Hii ni kwa sababu Viongozi wa Afrika wanapenda sana Rushwa. Kupenda Rushwa kwa Viongozi wa Afrika ndiko kumefanya kwa sasa bara la Africa kuongoza kwa uwekezaji wa Wachina na Wahindi.

Mchina na Mhindi ni watu wanaoamini kuwa ili jambo lake liende lazima atoe Rushwa. Endapo siku ikitokea ukafanyika uchunguzi huru wa namna kandarasi za Wachina na Wahindi zinavyopatikana hapa Tanzania na Afrika nawaambia wananchi wetu wanaweza choma nyumba zote za Viongozi wetu sio tu Tanzania bali Afrika nzima.

Waendesha Mashtaka wa Marekani kufungua Mashtaka dhidi ya tajiri wa kihindi Adani ni funzo kubwa kwetu kuwekeza kwenye katiba bora inayojenga na inayosimamia mifumo imara. Mifumo isiyotoa nafasi kwa rushwa na kuhakikisha fedha zote za walipakodi zinatumika kwa maendeleo ya wananchi tu na sio kuwanufaisha wachache.

Hapa Tanzania Adani kapewa sehemu ya Bandari yetu. Huwezi sikia hata siku moja PCCB wakifanya uchunguzi. Na kamwe hatutosikia. Hii ni kwa sababu Adani ameingia Tanzania kupitia Ofisi namba moja.

Sio mara ya kwanza kwa mzungu kuonyesha umuhimu wa Mifumo na Taasisi imara kwenye utawala bora. Tanzania tulishawahi rudishiwa chenji yetu ya Rada baada ya Wazungu kugundua kuwa kampuni zao zilitupiga na wakazibana zikarudisha kweli.

Kuna kipindi Bandarini Wazungu waligundua kuna kampuni zao zilitoa Rushwa kupata tenda za kufunga mifumo ya tehama kwenye Bandari yetu. Ila pamoja na Ile kampuni kubanwa nchini mwao hapa kwetu hatujasikia hadi leo wahusika wakifikishwa Mahakamani.

Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.

Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.
View attachment 3158628

Ipo siku

Lord denning
Qatar
Huu ni ukweli mtupu
 
Sisi ukimya wetu na kawimbo ketu haka ka amani, basi viongozi wamefanya ni advantage, wanatuona sisi ni zumbukuku ulimwengu uko huku.
 
Attachments

  • 5781825-51775523b226d8414338068b2d50cfec.mp4
    3 MB
  • IMG_3824.jpeg
    IMG_3824.jpeg
    50.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom