Miongoni mwa mashaur mepesi yaliyopelekwa TFF ni hili swala uvunjaj mkataba wa feisal salum, watu wengi wanachanganya kati ya breach of contract na termination of contract, breach of contract ni ukiukwaj wa mkataba kwa kutofuata masharti ya mkataba wakati termination of contract pamoja na tafsir zingne ila ni ufikaj tamat wa mkataba kwa maridhiano ya pande mbili au kwa kufuata masharti ya mkataba.
Kwa kuwa feisal hakufuata mkataba kwa maana alivunja bila ya kufuata masharti yake,(breach of contract) kisheria kuna (remedies)matokeo 3 iwapo kuna upande mmoja umevunja mkataba pasipo halali kwayo ni-
1. Compensation/upande uliovunja mkataba isivyo halali unaweza kutakiwa kulipa fidia kwa madhara ambayo ameyasababisha kwa upande wa mbili
2. Specific performance, upande kosaji unaweza kuelekezwa kuwa utekeleze kitu fulani kwa lazima, na mamlaka iliyo na uwezo wa kimaamuzi kilichopo ndani ya mkataba au nje ya mkataba kama sehemu ya adhabu,mara nying utekelezwaj wa hili huja baada ya kushndwa kwa upande kosaj kulipa fidia.
3. Injuction (zuio)-upande kosaj halikadhalika unaweza kuzuiwa usifanye kitu fulani kama adhabu na mamlaka yenye uwezo wa kuamua shauri husika kisheria.kama adhabu .
Kwa scenario ya feisal hapa bila shaka litafanyika swala moja au 2 nalo ni injuction, kwa maana ya zuio la yeye asiondoke na ni bado mchezaj wa yanga, simuoni akilipa fidia, zaidi ya kutakiwa kuitumikia yanga mpaka mwisho wa mkataba wake.
Nini yanga wafanye.?
kwa kuwa mchezaji mapenzi na yanga yameisha, ni ngumu kumlazimisha acheze kwa jitihada 100% ,na yanga walichokuwa wanapigania hapa ni kulinda status yao ya mchezaj kutokuondoka kirahisi, hvyo yanga wanaweza kuamua kumuuza kwa timu inayomtaka kwa timu hyo kufuata utaratibu wa kuwasiliana na yanga kwa kuwa mchezaj ana mkataba bado na mwajiri wake ambae ni yanga,pili yanga wanaweza kuendelea kumtumia kikosin mpk mkataba wake uishe na kisha aondoke bure.
Katika kuamua hili swala busara kubwa sana inatakiwa kwa pande zote mbili kujishusha hasa upande wa fei ni lazima waombe msamaha vingnevyo wanaweza kufanyiwa siasa za mpira kuumizwa, ili njia nyingne ifunguke ya kuweza kuondoka na kuwa huru lazima ajishushe na aombe radhi.
NB: Wachezaj lazima wajifunze kusoma na kuelewa vifungu vyote vya kisheria wakati wa kusaini mkatba,na kama hawana uhakika na kesho yao ni vyema wakasaini mikataba ya muda mfupi, na kuwa na wanasheria.
Pia wadau wote lazima wajue mashaur ya namna hii ambayo yatafungua mlango ambao sio mzur kwa uondokaj wa wachezaj katika vilabu vyao kamwe T.F.F hawawez kuukubali kuufungua kwani utakuja kuwatesa mbeleni na kuvitesa vilabu vyetu.
Ambacho nimejifunza watu wengi mapenzi kwa vilabu vyao/vyetu yanaathiri uwezo wa kufikiria.