Ya Ally Hapi yaendelee kuwakumbusha vijana, madaraka ni koti la kuazima

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
413
Reaction score
471
Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ambapo tumeshuhudia baadhi ya sura mpya, wengine wakihamishwa lakini kuna ambao wamepewa mkono wa kwaheri, ingawa gumzo kubwa limekuwa kutemwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi.

Hapi ambaye amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baadae kuhamishiwa Mara anakumbukwa kwa matendo yake yenye ukakasi, vitisho, na matumizi yanaonekana kuwa mabovu ya madaraka katika sehemu alizohudumu.

Hapi ambaye wengi wanamtazama kama taswira ya vijana waliopewa dhamana na wakizidiwa uwezo na kushindwa kuyadhibiti maneno na matendo yao, anaingia kwenye kundi la vijana waliolewa madaraka na sasa wanarudi mtaani kama ilivyokuwa kwa Bwana Paul Makonda na Lengai Sabaya ambaye anapambana na kesi katika mahakama ya Tanzania.

Hapi huyu ndiye aliwachimba mkwara wazee, wastaafu akiwaambia waache kuwashwawashwa na popote watakapojitokeza atawatangwa, na kama kuna maovu walitenda watubu na wasituharibie Nchi yetu ya Tanzamia.
Aliwataka wastaafu Wastaafu wakae kimya kwani zama zao zimepita, wasituharibie nchi yetu wasimpotezee focus Rais MAGUFULI.

Aliwahi kumwambia mtumishi wa idara ya Ardhi huko Iringa kuwa asimchezee hata kidogo kwani yeye ni mtu hatari sana, sasa yule mtu hatari aliyewatisha kina Kinana, kina Kikwete ametumbuliwa amerudi kitaani na hapa ndipo anawakumbusha vijana kuwa wanapopewa madaraka wasijisahau na kudhani watakaa madarakani milele kwani madaraka ni kama koti la kuazima tu ipo siku mwenye koti lake atalichukua

Hapo.jpeg
 
Mbona nape na makamba wamepewa uwaziri wakati walimtukana na kumsengenya rais. Hivi wangemsema kikwete leo hii wangekuwa mawaziri?

Ally hajakosea sema tu inategemea wakati.
 
Alilewa sana Madaraka kufikia kuwapiga Mkwara Viongozi wastaafu...
 
Mbona nape na makamba wamepewa uwaziri wakati walimtukana na kumsengenya rais. Hivi wangemsema kikwete leo hii wangekuwa mawaziri?

Ally hajakosea sema tu inategemea wakati.
Ndio maana hoja hapa ni kwamba hakuna ajuaye kesho, tulinde ndimi zetu, alafu mifano uliyoitoa haiendani na situation ya hapi
 
Mbona nape na makamba wamepewa uwaziri wakati walimtukana na kumsengenya rais. Hivi wangemsema kikwete leo hii wangekuwa mawaziri?

Ally hajakosea sema tu inategemea wakati.
Kwa jins ikivyokuw ktk utawal ule Ni vigumu San kudhibiti miemko kwa wakt ule kwani nadhna kina happi walikuwa wanatumwa na watu fln kutoa matamko mazito mazito hapo
 
Wakati mwingine ni kujiongeza kupita kiasi tu
 
Pamona na hayo!.

Happy hapo alipo anaenda kusimamia mamiradi yake na kamwe hutakutana nae mkiwa mmeshika bomba za kwenye daladala
 
Hapi huyu ndiye aliwachimba mkwara wazee, wastaafu akiwaambia waache kuwashwawashwa na popote watakapojitokeza atawatangwa, na kama kuna maovu walitenda watubu na wasituharibie Nchi yetu ya Tanzamia.
Aliwataka wastaafu Wastaafu wakae kimya kwani zama zao zimepita, wasituharibie nchi yetu wasimpotezee focus Rais MAGUFULI.
Huyu dogo akapimwe mkojo tu
 
Hata hiyo Kauli ya uongozi ni koi la kuazima ipo kisiasa tu kitishiana na kuwafanya watu kutenda Mambo kwa uoga, maana hata hao waliosema walikua na maana yao.

Muhimu kwa viongozi wote si vijana tu, upatapo MAMLAKA ya kuongoza watu, kuwa mpole, shusha mabega, waheshimu wote, Kisha ongoza kwa kufuata kanuni na Sheria za kazi zako[emoji120]

TIME HEALS ALL WOUNDS
 
Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ambapo tumeshuhudia baadhi ya sura mpya, wengine wakihamishwa lakini kuna ambao wamepewa mkono wa kwaheri, ingawa gumzo kubwa limekuwa kutemwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi.

Hapi ambaye amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baadae kuhamishiwa Mara anakumbukwa kwa matendo yake yenye ukakasi, vitisho, na matumizi yanaonekana kuwa mabovu ya madaraka katika sehemu alizohudumu.

Hapi ambaye wengi wanamtazama kama taswira ya vijana waliopewa dhamana na wakizidiwa uwezo na kushindwa kuyadhibiti maneno na matendo yao, anaingia kwenye kundi la vijana waliolewa madaraka na sasa wanarudi mtaani kama ilivyokuwa kwa Bwana Paul Makonda na Lengai Sabaya ambaye anapambana na kesi katika mahakama ya Tanzania.

Hapi huyu ndiye aliwachimba mkwara wazee, wastaafu akiwaambia waache kuwashwawashwa na popote watakapojitokeza atawatangwa, na kama kuna maovu walitenda watubu na wasituharibie Nchi yetu ya Tanzamia.
Aliwataka wastaafu Wastaafu wakae kimya kwani zama zao zimepita, wasituharibie nchi yetu wasimpotezee focus Rais MAGUFULI.

Aliwahi kumwambia mtumishi wa idara ya Ardhi huko Iringa kuwa asimchezee hata kidogo kwani yeye ni mtu hatari sana, sasa yule mtu hatari aliyewatisha kina Kinana, kina Kikwete ametumbuliwa amerudi kitaani na hapa ndipo anawakumbusha vijana kuwa wanapopewa madaraka wasijisahau na kudhani watakaa madarakani milele kwani madaraka ni kama koti la kuazima tu ipo siku mwenye koti lake atalichukua

View attachment 2309125
Kwhy we ulitaka awe vipi labda au kosa lake liko wapi?
 
ni utashi wa anayeteua kumpa mtu nafasi au la kutokana na utaratibu na mipango yake, mbona kuna kuna watu kibao waliongea mambo mengi na wapo kwa nafasi kubwa?

Tumuache jamaa wa watu hizi tabia za utabiri utabiri na ramli tuachie wanaowezana nao, nchi haiwezi kwenda kwa tabia za kuunganisha matukio kwa kubahatisha bahatisha. Ni aina ya umaskini wa mawazo!
 
Back
Top Bottom