Ya Ally Hapi yaendelee kuwakumbusha vijana, madaraka ni koti la kuazima

Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ambapo tumeshuhudia baadhi ya sura mpya, wengine wakihamishwa lakini kuna ambao wamepewa mkono wa kwaheri, ingawa gumzo kubwa limekuwa kutemwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi.

Hapi ambaye amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baadae kuhamishiwa Mara anakumbukwa kwa matendo yake yenye ukakasi, vitisho, na matumizi yanaonekana kuwa mabovu ya madaraka katika sehemu alizohudumu.

Hapi ambaye wengi wanamtazama kama taswira ya vijana waliopewa dhamana na wakizidiwa uwezo na kushindwa kuyadhibiti maneno na matendo yao, anaingia kwenye kundi la vijana waliolewa madaraka na sasa wanarudi mtaani kama ilivyokuwa kwa Bwana Paul Makonda na Lengai Sabaya ambaye anapambana na kesi katika mahakama ya Tanzania.

Hapi huyu ndiye aliwachimba mkwara wazee, wastaafu akiwaambia waache kuwashwawashwa na popote watakapojitokeza atawatangwa, na kama kuna maovu walitenda watubu na wasituharibie Nchi yetu ya Tanzamia.
Aliwataka wastaafu Wastaafu wakae kimya kwani zama zao zimepita, wasituharibie nchi yetu wasimpotezee focus Rais MAGUFULI.

Aliwahi kumwambia mtumishi wa idara ya Ardhi huko Iringa kuwa asimchezee hata kidogo kwani yeye ni mtu hatari sana, sasa yule mtu hatari aliyewatisha kina Kinana, kina Kikwete ametumbuliwa amerudi kitaani na hapa ndipo anawakumbusha vijana kuwa wanapopewa madaraka wasijisahau na kudhani watakaa madarakani milele kwani madaraka ni kama koti la kuazima tu ipo siku mwenye koti lake atalichukua

View attachment 2309125
Hivi kwanza Heri James yuko wapi?
 
Pamona na hayo!.

Happy hapo alipo anaenda kusimamia mamiradi yake na kamwe hutakutana nae mkiwa mmeshika bomba za kwenye daladala
Alishindwa kusimamia mamiradi akiwa RC?😀😀
 
ni utashi wa anayeteua kumpa mtu nafasi au la kutokana na utaratibu na mipango yake, mbona kuna kuna watu kibao waliongea mambo mengi na wapo kwa nafasi kubwa?

Tumuache jamaa wa watu hizi tabia za utabiri utabiri na ramli tuachie wanaowezana nao, nchi haiwezi kwenda kwa tabia za kuunganisha matukio kwa kubahatisha bahatisha. Ni aina ya umaskini wa mawazo!
Ujumbe wa mwandishi umekugusa sana. Pole
 
Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa ambapo tumeshuhudia baadhi ya sura mpya, wengine wakihamishwa lakini kuna ambao wamepewa mkono wa kwaheri, ingawa gumzo kubwa limekuwa kutemwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi.

Hapi ambaye amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baadae kuhamishiwa Mara anakumbukwa kwa matendo yake yenye ukakasi, vitisho, na matumizi yanaonekana kuwa mabovu ya madaraka katika sehemu alizohudumu.

Hapi ambaye wengi wanamtazama kama taswira ya vijana waliopewa dhamana na wakizidiwa uwezo na kushindwa kuyadhibiti maneno na matendo yao, anaingia kwenye kundi la vijana waliolewa madaraka na sasa wanarudi mtaani kama ilivyokuwa kwa Bwana Paul Makonda na Lengai Sabaya ambaye anapambana na kesi katika mahakama ya Tanzania.

Hapi huyu ndiye aliwachimba mkwara wazee, wastaafu akiwaambia waache kuwashwawashwa na popote watakapojitokeza atawatangwa, na kama kuna maovu walitenda watubu na wasituharibie Nchi yetu ya Tanzamia.
Aliwataka wastaafu Wastaafu wakae kimya kwani zama zao zimepita, wasituharibie nchi yetu wasimpotezee focus Rais MAGUFULI.

Aliwahi kumwambia mtumishi wa idara ya Ardhi huko Iringa kuwa asimchezee hata kidogo kwani yeye ni mtu hatari sana, sasa yule mtu hatari aliyewatisha kina Kinana, kina Kikwete ametumbuliwa amerudi kitaani na hapa ndipo anawakumbusha vijana kuwa wanapopewa madaraka wasijisahau na kudhani watakaa madarakani milele kwani madaraka ni kama koti la kuazima tu ipo siku mwenye koti lake atalichukua

View attachment 2309125
Koti la kuazima halina noma yeyote.

Ulaya ukiwa na shughuli maalum unaenda ku renti taxedo, koti la kuazima.

Koti likiwa la kwako mwenyewe ukawa unalirudia rudia pia ni umbwiga...
 
Back
Top Bottom